Serikali ya Tanzania yaanza mchakato wa kuunda Satelaiti yake

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Serikali imesema inatambua umuhimu wa nchi kuwa na satelaiti na kwamba katika mwaka huu wa fedha imeanza kuandaa utaratibu wa awali utakaowezesha kuunda na kurusha satelaiti yake angani.

Aidha, imesema ili kuwezesha kufikia azma hiyo tayari imeunda andiko dhana na kuunda timu ya watalaamu watakaoshauri aina ya satelaiti itakayorushwa angani itakayoendana na mahitaji halisi ya nchi.

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Mathew Kundo amesema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Bahi, Kenneth Nollo aliyetaka kujua ni lini Serikali itaanza programu ya kuunda na kurusha setelaiti angani.

“Ni matarajio kuwa timu hiyo itakamilisha kazi ya uchambuzi na kuwasilisha mapendekezo yake Serikalini kwa hatua za kimaamuzi ndani ya mwaka huu wa fedha,” amesema Kundo

Akizungumzia kwa upande wa Afrika, Kundo amesema kuwa hadi sasa Afrika ina jumla ya satelaiti 41, na kuanzia mwaka 2016 ni satelaiti 20 tu ambazo zimekuwa angani, na kati ya hizio 41 ni tisa tu ambazo zimetengenezwa na zina taswira ya Kiafrika.
 
Isiwe ni kwa nia ya kuonekana kama na sisi tumo baada ya Rwanda Kenya Nigeria na Angola kufanya hivyo. Kwa nini tusiimarishe mifumo yetu ya ardhini kwanza kabla ya kupapatikia mambo ya satellite?

Kwenye IT tuko nyuma kweli kweli, hiyo satellite 🛰️ tutaimudu? 🤔
 
Isiwe ni kwa nia ya kuonekana kama na sisi tumo baada ya Rwanda Kenya Nigeria na Angola kufanya hivyo. Kwa nini tusiimarishe mifumo yeti ya ardhini kwanza kabla ya kupapatikia mambo ya satellite?... Kwenye IT tuko nyuma kweli kweli, hiyo satellite 🛰️ tutaimudu? 🤔
Kwenye it tuko nyuma ya nani!?..umepomaje kwamba tuko nyuma?!..unavyoelewa wewe it ni nini!?
 
Satellite inaweza punguza gharama za mawasiliano.

Tunaponda serikali kuanza mchakato.

Na tunalia gharama za bando.

Satellite inaweza saidia Hali ya hewa.

Tunaponda serikali kutojiandaa na ukame na tunaponda tukisikia imeanza mchakato wa satellite.

Mradi kazi yetu kuponda kila kitu...
 
Sisi ni Taifa bandia lisilojielewa, ambalo likisikia tu Taifa fulani wanafanya, basi na sisi ili tuonekane ni Taifa, tunasema tutafanya bila hata kujua ni nini hicho ambacho hilo Taifa linalofanya linatarajia kupata kutoka kwenye jambo hilo.

Kufanya tu uchaguzi wa viongozi tumeshindwa, kuitoa tu ndege kutoka ufukweni mwa ziwa ili kuwaokoa wenzetu waliokwama ndani ya ndege tumeshindwa. Hata kuitoboa tu ndege ili waliomo wapate hewa tumeshindwa, halafu tunaongelea satellite kwa vile tu tumesikia kuna kitu kinaitwa satellite. Hawa watawala wetu hata ukiwauliza satellite nui nini, nina hakika hakuna hata anayeelewa.
 
Satellite inaweza punguza gharama za mawasiliano ..
Tunaponda serikali kuanza mchakato
Na tunalia gharama za bando...
Satellite inaweza saidia Hali ya hewa..
Tunaponda serikali kutojiandaa na ukame na tunaponda tukisikia imeanza mchakato wa satellite....

Mradi kazi yetu kuponda kila kitu...
Nikiukumbuka mkongo wa taifa ya motto yake nabaki kucheka tu😃
 
Satellite inaweza punguza gharama za mawasiliano ..
Tunaponda serikali kuanza mchakato
Na tunalia gharama za bando...
Satellite inaweza saidia Hali ya hewa..
Tunaponda serikali kutojiandaa na ukame na tunaponda tukisikia imeanza mchakato wa satellite....

Mradi kazi yetu kuponda kila kitu...
Hivi kwenye bomba la gesi mlisemaje kuhusu umeme??

Mjinga tu ndiye atakaye amini unayoyasema.

#MaendeleoHayanaChama
 
Miradi mikubwa kama ya kuunda satellites huwa ina multplier effects kibao kwenye sekta mbalimbali. Hembu fikiria ajira zitakazotengenezwa za vijana wa fizikia, electronics, computer science, mechanics, IT, electrical technicians kuhakikisha satellite inaenda angani.

Embu fikiria startups za IT zitakazozaliwa baada ya vijana kupata uzoefu kutokana na megaproject kama hiyo! Sema tu sina uhakika kama serikali hii ina watawala wenye guts za kuhakikisha kitu kama hicho kinatekelezeka. Kumbikumbi tu.
 
Back
Top Bottom