Serikali ya Rais Magufuli inatisha, vinara wa IPTL hawakupata hata ‘tip-off’!

E
Unasema vyombo vya habari havikujua mpaka Valentino alipo tangaza siku ya tatu? Unataka kusema pia na familia zao hazikujua wako wapi sio?

Seth umesema amekamatwa akiwa na mkewe.. Kwani huyo mwanamke alishindwa kusema kama angeamua?
Elewa mada na wewe.Vyombo vya habari havikujua chochote Hata kama Mke alikuwa anajua kwani Mke ni chombo cha habari?

Na vyombo vinavyopenda kuandika habari za mbele kwa hilo vingeshaandika tu lakini mtoa mada anasema toka akamatwe jmosi mpaka jtatu alipopelekwa mahakamani hakuna chombo chochote kilichokuwa kinajua hiyo habari ndiyo usiri wa kazi kwa Serikali ya Dr John Magufuli anao usemea mtoa mada.
 
Kwa kweli usiri uliofanyika hapo ni mkubwa na ndivyo inavyotakiwa. Ila sasa wewe mleta mada ulijuaje yote hayo kwamba kuna makachero walikua wanamfuatilia wakati anaelekea airport? Au ndo unatoa siri za ofisi yenu!!!
Hakuna siri ya watu wawili
 
Kwa muda wote Harbinder Singh Sethi na James Rugemalira hawakugundua kuwa vyombo vya usalama vinawachunguza na wako mbioni kukamatwa na kupelekwa mahakamani.
Ni uchunguzi gani waliokuwa wanafanyiwa wakati uchunguzi ulishafanyika tangu serekali ya JK na ikabainika kuwa wao ndio wahusika na baadhi yao walishachukuliwa hatua za kuvuliwa nyazifa zao kwa tuhuma hizo,kilichokuwa kinasubiriwa ni kuondolewa kinga ya mtu aliyekuwa ana walinda wasikamatwe na kupelekwa Mahakamani.

Knga ambayo imeondolewa na Magufuli,pia Siku ambayo Mlowola alipoteuliwa kushika wadhifa wake mpya aliweka wazi kabisa kuwa watuhumiwa wote mapapa pamoja na wa ESCROW atawakamata na kuwafikisha Mahakamani,kwa hiyo watuhumiwa walikuwa wanajua mambo yote yanayoendelea kwa kuwa pia kabla ya kufikishwa Mahakamani ni lazima kwanza uhojiwe kwanza na unapohojiwa unatakiwa uwe na Wakili wako au Ndugu yako wa karibu japokuwa siyo lazima,ila kulingana na unyeti wa kesi yenyewe watuhumiwa wasingekubali kuhojiwa bila kuwepo wanasheria wao na ndugu zao wa karibu.

Kwa hali ya kufanya mahojiano mbele ya wanasheria wako na ndugu zako wa karibu hata kama ni Siri ya namna gani ni lazima itavuja,tena ukishaambiwa uwaite wanasheria wako na ndugu wawepo kwenye mahojiano hiyo siyo Siri tena na ni kitu ambacho kisheria hakikwepeki na utajua Tu,kuwa leo utapelekwa Mahakamani na utanyimwa dhamana kwa kuwa makosa ya kudhamiwa yanajulikana na yasiyo na dhamana yanajulikana,isitoshe mwanasheria wako anakuwa ameshakujulisha kila kitu.
 
Unasema vyombo vya habari havikujua mpaka Valentino alipo tangaza siku ya tatu? Unataka kusema pia na familia zao hazikujua wako wapi sio?

Seth umesema amekamatwa akiwa na mkewe.. Kwani huyo mwanamke alishindwa kusema kama angeamua?
Unafikiri kusema ni suala la kuamua tu basi unasema?
 
Kwa muda wote Harbinder Singh Sethi na James Rugemalira hawakugundua kuwa vyombo vya usalama vinawachunguza na wako mbioni kukamatwa na kupelekwa mahakamani.

Vyombo vya usalama wa Taifa vilikuwa vinafuatilia nyendo zao kwa karibu wakati wao hawakufahamu pamoja na kuwa wana mtandao mkubwa ndani na nje ya nchi.

Harbinder Singh Sethi hakufahamu kuna makachero walikuwa wanamfuata nyuma mpaka Airport na alipotaka kupanda ndege ndipo wakamkamata.

Vyombo vya habari havikunusa habari ya Harbinder Singh Sethi na James Rugemalira kukamatwa mpaka siku ambayo Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Valentino Mlowola alipotangaza kuwa wako mbioni kuwafikisha mahakamani. Hiyo ilikuwa ni siku ya tatu wakiwa mahabusu baada ya kukamatwa. Walikatamatwa Jumamosi Juni 17 na kufikishwa mahakamani Jumatatu Juni 19.

Mwenyekiti Mtendaji wa IPTL/PAP, Habinder Seth Sigh akiwa na mkewe Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam, alikamatwa wakiwa safarini kwenda Afrika Kusini ambako ndiko yaliko makazi yao.

Usiri wa sasa wa serikali ya Rais Magufuli unawafanya vigogo wenye kashfa mbali mbali kupatwa na wasiwasi kwa sababu hawafahamu kinachoendelea kuhusu hatima zao kisiasa na kibiashara.

Zama za siri za serikali kuvuja kwa urahisi zimeanza kutoweka na hii ni ishara nzuri kwa ustawi wa taifa hasa kwa nchi kama Tanzania ambayo kiwango cha utajiri wako wa pesa au kisiasa ndio kinakuwezesha usiguswe na mkono wa dola.

