Serikali ya Magufuli kutoza VAT kwenye "on transit goods" ni aibu na fedheha!

Jana viongozi wa hawa jamaa wa usafiri na wakala wa forodha walikuwa hapo channel ten kuanzia saa nne usiku. Wakaeleza kuwa hii kodi imeongeza gharama ya bandari ya DSM ikawa dolla takribani 800 zaidi ya Mombasa. Hapo awali ilikuwa takribani dolla 350 chini. Ila hili unaongolea hapa sikusikia likigusiwa.

Ni wakati wa serikali kuangalia kama kweli kuna upotoshaji kiasi hiki ni muhimu hatua madhubuti zikachukuliwa. Maana yaonesha kuna watu wamedhamiria kwelikweli kuikwamisha hii serikaki. Tusisahau hapo kwenye kipindi kulisomwa mpaka barua pepe za wateja wanatumia bandari ya DSM waliositisha mizigo yao.
Ukwepaji wa kodi stahili uliwanufaisha wasafirishaji kiasi ikaleta hata kejeli na madharau kwa viongozi wa serikali waliokuwa na misimamo wasioyapenda. Inasemekana bwana mkubwa mmoja aliwahi kumkejeli kiongozi kwa kusema 'mimi ninaongea na mwenye mbwa' kutokana na kutopendezewa na msimamo wa kiongozi huyo na wakubwa hao wakaenda juu zaidi na kupewa afueni.
 
UPOTOSHAJI. Nosense and Rubish!

Kinachotakiwa kulipiwa VAT ni Mapato yanayotozwa hapa nchini kwa huduma zinazotolewa kwa mizigo hiyo na si mizigo yenyewe.

Watanzania tulipe kodi tuacha uzushi wa visingizio ili tusilipe kodi.

Je atakayelipa hiyo VAT kwa mapato yanayotozwa hapa nchini si mlaji wa nchi jirani ambapo mzigo unakwenda? Kumbuka mtoa huduma wa hapa hatailipa hiyo VAT kutoka mfukoni mwake bali will pass it over to importers from the neighbouring countries. Kwa hiyo suala hapa siyo watanzania kutoa visingizio kutokulipa kodi bali ni je bandari zetu zitakuwa zitahimili ushindani wa bandari lukuki zilizotuzunguka?
 
Angelina nilimsikiliza vizuri tu, Kama walivyo Watanzania wengi anaongelea kijumlajumla. Anasema watu wanatumia Bandari ya Durban, sijui watu wanajenga reli lobindo, nk na hatuambia gharama za kutumia hiyo bandari au usafiri wa hiyo reli ukilinganisha na hapa kwetu. Na gharama hapa iwe kwa maana ya gharama zote, Umbali, usalama muda wa mzigo kumfikia mteja n.k.
Sasa yeye katumia kigezo cha fedha tu.

QUOTE="Destined to heaven, post: 16827061, member: 371827"]ndugu ukweli siku zote lazima upingwe kwa nguvu zote lakini all in all time will tell lakini nashukuru alitoa mfano wa yusuph ktk bible.mwenye masikio na asikie hakuna anaelazimisha maana kila kitu kina positive na negative usinganganie positive tu ya kukusanya mapato na kuongeza salio angalia na madhara ya any tax increment unayoifanya kwa you competitor.kama ulimsikiliza yule mama as an expart utamwelewa hana nia mbaya kama unavyodhania.wake up guys msije kumbuka shuka kokoliko analia ohooooooooooo!!!!!!!![/QUOTE]
 
Unaikumbuka misamaha ya kodi iliyomake headline bungeni from Wapinzan kwenye serikari ya awamu ya 4 ?
Asante kwa kunielewa

Mtu anakuja akishangilia na kutishia kuwa bandari kavu hazina mizigo. Sasa mizigo kama ilikuwa ni ya biashara za magunashi na sasa zina pigwa vita mlitegemea hizo icd zipate wapi mizigo?
 
