Tanzania kujenga satelaiti yake

Donnie Charlie

JF-Expert Member
Sep 16, 2009
15,167
16,257

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali yake imeanza mazungumzo kwa ajili ya ujenzi wa satelite.​

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Mei 18, 2023 katika uzinduzi wa mradi wa minara ya kurusha matangazo ya Televisheni ardhini (DTT) inayomilikiwa na kampuni ya Azam Media Limited.

Endapo mpango huo utakuwa dhahiri, Tanzania itakuwa miongoni mwa nchi za Afrika zilizofanikiwa kupeleka kifaa hicho angani, ambazo ni Algeria, Ethiopia, Kenya, Zimbabwe, Afrika Kusini, Morocco, Misri, Ghana na Nigeria, huku Rwanda ikikusudia kufanya hivyo mwishoni mwa mwaka huu.

Hata hivyo, Rais Samia ameoneka kutofurahia ujenzi wa minara ya mawasiliano unaoendela nchini huku akishauri kuangaliwe namna bora ambayo kwayo nchi inaweza kukusanya mambo yote kwa pamoja bila kuwa na mambo mengi.

"Tatizo nililonalo kichwani kwangu ni moja, nikamuambia Waziri, minara 758 mipya, kuna minara ambayo tayari ipo ndani ya nchi, kuna minara ya Azam Media itakwenda kujengwa na wengine watakuja na minara," amesema.

Kwa mujibu wa Rais Samia, hali hiyo ya uwepo wa minara mingi ilimfanya kumhoji Waziri mhusika ili kujua kama kunawezakuwa na teknolojia mbadala.

"Nikamuuliza Waziri hakuna teknolojia ya kuchanganya haya yote yakaingia sehemu moja, kwa sababu nchi yote itajaa minara, kila utakapokwenda minara, minara, ukiuliza huu wa wa Azam, Tigo na huu wa Voda, nchi yote itajaa minara," amehoji Rais Samia.

Amesema ni vyema kama nchi ikatafuta teknolojia itakayoweza kuchanganya vyote kwa pamoja.
Akiuthibitishia umma, Rais Amesema: “Najua kama Serikali tunajipanga kuja na setelaiti ambayo niwahakikishie kuwa itakuwepo Tanzania, tunajipanga vizuri tumeanza mazungumzo tutajenga setelaiti Tanzania.”

Amesema wakati hilo likifanyika ni vyema kuangalia namna ya kukusanya mambo yote na nchi ikapata huduma zote kwa moja bila ya kuwa na mambo mengi yamesimama.
 
Tukipeleka satellite mwezini, wakenya watatukoma.
Sio ya kwenda mwezini. Satellite kwenda mwezini ni jambo la starehe na sifa.

Hapo anazungumzia satellite kwa ajili ya mawasiliano ya simu, matangazo ya radio na televisheni, usalama, telemedicine, GPS, ramani, location, research and education, utabiri wa hali ya hewa na mambo kama hayo ya msingi.
 
Sorry mkuu nilikua fasta sana, nilitaka niandike space.
 
"Nikamuuliza Waziri hakuna teknolojia ya kuchanganya haya yote yakaingia sehemu moja, kwa sababu nchi yote itajaa minara, kila utakapokwenda minara, minara, ukiuliza huu wa wa Azam, Tigo na huu wa Voda, nchi yote itajaa minara," amehoji Rais Samia.
Kikubwa zaidi anachokijua Waziri kwenye teknolojia ni kupakua tweeter na youtube basi, ukienda zaidi umemchanganya
 
Sio ya kwenda mwezini. Satellite kwenda mwezini ni jambo la starehe na sifa.

Hapo anazungumzia satellite kwa ajili ya mawasiliano ya simu, matangazo ya radio na televisheni, usalama, telemedicine, GPS, ramani, location, research and education, utabiri wa hali ya hewa na mambo kama hayo ya msingi.
🤣🤣🤣
 
Idadi ya minara inayojengwa voda, tigo, airtel, halotel, azam, ni sawa na idadi ya vitambulisho Tanzania: NIDA, NHIF, CRDB, NBC, NMB, driving licence, etc.

The worst part of it, zingine hazitambuliki kabisa unapotaka kufanya application fulani.
 
Hayo makampuni ya simu kwa kutumia minara tu gharama ndio hizi kila siku ni kelele,sembuse kwenye satellite?!!duniani kote minara ya simu inatumika sana,kwani faida yake ni kubwa sana.Kuna simu hapa Tz sijui kama bado zipo THURAYA,zilikuwa zinatumia satellite,bei yake sio mchezo!!
 
Back
Top Bottom