Kiboko ya Jiwe
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 12,705
- 36,158
Baada ya kuweka juhudi za kuzuia ujangiri awamu ya Kikwete mpaka utawala wa Magufuli tembo waliongezeka sana kwenye pori la akiba la Selous na mapori mengine hapa nchini.
Juhudi za kuzuia na kupambana na ujangiri zinaendelea kuimarika hata Sasa. Tembo wameongezeka mara dufu. Wilaya ya Tunduru, Liwale na wilaya zingine za kusini tembo mpaka mjini wanafika. Wijijini Sasa wamekuwa kama mbuzi, wanazurura tu.
Watu wanakufa sana, hata leo kazikwa mjomba wangu huko Liwale Kijiji cha Mtawango kauliwa na tembo. Kwanini serikali isiwavune na kuuza nyama zao au hata kugawa Bure? Walaji tuko wengi mbona. Au iwauze nje, itangaze mnada kupunguza hili wimbi.
Miaka inaenda watu wanakufa, mazao yao yanaliwa na kuishia kupewa fidia za kiwendawazimu. Mtu auawe kwa uzembe wa serikali kisha familia yake muitulize kwa millioni 1. Hii ni sawa? Mbona mtu akikutwa na meno ya tembo anapigiwa thamani kubwa sana. Anafungwa m3ka mpaka 50 na faini juu?
Mtanzania maskini hana thamani kiasi hichi?