Serikali yafanikisha Wajawazito kupimwa vipimo vya awali bure

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inazidi kuboresha huduma za afya kwa wananchi na kuanzia sasa akina mama wajawazito wanaofika kwenye kliniki za uzazi na zile za mama na mtoto kupimwa vipimo vya uwingi wa damu, mkojo, kuangalia uwingi wa protini, shinikizo la damu pamoja na kusikiliza mapigo ya moyo ya mtoto kwamba huduma hizo kwasasa zitatolewa bila malipo nchi nzima.

Uamuzi huo wa Serikali ya Rais Samia umetangazwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu mkoani Dodoma wiki hii wakati akikabidhi vifaa tiba vya kuboresha huduma za afya ya uzazi kwa halmashauri za mkoa wa Dodoma.

Waziri Ummy amesema vipimo hivyo ni muhimu sana kwa mama mjamzito ili kuepusha kifafa cha mimba na vifo kwa wajawazito na ndiyo maana Serikali ya Rais Samia imeona kuanzia sasa vipimo hivyo viwe bila malipo kwa wajawazito.

Waziri Ummy kwenye mkutano huo aliwasisitiza watoa huduma za afya kote nchini kufanya kazi kwa weledi mkubwa kusaidia wananchi kwani Rais Samia Suluhu Hassan ameshatimiza wajibu wake kwa kujenga majengo, maboresho ya miundombinu, kuongeza ajira na kuongeza fedha za dawa mpaka bilioni 20 kila mwezi.

1217243002.jpg
392194150.jpg
626019799.jpg
-649003152.jpg
-73405235.jpg
1167533478.jpg
1317016110.jpg
1988710135.jpg
-279698744.jpg
1341268017.jpg
 
Back
Top Bottom