Serikali ya Rais Samia inavyotekeleza huduma za Maji

Serikali ya Rais Samia inavyotekeleza huduma za Maji

kalacha mateo

Senior Member
Joined
Sep 27, 2021
Posts
122
Reaction score
241
Watumiaji wa huduma za Maji nchini moja kati ya kero zao ilikua ni kuhusu ubambikaji wa bili za maji kwa wananchi, Miongoni mwa maagizo aliyowahi kutoa Rais Samia Suluhu ni pamoja na uharakishwaji wa uwepo wa mita za malipo ya kabla kwa watumiaji wa maji nchini.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya, CPA Gilbert Kayange amesema baada ya majaribio ya muda mrefu sasa wameanza utekelezaji na tayari wateja 713 wameanza kuunganishiwa mita za malipo ya kabla (LUMAKU).

Mpango wa serikali ni wananchi wote wafungiwe mita za LUMAKU ili kupunguza changamoto zinazojitokeza kwa watumiaji wa maji hususani kwenye usomaji na ulipaji wa bili za maji.
 
Back
Top Bottom