Serikali ya Rais Magufuli inatisha, vinara wa IPTL hawakupata hata ‘tip-off’!

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,739
2,000
Kwa muda wote Harbinder Singh Sethi na James Rugemalira hawakugundua kuwa vyombo vya usalama vinawachunguza na wako mbioni kukamatwa na kupelekwa mahakamani.

Vyombo vya usalama wa Taifa vilikuwa vinafuatilia nyendo zao kwa karibu wakati wao hawakufahamu pamoja na kuwa wana mtandao mkubwa ndani na nje ya nchi.

Harbinder Singh Sethi hakufahamu kuna makachero walikuwa wanamfuata nyuma mpaka Airport na alipotaka kupanda ndege ndipo wakamkamata.

Vyombo vya habari havikunusa habari ya Harbinder Singh Sethi na James Rugemalira kukamatwa mpaka siku ambayo Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Valentino Mlowola alipotangaza kuwa wako mbioni kuwafikisha mahakamani. Hiyo ilikuwa ni siku ya tatu wakiwa mahabusu baada ya kukamatwa. Walikatamatwa Jumamosi Juni 17 na kufikishwa mahakamani Jumatatu Juni 19.

Mwenyekiti Mtendaji wa IPTL/PAP, Habinder Seth Sigh akiwa na mkewe Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam, alikamatwa wakiwa safarini kwenda Afrika Kusini ambako ndiko yaliko makazi yao.

Usiri wa sasa wa serikali ya Rais Magufuli unawafanya vigogo wenye kashfa mbali mbali kupatwa na wasiwasi kwa sababu hawafahamu kinachoendelea kuhusu hatima zao kisiasa na kibiashara.

Zama za siri za serikali kuvuja kwa urahisi zimeanza kutoweka na hii ni ishara nzuri kwa ustawi wa taifa hasa kwa nchi kama Tanzania ambayo kiwango cha utajiri wako wa pesa au kisiasa ndio kinakuwezesha usiguswe na mkono wa dola.

Unapowaona wafanyabiashara wakubwa kama Harbinder Singh Sethi na James Rugemalira wanapigishwa magoti kwa amri ya Warder/wardress wa Magereza lazima utajiuliza maswali magumu kuhusu hatima ya ufisadi nchini.

Mwingereza Leslie Bricusse ambaye ni mtunzi aliwahi kusema, “It's a new dawn, it's a new day, it's a new life, and I'm feeling good”.

DCsQSSzXUAIpoud.jpg:large
 
Miss Natafuta

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
23,490

seth aliitwa aje asaini mkataba mpya wa iptl
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
7,860
2,000
Usiri uko wapi hapo sasa,??? umeshatuambia Singasinga alikuwa anaelekea airport kupanda ndege kuelekea south anakoishi na sikwamba alikuwa anakimbia...kukamatwa kwa Singasinga na mwenzie sio kitu cha kushangaza maana tayari hata mtoto mdogo alikuwa anajua ni wahalifu wenye kinga ya CCM na serikali.

Watanzania tulikuwa tunashangaa kwa serikali kutotimiza majukumu yake siku zote, lakini sasa serikali imetimiza majukumu yake tena robo tu kulingana na makosa na chain ya wahusika kupongeza sio kazi yetu kwa serikali tena imechelewa kufanya kile tulichowatuma na kiapo walichoapa, pia ni jukumu letu wote kulalamika na kupaza sauti serikali ikishindwa kutimiza majukumu au kufanya kazi tofauti na kiapo..

Swali ile mitambo inayounguruma pale tegeta ni nani analipwa kwa sasa??..
Ni nani aliruhusu hawa jamaa kutuibia kwa kusaini nao mkataba wa hovyo??
Nani wanufaika wa iptl na tunawaadhibu vipi.
Ni nani alizuia hii mitambo isifanyiwe conversion from heavy oil fuel into gas??. na hii heavy oil fuel anaagiza nani? Gas is cheap than hiyo heavy oil fuel..
Tunafanyeje kuondokana na hili dude??- suluhu ni nini sasa??..
Tuna policy gani sasa itakayoilinda nchi na mikataba kama hii siku za usoni??....

Kazi ya vyombo vya usalama ni kuzuia taifa lisipate hasara na sio kukamata watu baada ya kutia hasara zitakazo lipwa na vizazi na vizazi..

Kijana jaribu kufikiri kwa manufaa ya taifa kwani
Tanzania ni moja ya nchi masikini kabisa duniani ambayo pato la mwanachi wake ni chini ya $1/day, zaidi ya 60% ya watu wake hawana Maji safi na salama, nk nk nk...matatizo ni mengi hapa hayawezi kutosha..
 
Graph

JF-Expert Member
Jul 20, 2016
2,742
2,000
Hamna kitu zaidi ya show tu, hawa ni wale sacrificial lambs, hizi double standards, bashite yupo karibu nayr kabisa haonekani pamoja na ukuda wote anaoufanya, marais wote waliopita hadi wamefungia gazeti miaka miwili. Yeye anaangalia urafiki?
Hamna kitu hapo zaidi ya misifa tu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom