Serikali ya Mseto yanukia

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
19,586
14,138
Niwasalimu kwa jina la JMT..

Kuna dalili na kelele za watu hususani wapinzani uchwara kutaka Serikali ya Mseto kwa visingizio vya eti kuponya Nchi na kuleta maridhiano..

Binafsi siungi mkono kwa sababu hakuna hicho wanachosema mgawanyiko hapa Nchini. Hizi ni mbinu za wapinzani kutafuta asali na Wala sio kuwatumikia Wananchi.

Pia Serikali ya Mseto inasimamia nini zaidi ya migogoro na kutunishiana misuli? Tukatae huu uhuni.👇

gazeti.JPG
 
Wapinzani wako au wapinzani wakitufani?kumbuka Tanzania ni ya watanzania wote bila kujali ,rangi ,elimu,dini ,kabila itikadi au muonekano wa mtu.usijiumize Bure kwa kuchukua mtu bila sababu yoyote ile maana kuto mpenda wewe hakumuondolei yaki sake zote kama mtanzania.
 
Kwanza hakuna kitu kama serikali ya mseto kwa Tanganyika na sababu ya huo mseto haupo hata nyie mnaofikilia mseto ni mnataka kuja kutekeleza sera za mtu mwingine as kinachotokea Zanzibari kwa makamu wa kwanza wa Rais.
 
Kwani imekuaje mpk mwananchi wameandika hivi? Huu mseto unatoka wapi? Imekuaje? Kwa Katiba hipi?
 
..kuliponya taifa tunahitaji Tume ya Ukweli na Maridhiano.

..wote waliotendewa uovu au waliodhulumiwa na watawala wajulikane, wafidiwe, na kuombwa msamaha.

..walioshiriki kutenda uovu au dhuluma wasamehewe au wafikishwe mahakamani.

..Serikali ya mseto sio njia sahahi ya kuponya majeraha na makovu yaliyosababishwa na serikali zetu tangu Uhuru na Mapinduzi.
 
Niwasalimu kwa jina la JMT..

Kuna dalili na kelele za watunhususani wapinzani uchwara kutaka Serikali ya Mseto kwa visingizio vya eti kuponya Nchi na kuleta maridhiano..

Binafsi siungi mkono kwa sababu hakuna hicho wanachosema mgawangiko hapa Nchini.Hizi ni mbinu za wapinzani kutafuta asali na Wala sio kuwatumikia Wananchi..

Pia Serikali ya Mseto inasimamia nini zaidi ya migogoro na kutunishiana misuli? Tukatae huu uhuni,.👇
Akili za kimaskini hizi ...mtu kama huyu akikukuta bar unagonga Windhoek unakutumbulia macho kama msomali wa Kajiado

Dunia imebadilika acha UJIMA
 
Uwezi kuongelea swala la Mseto wakati kimsingi wapinzani wa nchii hii hata uchaguzi ukiwa wanavyotaka hawana uwezo wa kushinda majimbo hata 80 ya uchaguzi! Pamoja na kuwepo kwa kelele za uchaguzi kuibwa 2020 bado sijawai kushuhudia nguvu ya upinzani kutwaa majimbo hata 100 ya uchaguzi!

Hata mizania ikiwa sawa kweli wanaweza pata majimbo hata 100? Kweli wanaaminika kwenye box la kura? Nyakati za kampeni ni tofauti kabisa na nyakati za kupiga kura ...nyakati hizi ni tofauti kabisa kwa wapiga kura na huwa nafikra tofauti kabisa!

Serikali ya mseto sio huruma bali ni nguvu kwenye boksi la kura na ukweli ni kwamba bado wapinzani hawana nguvu ya kushawishi serikali ya mseto!
 
..kuliponya taifa tunahitaji Tume ya Ukweli na Maridhiano.

..wote waliotendewa uovu au waliodhulumiwa na watawala wajulikane, wafidiwe, na kuombwa msamaha.

..walioshiriki kutenda uovu au dhuluma wasamehewe au wafikishwe mahakamani.

..Serikali ya mseto sio njia sahahi ya kuponya majeraha na makovu yaliyosababishwa na serikali zetu tangu Uhuru na Mapinduzi.
Mnaposema yawepo maridhiano ya kitaifa kwa ajili ya kuponya maumivu yaliyosababishwa na uovu na dhulma iliyofanyika hapa Nchini wengi wanadhani awamu ya tano pekee ndio iliyofanya hivyo kumbe hata kabla ya awamu ya tano kuingia madarakani uonevu na dhulma vilifanyika !!
 
Uwezi kuongelea swala la Mseto wakati kimsingi wapinzani wa nchii hii hata uchaguzi ukiwa wanavyotaka hawana uwezo wa kushinda majimbo hata 80 ya uchaguzi! Pamoja na kuwepo kwa kelele za uchaguzi kuibwa 2020 bado sijawai kushuhudia nguvu ya upinzani kutwaa majimbo hata 100 ya uchaguzi!

