Serikali ya Tanzania yataka majibu ya corona ndani ya saa 24

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi ameuagiza Uongozi wa Maabara ya taifa ya Afya ya Jamii kutoa majibu ya sampuli za Ugonjwa wa Covid-19 ndani ya saa 24, badala ya saa 72 kwa hospitali zinazopeleka Sampuli hizo au kwa wananchi wanaojitokeza kupima ugonjwa huo kwa nia ya kutaka kusafiri nje ya nchi, ili kuondokana na malalamiko ambayo yamekuwa yakielekezwa kwa maabara hiyo kuwa kuna ucheleweshaji mkubwa wa majibu ya vipimo hivyo.

Mganga Mkuu wa Serikali ametoa agizo hilo leo wakati akizungumza na Uongozi wa Maabara hiyo, Waganga wakuu na wasimamizi wa Maabara kutoka Hospital za Rufaa za Serikali na za Binafsi kutoka mkoa wa Dar es salaam mara baada ya kufanya ziara katika Maabara Kuu ya Taifa ya Afya ya jamii, kujadili namna ya kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili maabara hiyo.

Prof. Makubi amesema pamoja na kuweka mifumo mizuri katika maabara hiyo lakini bado kumekuwepo na malalamiko wanayapokea kutoka kwenye baadhi ya Hospitali na hata kwa wasafiri wanaofika katika maabara hiyo kwa ajili ya kufanyiwa vipimo, ucheleweshaji ambao umekuwa kero kwa wananchi hao na kamwe hautaweza kuvumiliwa.

“Tafuteni njia mtakayofanya ila hakikisheni kuanzia sasa majibu yote ya Covid-19 yanatolewa ndani ya saa 24 kwa wale wote watakaofanyiwa vipimo kwa Dar es salam na masaa 48 kwa mikoani, na lazima suala hili lisimamiwe na wasimamizi wote wa maabara zinazohusika ili kuhakikisha kero hii inaondolewa” Alisema Prof. Makubi .

Aidha mfumo wa kufatilia vipimo na majibu kati ya Maabara kuu na Hospitali lazima uboreshwe na kufanyiwa tathimini kila wakati na kila msimamizi atimize wajibu wake bila kuchelewesha. Katika hili Prof.Makubi ameutaka uongozi huo kulisimamia kisawa sawa jambo hili na kuhakikisha unaweka mfumo mzuri ambao utaweza kuzifuatilia sampuli zote za Covid-19 ambazo zitafika katika maabara hiyo kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.

Katika Hatua nyingine Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi ameshangazwa na Kitendo cha kupotea kwa baadhi ya sampuli za Covid-19 ambazo zimekuwa zikifikishwa katika maabara hiyo kwa ajili ya kufanyiwa vipimo, na kushindwa kuelewa inakuwaje sampuli hizo zinapotea na kulazimika kurudiwa , tena kwenye maabara kuu ya taifa ambayo inategemewa na maabara nyingine.
 
Maneenerr...
Kuna uzi ulikuja juzi hapa. Hakuna kima itavuka boda bila kuwA cleared Covid Free...

Lets see where this is gonna take us..
 
Ukiona serikali ishaanza kutaja taja hili neno Covid-19 mara nyingi hivi,ujue kuna mfumuko ushaanza pahala

Wanaanza stori stori hizi kujenga uhalali...

I smell a lie here

Kuna mfumuko ushaanza

Hapa sasa walowafanya wakubali Covid ipo watawaita Mabeberu..😂😂

Kesho watawaita.. 😂😂!??

Ikija misaada..
 
By clouds Media kupitia twitter:

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi ameuagiza uongozi wa Maabara ya Taifa kutoa majibu ya sampuli za ugonjwa wa Covid-19 ndani ya saa 24, badala ya masaa 72 kwa hospitali zinazopeleka sampuli au kwa wananchi wanaojitokeza kupima ugonjwa huo kwa nia ya kusafiri nje ya nchi

1608998819343.png
 
By clouds Media kupitia twitter:

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi ameuagiza uongozi wa Maabara ya Taifa kutoa majibu ya sampuli za ugonjwa wa Covid-19 ndani ya saa 24, badala ya masaa 72 kwa hospitali zinazopeleka sampuli au kwa wananchi wanaojitokeza kupima ugonjwa huo kwa nia ya kusafiri nje ya nchi
Mbona wanatoa ndani ya 24 hrs mimi nimepata hiyo huduma hivi karibuni
 
Mbona jana huyo anayejiita mwendawazimu alidai Tanzania tumenusurika hakuna COVID19 Nchini? Ama kweli mficha ugonjwa kifo kitamuumbua.
By clouds Media kupitia twitter:

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi ameuagiza uongozi wa Maabara ya Taifa kutoa majibu ya sampuli za ugonjwa wa Covid-19 ndani ya saa 24, badala ya masaa 72 kwa hospitali zinazopeleka sampuli au kwa wananchi wanaojitokeza kupima ugonjwa huo kwa nia ya kusafiri nje ya nchi
 
Back
Top Bottom