Unapowaona wafanyabiashara wakubwa kama Harbinder Singh Sethi na James Rugemalira wanapigishwa magoti kwa amri ya Warder/wardress wa Magereza lazima utajiuliza maswali magumu kuhusu hatima ya ufisadi nchini.

Mwingereza Leslie Bricusse ambaye ni mtunzi aliwahi kusema, “It's a new dawn, it's a new day, it's a new life, and I'm feeling good”.

DCsQSSzXUAIpoud.jpg:large
Huyu Rais ananibariki Sana. Mungu wangu ambariki mpaka dunia imtungie vitabu. Dunia isimame chini ya Rais Magufuli.
 
Good topic MsemajiUkweli,ila uelewe ni haki ya kikatiba ya kila mmoja wetu kupewa taarifa na vyombo vya usalama once wanapoanza kukuchunguza,na uelewe mpaka dakika hii hawa ni innocent hadi hapo mahakama itakapoamua kwa hiyo kitendo walichofanyiwa kama kupigwa picha before to appear in court of law ni makosa ,kuchuchumaa vile ni kuwadhalilisha,na hili si la kushangilia,we kuishi kwenye nchi inayozingatia haki za binadamu na sheria,ukivunja sheria kuna utaratibu wa kufuata sio kudhalilishana,and please kuna yeyote anayejua hili kama TAKUKURU wana uwezo wa to arrest na kumfungulia mashitaka mtuhumiwa,kwangu naona ni kazi ya polisi.
 
seth aliitwa aje asaini mkataba mpya wa iptl

Ndo ukisikia serikali ni walaghai first grade ndo kama hapo.

Katumwa chambo Ngalamgosi wa EWURA amvute Seth arudi bongo. Jamaaa akajua mambo yameshapoa. Anafika waziri mkuu anakula kichwa cha EWURA boss hajakaa vizuri anaona hii soo anataka kuteleza Airport anakutana na bangili za Mlowola

Hata yeye atakua haamini sinema waliyomchezea
 
Kwa muda wote Harbinder Singh Sethi na James Rugemalira hawakugundua kuwa vyombo vya usalama vinawachunguza na wako mbioni kukamatwa na kupelekwa mahakamani.

Vyombo vya usalama wa Taifa vilikuwa vinafuatilia nyendo zao kwa karibu wakati wao hawakufahamu pamoja na kuwa wana mtandao mkubwa ndani na nje ya nchi.

Harbinder Singh Sethi hakufahamu kuna makachero walikuwa wanamfuata nyuma mpaka Airport na alipotaka kupanda ndege ndipo wakamkamata.

Vyombo vya habari havikunusa habari ya Harbinder Singh Sethi na James Rugemalira kukamatwa mpaka siku ambayo Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Valentino Mlowola alipotangaza kuwa wako mbioni kuwafikisha mahakamani. Hiyo ilikuwa ni siku ya tatu wakiwa mahabusu baada ya kukamatwa. Walikatamatwa Jumamosi Juni 17 na kufikishwa mahakamani Jumatatu Juni 19.

Mwenyekiti Mtendaji wa IPTL/PAP, Habinder Seth Sigh akiwa na mkewe Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam, alikamatwa wakiwa safarini kwenda Afrika Kusini ambako ndiko yaliko makazi yao.

Usiri wa sasa wa serikali ya Rais Magufuli unawafanya vigogo wenye kashfa mbali mbali kupatwa na wasiwasi kwa sababu hawafahamu kinachoendelea kuhusu hatima zao kisiasa na kibiashara.

Zama za siri za serikali kuvuja kwa urahisi zimeanza kutoweka na hii ni ishara nzuri kwa ustawi wa taifa hasa kwa nchi kama Tanzania ambayo kiwango cha utajiri wako wa pesa au kisiasa ndio kinakuwezesha usiguswe na mkono wa dola.

Unapowaona wafanyabiashara wakubwa kama Harbinder Singh Sethi na James Rugemalira wanapigishwa magoti kwa amri ya Warder/wardress wa Magereza lazima utajiuliza maswali magumu kuhusu hatima ya ufisadi nchini.

Mwingereza Leslie Bricusse ambaye ni mtunzi aliwahi kusema, “It's a new dawn, it's a new day, it's a new life, and I'm feeling good”.

DCsQSSzXUAIpoud.jpg:large
I feel good too.May God bless our President.TISS heshima yake iliyokuwa imepotea inarudi pole pole.Mungu ibariki Tanzania.
 
Good topic MsemajiUkweli,ila uelewe ni haki ya kikatiba ya kila mmoja wetu kupewa taarifa na vyombo vya usalama once wanapoanza kukuchunguza,na uelewe mpaka dakika hii hawa ni innocent hadi hapo mahakama itakapoamua kwa hiyo kitendo walichofanyiwa kama kupigwa picha before to appear in court of law ni makosa ,kuchuchumaa vile ni kuwadhalilisha,na hili si la kushangilia,we kuishi kwenye nchi inayozingatia haki za binadamu na sheria,ukivunja sheria kuna utaratibu wa kufuata sio kudhalilishana,and please kuna yeyote anayejua hili kama TAKUKURU wana uwezo wa to arrest na kumfungulia mashitaka mtuhumiwa,kwangu naona ni kazi ya polisi.

Takukuru wana uwezo wa kuarrest na pia wana waendesha mashitaka wao/kufungua mashitaka ila wote TAKUKURU na Polisi wanapaswa wapate kibali cha DPP kufungua mashitaka.

Zamani waendesha mashitaka walikua wa Polisi pekee ila nadhani sasa hivi hata wake polisi wanakua chini ya DPP. Sijazunguka mahakamani siku nyingi

Ngoja tuombe msaada wa kaka msomi Petro E. Mselewa
 
Back
Top Bottom