Serikali ya Tanzania na Ubaguzi kwa Watumia Dawa za Kulevya na Madawa ya Kulevya

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,739
4,732
Sakata la Dawa za Kulevya katika nchi hii kwa sasa limeshika kasi ya Ajabu na kuifanya Tanzania kuogopwa na Nchi karibia Zote duniani na kufanya kila kitu chenye kuonyesha kina Nembo au asili ya Tanzania kuchunguzwa kwa makini sana.
Kwa leo mada yangu inajikita katika Ubaguzi unaoonyeshwa na Serikali yetu Juu ya watumiaji wa Madawa haya na Madawa yenyewe.

1. Kwa upande wa watumiaji tumeshuhudia kila siku wale Wavuta Bangi (Malijuana) wakikamatwa na kuitwa wahuni na kuhukumiwa vifungo mbalimbali katika mahakama zetu lakini wale watumiaji wa Cocain, Mandrax, Heroin wanaitwa ni wagonjwa na wameanzishiwa taasisi kwa ajili ya kwenda kupatiwa matibabu ya Bure ili waondokane na utumiaji huo Mifano hao ipo kwa wasanii Ray C, Q.Chilla, M2THEP aliyeugua kwa madawa hayo nusu ya kufa kule South Africa na wengine wengi.

2. Kinachonishangaza kwa Serikali yetu kuwaacha hawa watumiaji wa Madawa haya ya Mandrax, Heroin na Cocain bila kuwachukulia hatua yeyote huku sheria inasema wazi wauzaji na watumiaji wote ni watuhumiwa na kichekesho kilitokea pale walipokwenda Ikulu yetu Ambayo tunapaita patakatifu na kukutana na Mh. Rais huku wakionekana eti ni Mashujaa.

3. Kwa upande wa Madawa yenyewe tumeshuhudia kila siku Bangi ikikamatwa inachomwa hadharani iwe kwenye mashamba au iliyofungwa tayari lakini cha ajabu kwa haya madawa mengine (Cocain, Mandrax ,Heroin ) Tangu nizaliwe sijawahi kuona wala kusikia kuwa yameteketezwa nabaki najiuliza huwa yanapelekwa wapi? na kama yamehifadhiwa yamehifadhiwa wapi kwani kwa orodha iliyotolewa na kitengo cha udhibiti wa Madawa ya kulevya hapa nchini kwa kipindi chote kilichopita ni Tani kadhaa zimeishakamatwa lakini hatujui zilipo na hata kesi zenyewe hazijulikani pia kama kweli wahusika waliokamatwa wamefungwa au vipi.

Nawasilisha Hoja.
 
kinachosikitisha ni kwamba majina ya wauza unga kikwete ambaye ndie rais wa nchi anayo sasa kwa kukaa kimya kwake watu wakisema anawaogopa waaitwa wachochezi?....poor Tanzania
 
Tokea nimepata ufahamu hapa sijawahi kusikia madawa haya kuteketezwa ama kuharibiwa,HUWA YANAPELEKWA WAPI??? SERIKALI NJOONI MSEME MADAWA HAYA YAKO WAPI NA YANATUNZWA ILI HATMA YAKE IWE NINI???
 
Back
Top Bottom