Hali ya sintofahamu imeendelea kuwakumba vijana wa vyuo vikuu ambao bado hawajapata pesa zao ambazo walitegemea kupata katikati ya mwezi wa 5, ikumbukwe kwamba wiki iliyopita bodi ya mikopo vyuo vikuu (Heslb) ilitoa tamko kwamba wiki hii vijana hao wangepata pesa yao lakini mpaka sasa hawajapata pesa hizo na kila wakifuatilia wanaambiwa bodi hawajatuma pesa.
Hali hii imesababisha wanafunzi wengi kuishi kwa hofu kutokana na madeni huku wengine wakifukuzwa kwenye vyumba walivyokuwa wamepanga, vilevile kuna baadhi ya vyuo vimewazuia wanafunzi wake kufanya mitihani inayoanza wiki ijayo kwa kigezo cha kushindwa kulipa ada, ieleweke kwamba wanafunzi hao walikuwa wanajilipia ada kutokana na pesa wanazopata toka bodi ya mikopo.