Serikali ya Rais John Magufuli yathibitisha umahiri wake katika kupambana na corona na kuwalinda wananchi wake

Abdalah Abdulrahman

Senior Member
Aug 29, 2019
188
250
Pascal Mayalla,
Pascal Mayala..Kanuni za kimaumbile zinasema ukikaa na njaa zaidi ya sikukuu kadhaa utakufa,haijslishi wewe ni mchamungu kiasi gani na unamuomba Mungu kiasi gani,hivyo Raisi wetu,

sio tu anamtegemea Mungu akaacha kufanya jitihada za kumwonesha Mungu kuwa anahitaji msaada wake..anafanya jitihada hizo za kitaalamu na Watanzania wote pamoja na wale waliotaka kutumia janga hili kuwaangamiza Watanzania wanamuelewa
 

barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
31,661
2,000
Au sio lakini Muda bado na corona bado lipo linawapoteza watu tayari mbongo mmoja kashaondoka kama likija kuripuka baadae naomba usije kukana kauli zako na kumkana mzee nijambo la muda omba sana lisiripuke mkuu
Acha wivu. Toa mapendekezo mbadala kama unaona hatua alizochukua sio sahihi.
 

Graph

JF-Expert Member
Jul 20, 2016
2,741
2,000
Upuuzi tu, Sifia sifia kila kitu hahaha, sasa alichofanya hasa ni kipi? Amekaa tu anasubiri, omba huyo mtu wenu aliyekaa mawinguni msijeugua kama nje maana tanzania haina uwezo wowote ule wa kudeal na hili swala
 

samilakadunda

JF-Expert Member
Oct 13, 2011
1,777
1,500
Abdalah Abdulrahman, Maandishi yako ni marefu sana, ila ukumbuke China sio Tanzania , wenzetu wanatambua maambukizi kwakuwa wanavipimo vya kutosha nchi nzima, sisi hadi sample ichukuliwe ipelekwe maabara kuu, majibu baada ya week,

hebu jiulize aliyopo huko niombe usagatikwa anaeumwa atapimwa na kipimo kipi, mwisho atakufa nahajakujua ni corona imemuua, kiukweli Bado tupo nymama kitaalamu na kiuwezo kupambana na ugonjwa huu, sisi twendelee kumuomba Mungu kila kuitwao leo .

Goodmorning

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,970
2,000
Uzalendo gani? Unatumia matriliin kununua mandege ila unashindwa kutoa huduma za maana kuoambna na ugonjwa. Ni sawa na mzazi anayenunua gari ila anashindwa kulipa pesa kuwapeleka wanae hospitali anawapa mitishamba.

Huu ugonjwa piga ua lazima sstage ya total home quarantine tutafika tu. Tena ndani ya mwezi huuu. Mark my words.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
12,241
2,000
Mfano zipo nchi zilizochukua maamuzi ya kuwazuia watu wake kutoka nyumbani na kufunga kabisa shughuli za uzalishaji,na zipo nchi zilizochukua maamuzi ya kufunga mipaka yake kutokuruhusu kuingia na kutoka kwa wananchi wake.Lakini cha kustaajabu nchi hizi zimeendelea kukabiliwa na maambukizi na kuongeza ukubwa wa tatizo kwa wananchi wake.Ukubwa wa tatizo hili katika baadhi ya nchi unaongezwa na msongo wa mawazo na kukata tamaa kwa wananchi,uchumi wa familia unaoambatana na ukosefu wa chakula kutokana na kutokuwepo maandalizi stahiki na mlipuko wa magonjwa mengine ya kijamii.
Wewe na wenzako msichojua ni kwamba, nchi zote hizo zilichukua hizo hatua wakati it's TOO LATE.. I repeat, it's TOO LATE!

Iran kwa mfano, wakati China hali ni tete, viongozi wa Iran wakatamka hadharani kwamba nchi yao italindwa na Mungu bila kujali Mji Mtakatifu wa Qom una projects kibao za Wachina, na kwahiyo kuna Wachina kibao!!!

Spain nao, wakati Italy hali ni tete, Mkuu wa Tiba za Dharula, Madrid, Dr. Fernando Simon akatangaza hadharani kwamba Spain itaathirika kwa kiasi kidogo sana kwa sababu they don't even share the border with Italy!

Matokeo yake, muda wote huo watu wakaendelea kula bata huku wakijazana viwanjani kuangalia soka!

Sio tu hivi sasa Spain wameipiku hata China na Iran kwa idadi ya vifo, bali Dr. Fernando mwenyewe majuzi was relieved from duties kwa sababu na yeye amekuwa infected na COVID-19!

Hata hivyo, Maria Jose Sierra aliyechukua nafasi ya Dr. Fernando juzi ametangaza kwamba total quarantine imesaidia sana kupunguza maambukizi ya coronavirus nchini spain.

Sio kwamba maambukizi kwa ujumla yanapungua, hell no bali yanaongezeka BUT at decreasing rate in contrast at increasing rate!

Kwahiyo kwa watu wanaofuatilia hili janga nje ya bara la Afrika, watu aina yenu tunawaona walevi tu!!!

Kule Korea ya Kusini, Mwanzilishi wa Shincheonji Church of Jesus, Lee Man-hee akataka kuleta masihara kama mnayoleta nyie na Magufuli wenu mliyeapa kutetea kila anachoongea hata kama ni cha kijinga!!

Wakati China hali ni tete, Lee Man-hee akahamasisha wafuasi wake waendelee kujazana makanisani! After the first gathering, baada ya Korea Kusini kufanya COVID-19 testing, watu zaidi ya 400 wakakutwa na virus huku zaidi ya nusu ya waathirika wakiwa ni wafuasi wa Shincheonji Church!!

Hapa chini ni Lee Man-hee akiomba msamaha baada ya kusababisha janga kubwa Korea ya Kusini:-

Hata Wataalamu kutoka Italy waliokuwa wamehojiwa, wengi wanaamini wakati serikali inachukua hatua, it's already too late! Kwa mfano, mtu wa kwanza kabisa kuwa tested positive, huyu alijipeleka mwenyewe hospitali ikiwa na maana hadi wakati huo hapakuwa na mkakati wowote wa kudhibiti ugonjwa!

The question is, huyu mtu ambae alikuwa amekutana mara kwa mara na mwenzake aliyekuwa ametoka China, alikuwa amekutana na watu wangapi kabla hajajipeleka mwenyewe hospital, na huyo mwenzake alikuwa amekutana na watu wangapi ukitoa huyu ambae ni first confirmed case!

Ni kutokana na ukweli huo, ndio maana haikushangaza less than 24 hours later, watu wengine 16 wakagundulika kuwa na virus, na miongoni mwao, kulikuwa na madaktari na manesi 5, na watu wengine watatu waliokuwa wameenda kumwangalia yule mtu ambae aligunduliwa kama mtu wa kwanza!

Ukiangalia hayo, utaona wazi kwamba, sio tu watu wa kawaida bali hata health workers walikuwa bado hawachukui tahadhali!!

Na hata serikali ilipoanza kuchuka hatua, walianza kama Tz... walioathrika ndio walipigwa quarantine ingawaje tayari na wao walikuwa wameshaambukiza mwingine!

Mifano ipo mingi lakini itoshe tu kusema siasa zisiwafanye muwe vipofu! Kwamba hata waliofanya lockdown haikuwasadia ni uongo usio na maana yoyote... haikuwasaidia sio kwa sababu haisaidii bali haikusaidia kwa sababu walichukua serious measures when it's too late!

Donald Trump kwa mfano! NI mara ngapi alikuwa akisikia kufanya masihara hadi kufikia kuita ni Chinesevirus, mara Wuhanvirus, mara aite Foreignvirus?! Ni Trump huyo huyo ambae back in January alitangaza kwamba US imei-contain coronavirus na kwamba kulikuwa na mgonjwa mmoja tu, tena from China!!

Akaendelea kuleta mzaha kiasi cha kutangaza chloroquine inatibu COVID-19!!!

In short, kote Ulaya na America walichelewa kuchukua hatua! Trump alizuia ndege kutoka Europe takribani wiki 2 tu zilizopita!! Je, hali ya maambukizi 2 weeks ago ilikuwaje Europe?!