Mizigo ya Transit ilikukwa haitozwi kodi yoyote ile lakini wasafirishaji walitumia mwanya huo kudanganya. Kwa mfano gari la mafuta ya petroli ambalo linapaswa kwenda DRC lakini linaishia chalinze na makaratasi hupigwa muhuri kana kwamba lile gari lilivuka mpaka wa nchi kwenda huko. matokeo ya matumizi mabaya ya namna hii ndiyo maana mizigo hiyo inalipishwa VAT na wakisha wakilisha mizigo hiyo nje ya nchi hurejeshewa hizo pesa walizolipa kama VAT.
Kilichokuwepo hivi sasa ni kampeni za wenye magari makubwa wakitaka huruma ya jamii ili waendelee kutuhujumu.
HAYA NI MATOKEO YA KUTOFANYA BIASHARA KIUADILIFU- muwe wapole na mlipe tu hiyo hela halafu muombe refund kama sheria inavyosema.
Daah umenifungua macho..
 
Mfalme J. in the making.

Kuna makubaliano ya kikodi yanaitwa double taxation agreements. Ikiwa nchi mbili zikikubaliana kuwa nchi moja itoze kodi kwa kutumia "Origin Principle", basi nchi nyingine isitoze kodi. AU,

Ikiwa zikakubaliana kutumia "destination principle", basi kodi itatozwa kule bidhaa inakokwenda na haitatozwa kule inakotoka, au itatozwa kwa kutafuta tofauti ya kodi iliyotozwa kwenye origin (ilikotoka) na ile itakayotozwa kwenye destination (inakokwenda).

Kinyume na hapo, kutakuwa na double taxation.

Washauri wa Rais Mpooo??????
Mfalme J....
(ataomba kunyongwa kwa hiari hapo mbeleni?)
 
Kuna vitu vingine mtu au watu kuvifanya ni lazima wajiulize mara mbilimbili na kutafakari kwa kina madhara yake.

Serikali tukufu ya rais John Magufuli kwa mwaka wa fedha ulioanzia July moja, ilianza kutoza VAT kwa "on transit goods" mizigo ambayo inatoka bandarini eidha ya Dar es Salaam ama nyingine za hapa nchini kupitia ardhi ya Tanzania kwenda nchi jirani hasa za Congo (DRC) na Zambia. Hii bila kumung'unya maneno ni jambo lisilo sahihi kabisa!

Mzigo unakotoka (kule kiwandani) umelipiwa tayari VAT na wenzetu wakienda kuuza nchini mwao wanalipa VAT, sasa wewe Tanzania unataka VAT kwa biashara gani uliyofanya?

Isitoshe jambo hilo limetokomezea mbali uhusiano mzuri wa kibiashara baina ya Tanzania na mataifa hayo, mambo sasa yanaenda ndivyo sivyo. Mimi kama mdau wa Maendeleo ya nchi napinga utozaji holela wa VAT usiofuata tararibu za kikodi hivyo napingana na mipango ya waziri Mpango juu ya VAT.

Tusipoiangalia hii VAT tunayotoza kiholela tutajikuta tukiwapa mzigo mkubwa watu wengi huku tukiishia kupoteza fursa muhimu.

Rai yangu ni kuwa swala la ulipaji VAT lishughulikiwe kwa umakini na serikali isione kama ni sehemu ya kupatia ahueni bila kufuata taratibu za kodi.

Niliwahi kutoa maoni humu kuwa sasa serikali ya Magufuli iwe na "sites" maalum za kukusanyia VAT. Kuwa na EFD nyingi zilizozagaa mtaani siyo suluhisho la ukusanyaji mapato bali nyingi ni zile zinazoumiza nakuzorotesha biashara pamoja na maisha ya kila siku.
Kimantiki kodi ya ongezeko la thamani (VAT) ulipwa na consumer mlaji wa mwisho. Na hawa wafanyabiashara wanakuwa ni mawakala tu wa kukusanya. Sasa swali la kujiuliza Je mfanyabiashara wa Congo, Burundi, Zambia na kwingineko anawezaje kurefund kodi hii. Na Je tumefanya utafiti kubaini iwapo bandari yetu inatoza Gharama nafuu kilimo nyingine zinazoweza kuhudumia nchi hizo!?
 
Mfalme J. in the making.