Hata mizania ikiwa sawa kweli wanaweza pata majimbo hata 100? Kweli wanaaminika kwenye box la kura? Nyakati za kampeni ni tofauti kabisa na nyakati za kupiga kura ...nyakati hizi ni tofauti kabisa kwa wapiga kura na huwa nafikra tofauti kabisa!

Serikali ya mseto sio huruma bali ni nguvu kwenye boksi la kura na ukweli ni kwamba bado wapinzani hawana nguvu ya kushawishi serikali ya mseto!

Ww lazima utakuwa ni mzee, na kama ni kijana basi ni wale wanaoogopa mabadiliko. Hiki sio kizazi cha CCM, dola pekee ndio kinga yake. Uwezo wa CCM kushinda tena kihalali kwenye box la kura kwa zaidi ya 50% haupo, na sio kwamba tu haupo, bali zama hizo hazitakaa zirudi tena.

Ule ushenzi, uhayawani na ukatali wa wazi ili CCM watangazwe washindi kwa shuruti sio bahati mbaya, bali hakuna jinsi ili CCM ipate wingi wa vitu bungeni wa kupitisha chochote watakacho. Kama huamini washawishi CCM wenzako uchaguzi uwe wa haki ndio utajua hujui.
 
Mnaposema yawepo maridhiano ya kitaifa kwa ajili ya kuponya maumivu yaliyosababishwa na uovu na dhulma iliyofanyika hapa Nchini wengi wanadhani awamu ya tano pekee ndio iliyofanya hivyo kumbe hata kabla ya awamu ya tano kuingia madarakani uonevu na dhulma vilifanyika !!

Unaamini kabisa hatujui tofauti ya hizo awamu, au unadhani tuna ubongo mdogo kiasi kwamba tumesahau uhayawani uliofanyika awamu ya tano?
 
Kwani imekuaje mpk mwananchi wameandika hivi? Huu mseto unatoka wapi? Imekuaje? Kwa Katiba hipi?
Mambo ya Sihasa hayo !! Waswahili wanasemaga Kikulacho ki-nguoni mwako !! Ukiona nyumbani hakueleweki eleweki sio mbaya kutaka msaada kidogo kutoka kwa jirani !! Maana jirani naye ni ndugu pia !! Na anaweza kuwa na msaada mkubwa zaidi kuliko ndugu wa kuzaliwa naye !!
 
Unaamini kabisa hatujui tofauti ya hizo awamu, au unadhani tuna ubongo mdogo kiasi kwamba tumesahau uhayawani uliofanyika awamu ya tano?
Tunakumbushia tu kwamba na sisi wa kabla ya awamu ya tano tusisahauliwe katika hayo maridhiano !! Maana wengine majeraha yetu hayajapona mpaka hivi sasa !!
 
Mkuu unasubiri watu wakupambanie? We hata kama umeonewa enzi za mkoloni au awamu ya kwanza paza sauti, sio ukae mahali ukisubiri watu wakupambanie kisha uitwe.
 
Mkuu Suluba nilizozipata ni katika mapambano kama haya haya !! Ya kukataa uonevu !! Mimi sio wa kusubiri nipambaniwe !! Ni angalizo tu kwamba na sisi wa kabla ya awamu ya tano bado tupo !!
 
Niwasalimu kwa jina la JMT..

Kuna dalili na kelele za watunhususani wapinzani uchwara kutaka Serikali ya Mseto kwa visingizio vya eti kuponya Nchi na kuleta maridhiano..

Binafsi siungi mkono kwa sababu hakuna hicho wanachosema mgawangiko hapa Nchini.Hizi ni mbinu za wapinzani kutafuta asali na Wala sio kuwatumikia Wananchi..

Pia Serikali ya Mseto inasimamia nini zaidi ya migogoro na kutunishiana misuli? Tukatae huu uhuni,.👇
Kwa hii CCM ?
 
Niwasalimu kwa jina la JMT..

Kuna dalili na kelele za watu hususani wapinzani uchwara kutaka Serikali ya Mseto kwa visingizio vya eti kuponya Nchi na kuleta maridhiano..

Binafsi siungi mkono kwa sababu hakuna hicho wanachosema mgawanyiko hapa Nchini. Hizi ni mbinu za wapinzani kutafuta asali na Wala sio kuwatumikia Wananchi.

Pia Serikali ya Mseto inasimamia nini zaidi ya migogoro na kutunishiana misuli? Tukatae huu uhuni.👇
View attachment 2273363View attachment 2273364
Watu makini wanaona act kinapewa nguvu Eti.

Uonavyo sivyo nionavyo.
 
Back
Top Bottom