Abunwasi
JF-Expert Member
- Jun 25, 2009
- 5,486
- 3,468
Ukwepaji wa kodi stahili uliwanufaisha wasafirishaji kiasi ikaleta hata kejeli na madharau kwa viongozi wa serikali waliokuwa na misimamo wasioyapenda. Inasemekana bwana mkubwa mmoja aliwahi kumkejeli kiongozi kwa kusema 'mimi ninaongea na mwenye mbwa' kutokana na kutopendezewa na msimamo wa kiongozi huyo na wakubwa hao wakaenda juu zaidi na kupewa afueni.Jana viongozi wa hawa jamaa wa usafiri na wakala wa forodha walikuwa hapo channel ten kuanzia saa nne usiku. Wakaeleza kuwa hii kodi imeongeza gharama ya bandari ya DSM ikawa dolla takribani 800 zaidi ya Mombasa. Hapo awali ilikuwa takribani dolla 350 chini. Ila hili unaongolea hapa sikusikia likigusiwa.
Ni wakati wa serikali kuangalia kama kweli kuna upotoshaji kiasi hiki ni muhimu hatua madhubuti zikachukuliwa. Maana yaonesha kuna watu wamedhamiria kwelikweli kuikwamisha hii serikaki. Tusisahau hapo kwenye kipindi kulisomwa mpaka barua pepe za wateja wanatumia bandari ya DSM waliositisha mizigo yao.