Serikali ya Rais John Magufuli yathibitisha umahiri wake katika kupambana na corona na kuwalinda wananchi wake

Hivi kama muungwana,unashindwaje kusema maamuzi ya Raisi Magufuli ni ya akili kubwa?.Huku ni Ku appreciate alichotufanyia watanzania.Haishii kwenye maamuzi na mandalizi ni makubwa pia
 
Maamuzi ya Mh.Dk John Joseph Pombe Magufuli ni maamuzi magumu na ya kihistoria ambayo yatakumbukwa na vizazi vijavyo katika mchakato huu wa kupambana na virus vya COVID19. Tumeona mataifa menig yakifunga mipaka na kuzuia watu kutoka nje kwa kuwalinda raia wao wasipate maambukizi ya Corana. Nchi zilizotumia mbinu hizo nyingi ni zilizo endelea kiuchumi mfano USA na China. Kabla sjaendelea kuandika uzi wangu embu tujiulize , ‘mfano wewe upo vitani anakuja adui kuwashambulia wewe pamoja na rafiki yako. Wewe upo na risasi 2 mwenzako ana magazin nne zote zimejaa risas, rafiki yako akatumia risas nyingi kumuua yule adui na hatimaye adui akafa. Swali linakuja je, wewe mwenye risasi 2 ungetumia risasi hizohizo tu au ungekubali kufa na risas zako. Jibu ni wewe lazma ungejitete na risasi zako 2. Na hivi ndivyo ilivyo kwa Tanzania yetu, ni lazma tujitetee na vitu na mikakati iliyo ndani ya uwezo wetu. USA wanampango wa kugawa $1200 kwa kila mwananchi ili aweze kujikimu na ndio maana wakafunga mipaka. Leo kwa sisi hapa pangu pakavu tia mchuzi Mh Rais akiamua kufunga mipaka na tusitoke nje ni nan ataumia? Nilijaribu kupitia kurasa mbalimbali za kijamii za mitandaoni nikakutana na Tweet ya Mh Zitto Kabwe akishinikiza kufungwa kwa mipaka na watu kukaa ndani. Nikajiuliza ‘huyu kweli ni mwana uchumi’? Tusipende kupinga vitu ilimradi tumepinga tu, tuangalie ni kwa namna gani tunaweza kupambana na huyu Corona kikwetukwetu.

Abdulkarim Mzee
 
Well said Abdulkarim Mzee,
Wasomi wetu wameharibiwa na elimu hizi za kikoloni,kuiga mambo ambayo sio sahihi kwa mazingira yetu.Zitto Kabwe na wenzake ni watu wa kugoogle tu hakuna uchumi kichwani...nchi zilizofungia watu wake sasa zinaidadi kubwa ya vifo na maqmbukizi pamoja na mqtatizo mengine
 
Ndugu yangu umeandika vyema kulingana na upeo wa wengi. Lakini nikuombe uweke huu waraka wako pembeni kwa siku 14 tuzijazo, unaweza kupata picha halisi na kuifahamu Corona. Wataalamu wa magonjwa ya kuambukiza (experts in Infectious disease) na wale wa epidemiologia wanakwenda mbali zaidi ya kutoa tu pongezi pasipo na vigezo.
Mfano nikikuuliza Serikali imechukua hatua gani zaidi ya kuwaambia watu wanawe mikono na kuandaa sehemu za kuwatibia waathirika (zisizofahamika au kuwa wazi) kwa wengi? Kuomba na kumtegemea Mungu yafaa sana, lakini pasipo kuwa na wajibu kutoka kwetu pamoja na serikali ni kazi bure.

Ukweli ni kuwa maendelea ni hatua, na historia inatuonyesha maarifa na uzoefu kuwa miongoni mwa sababu za mafanikio. Sijui sisi tunakiwango gani kikubwa kuliko hao wanaoangamia kwa janga hili sasa.

Nikupe tu takwimu za karibu, Italia tar 21 Feb walikuwa na wagonjwa 21 na kifo 1 tu (Hii ni kama hapa tulipo sasa). Wiki mbili baadae walikuwa na wagonjwa zaidi ya 5800 na jumla ya vifo takribani 233. Wiki mbili baadae, unaweza kujisemea mwenyewe (vifo zaidi ya 800 kwa siku), nchi kadhaa zimeunga behewa zikiwemo USA, UK, Ufaransa, Spain, Belgium nk. Inawezekana tukawa na sababu mbalimbali zinazoweza kupelekea hali kwetu isiwe mbaya sana, lkn vilevile inawezekana ikawa hata mbaya zaidi. Hivyo ni wajibu wetu kuchukua tahadhari na kufanya yale ya msingi zaidi ya yale yanayoagizwa na serikali kupambana na janga hili. Mfano matumizi ya maski, kuepuka misongamano hususan kwenye mabasi/daladala, kuepuka kwenda baa na sehemu zinazofanana na hizo, kuzingatia usafi kwa maji yanayotirirka n.k

Hiki sio kipindi cha kufikiria kwenye ushindani wa kisiasa, na nashangaa wengi mnaofikiria vyeo vya kisiasa wakati uhakiki wa kuishi ukiwa umetishiwa kwa kiaisi hiki. Uchumi unakwenda kuanguka kuliko unavyoweza kufikiri nk. Ni wakati wa kuja pamoja kama taifa tupigane dhidi ya adui mmoja tu ambaye ni CORONA.
 
Wiki chumvi kali.
Sent using Jamii Forums mobile app by My phone
 
Corona kuathiri wachache ni swala ambalo sidhani kama rais anahusika nalo na kama mtu anamsifu kwa hilo basi labda anafanya hivyo kwa maslahi yake binafsi.

Vivyo hivyo pia huwezi ukawalaumu viongozi ktk zile nchi ambazo maambukizi yamekuwa makubwa kwani hawawajibiki kwa njia yoyote na kusambaa kwa janga hili ktk nchi zao.

Watu wenye ufinyu wa fikra kama kawaida watatumia tukio lolote lile kama fursa ya kueneza propaganda feki za kisiasa which is not only shallow thinking but a reflection of parochial mind.
 
Ila wewe Antibayotike unaijua akili yako mwenyewe eti baadae Ahera kabisa ahahhahahaaaa
 
Huko Kenya Polisi wameshaua watu 3 kuwalazimisha kukaa ndani,na bado wanaendelea,corona imeua less than that...
Akili kubwa ni kubwa tu,...tuendelee kuangalia.
 
Wabongo bana mataifa yenye uwezo watu wanapukutika alafu unaleta hadithi za kusifia sifia.weka akiba ya maneno.
 
Au sio lakini Muda bado na corona bado lipo linawapoteza watu tayari mbongo mmoja kashaondoka kama likija kuripuka baadae naomba usije kukana kauli zako na kumkana mzee nijambo la muda omba sana lisiripuke mkuu
Ulipuke vipi wakati measures zinachukuliwa.? Ndoo za maji kila sehemu na watu wananawa. Sanitizers hadi zimeisha na watu wanatengeneza za kwao kwa kutia dettol.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yes brother, Hali ya sas inabid Tushikamane
 
Kuna watu wanataka total lockdown Kwa malengo yao .

Watu wenye kipato cha juu ambao wanaweza kumudu maisha hayo kwa kipindi kirefu,huku wale wenye maisha ya chini wakifa njaa ndani au kuvamia nyumba za watu na kupora kama yanayiendelea katika nchi za Kenya,Uganda na South Africa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…