Kuna makubaliano ya kikodi yanaitwa double taxation agreements. Ikiwa nchi mbili zikikubaliana kuwa nchi moja itoze kodi kwa kutumia "Origin Principle", basi nchi nyingine isitoze kodi. AU,

Ikiwa zikakubaliana kutumia "destination principle", basi kodi itatozwa kule bidhaa inakokwenda na haitatozwa kule inakotoka, au itatozwa kwa kutafuta tofauti ya kodi iliyotozwa kwenye origin (ilikotoka) na ile itakayotozwa kwenye destination (inakokwenda).

Kinyume na hapo, kutakuwa na double taxation.

Washauri wa Rais Mpooo??????
Binafsi nadhani dhana nzima ya ukusanyaji kodi inapotoshwa Kama Si kwamba inahujumiwa. vat Katika kila Huduma itazamwe vizuri jamani. Isijekuwa ndo tunagawana mbao za jahazi letu tukidhani tunajinusuru.
 
UPOTOSHAJI. Nosense and Rubish!

Kinachotakiwa kulipiwa VAT ni Mapato yanayotozwa hapa nchini kwa huduma zinazotolewa kwa mizigo hiyo na si mizigo yenyewe.

Watanzania tulipe kodi tuacha uzushi wa visingizio ili tusilipe kodi.
Kama hivyo ndivyo basi kodi hiyo haina adhi ya kuitwa VAT. Maana vat ikiwa na mlaji wa mwisho mtoa Huduma ni Wakala wa ukusanyaji tu
 
Kuna vitu vingine mtu au watu kuvifanya ni lazima wajiulize mara mbilimbili na kutafakari kwa kina madhara yake.

Serikali tukufu ya rais John Magufuli kwa mwaka wa fedha ulioanzia July moja, ilianza kutoza VAT kwa "on transit goods" mizigo ambayo inatoka bandarini eidha ya Dar es Salaam ama nyingine za hapa nchini kupitia ardhi ya Tanzania kwenda nchi jirani hasa za Congo (DRC) na Zambia. Hii bila kumung'unya maneno ni jambo lisilo sahihi kabisa!

Mzigo unakotoka (kule kiwandani) umelipiwa tayari VAT na wenzetu wakienda kuuza nchini mwao wanalipa VAT, sasa wewe Tanzania unataka VAT kwa biashara gani uliyofanya?

Isitoshe jambo hilo limetokomezea mbali uhusiano mzuri wa kibiashara baina ya Tanzania na mataifa hayo, mambo sasa yanaenda ndivyo sivyo. Mimi kama mdau wa Maendeleo ya nchi napinga utozaji holela wa VAT usiofuata tararibu za kikodi hivyo napingana na mipango ya waziri Mpango juu ya VAT.

Tusipoiangalia hii VAT tunayotoza kiholela tutajikuta tukiwapa mzigo mkubwa watu wengi huku tukiishia kupoteza fursa muhimu.

Rai yangu ni kuwa swala la ulipaji VAT lishughulikiwe kwa umakini na serikali isione kama ni sehemu ya kupatia ahueni bila kufuata taratibu za kodi.

Niliwahi kutoa maoni humu kuwa sasa serikali ya Magufuli iwe na "sites" maalum za kukusanyia VAT. Kuwa na EFD nyingi zilizozagaa mtaani siyo suluhisho la ukusanyaji mapato bali nyingi ni zile zinazoumiza nakuzorotesha biashara pamoja na maisha ya kila siku.

kaka kama hujui jambo ni vema ukaomba ueleweshwe kuliko kukurupuka na kupotosha watu, kinachotozwa VAT ni gharama za huduma za kupitisha mizigo bandarini, mfano, gharama wanazotoa kwa TICS zinakatwa VAT, gharama wanazotoa kwa mawakala zinatozwa VAT.
 
Kuna watu wanatumiwa na wafanyabiashara ili kuipotosha jamii. Lipeni kodi hizo on transit zinapita hewani? si ndo hizo zinaharibu mpaka barabara zetu
Hivi visingizio vya kukwepa kujibu hoja kwa Kudai watu wanatumiwa ni vya kizembe. Kama tunahitaji kuongeza mapato ya bandari tubadilishe tariffs na rates tu siyo kutoza VAT tunachafua na kufukuza Wateja. