Serikali yaajiri walimu hewa(?) Ushahidi huu hapa...

Hujapata hata "LIKE" moja!! Sijui kwa nini
 
Kama Namuona Huyo Bujibuji S3283/0132
 
Kwa hili waziri Jafo na watu wake wahusika 100%. Haiwezekani ukae na data muda mrefu namna ile uje na huu upuuzi. Kuna mtoto/ndugu wa Gerson Msigwa kamaliza kidato cha nne 1994(miaka ishirini na tano iliyopita). Lakini kaajiriwa wameacha kijana aliyena umri wa miaka 24-30 kwa manufaa ya taifa. Wao wanafuata maelezo kutoka juu(vimemo). Aibu hii ni ya Jaffo!!!
 
MnHh...!!!??

Watu wafukunyuku balaa...!!!

Sasa tunaelekea wapi...!!!??

Basi kuna maupendeleo huko. Mbaya sana hii..
 
Huu uzi inabidi mods muufikishe kwa wahusika maana evidence zipo au wanasiasa waingilie kati
 
Kwa hiyo unataka kushindana na chato? Kwani mbarali walipewa intaneshino eapoti? Benki ya gorofa? Taa za "njiani"? Utapata tabu sana
Mkuu kuna makosa mengi sana yamejitokeza kwenye kupanga walimu wapya sijajua ni uharaka au nini? kuna shule za msingi zingine zimekosa walimu kabisa japo kuna hitaji kubwa sana cha kushangaza kuna shule moja huko Rorya wamepewa walimu wa shule ya msingi 9. Haya ni maajabu ya dunia.
 
Vipi documents mtu kahitimu 1994, huku majina yanafanana number za mwisho zitofautiane, Ku create majina tifauti hakufanyi hyo issue itokee
Kama mtu kamaliza form 4 mwaka 1994
Tukichukua kama alianza na miaka 7 (vigumu sana miaka hii kuanza shule umri huo) akamaliza na miaka 17+ 25 (ukihesabu mwaka huo hadi 2019)= 42 ambapo kikanuni maximum age kuajiriwa ajira ya kudumu ni 45 serikalini ajira za kawaida.. Sasa jamaa atafanya miaka 15 au 17 tu anakula kikokotoo.
Maisha kweli hayana formula.
 
Mkuu ni masikitiko halafu kuna kitu kingine watu hawajakiona watu waliopata kazi asilimia kubwa ni watu wenye majina ya kanda ya ziwa niko na list kuna majina ya kisukuma zaid ya 500 yanayoonekana ....

Kwa sababu mm natoka uko na majina nayajua
Kama mtu anabisha atafute majina Yale yale 4500 waone maajabu mengine ya Serikali ya CCM na ukabila....
 
Hakuna umakini kabisa period!! Unakuwa kama unatetea hapa!! Soma vizuri hii post ya huyu Great Thinker of the year, idadi ya walioajiriwa ni hewa!!!
Atakuwa pale utumishi uyo anatetea kazi yake
 
Huku waziri wa ulinzi katimuliwa na waziri mkuu UK
Sasa hebu tuone huko nani atatimuliwa kwa msala huu
 
.
Hakuna cha makosa ya kibinadamu hapa. Huu ni UFISADI.
Hapana mkuu mimi naona ni makosa ya kiuandishi ndio maana hata idadi ya watu kujirudia siyo kubwa na hili lili wahi tokea tena hata kwa miaka ya nyuma...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…