Leo hii quarantine isiposaidia US utasema quarantine ni ineffective au serikali ya Trump haikuwa serious hadi ilipokuwa too late?!
 

Zawadini

JF-Expert Member
Feb 2, 2012
1,588
2,000
Tofauti na nchi zingine njia hizi zimeweza kuleta matuamaini makubwa kwa Watanzania kwani idadi ya maambukizi mapya imekua kwa kiwango kidogo kulinganisha na nchi zingine.
Ni sawa mkuu. Ngoja nikudokeze. Ugojwa huu unayokawaida ya kuanza polepole na baadae kuripuka ghafla na watu wakataharuki. Sawa tumpongeze mtukufu ila huenda takwimu hizi zitasaidia:Italy Februari 21, 2020 wagonjwa 21 lakini Machi 27, 2020 wagonjwa 86,498; Arekani februari wagonjwa 16 Machi wagonjwa 100,037Ufaransa Februari 26 wagonjwa 18 Machi 27 wagonjwa 32,964. Nawasihi Watanzania tuchukue tahadhari hakuna umahiri wa huyu wa yule.
 

konyola

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
2,184
2,000
UNADHANI KWA KULETA HIZI SIFA NDO UTAUPATA UKUU WA WILAYA? PAMBANA NA HALI YAKO HUPATI U-DC WALA U-DED hata U-DAC utausikiaga tu maana najua kwenye korona kuna watu watasifia hadi upuuzi ili wakumbukwe
 

Bishweko

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
2,989
2,000
Alafu eti Jack Ma anatuma vifaa huku ...Yaani nchi zije zijifunze kwa JPM jinsi anavyoipukutisha Covid-19
 

Abdalah Abdulrahman

Senior Member
Aug 29, 2019
188
250
UNADHANI KWA KULETA HIZI SIFA NDO UTAUPATA UKUU WA WILAYA? PAMBANA NA HALI YAKO HUPATI U-DC WALA U-DED hata U-DAC utausikiaga tu maana najua kwenye korona kuna watu watasifia hadi upuuzi ili wakumbukwe
Nina kazi nzuri inayolipa kuliko U_DC...Mawazo ya kimaskini na kifisadi ni kuwa ukiwa kiongozi ndio unapata rsha,uliza kuhusu kuongoza katika serikali inayochukia rushwa na sikivu kwa wananchi.Hakuna rangi kiongozi haioni...kiongozi awamu hii ni mtumwa wa wananchi
 

Abdalah Abdulrahman

Senior Member
Aug 29, 2019
188
250
Mimi ni guru kwenye masuala ya strategic management... Kiongozi bora hutoa muelekeo na kuwaamini wasaidizi wake.
Shida yako unaamini Raisi ni kiongozi wa Mkoa wa Dar Es salaam,badilika fikra,Raisi anatakiwa kuendelea na mambo mengine
 

mafutamingi

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
2,625
2,000
Mkuu bila kuwa biased wala kuombea mabaya, hebu hili bandiko lako tuliache Kwanza Hadi wiki 3 au 4 zijazo alafu tulijadilia

Sent using Jamii Forums mobile app
Wiki moja iliyopita Rais Trump alikuwa na mtazamo kama wa JPM na hakutaka kabisa lockdown iliyokuwa imewekwa katika baadhi ya majimbo iendelee. Hovyo akatangaza nia yake ya kusitisha hiyo lockdown. Hapo ndipo wataalam wake wakampa ukweli kuwa hali ni mbaya na wamarekani si chini ya 100,000 watakufa kutokana na corona. Ndipo Trump akasema "Nothing can be worse than declaring victory before victory is won", yaani hakuna kitu kibaya kama kutangaza ushindi kabla ya ushindi haujapatikana.

Kumbukeni pia ya kwamba kisa cha kwanza huko USA kilitangazwa January 20, na baada ya hapi vifo viliongezeka kwa kasi ndogo sana hadi March 16 ndipo hali ikabadilika. Sisi Tanzania kisa cha kwanza kilitangazwa March 16 na mpaka sasa hali haijawa ya kutisha. Hali hii isitufanye tuamini kwamba tayari tumeshinda vita. Muda ndo utaamua. Kwa sasa tujiepusha na kusifia!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom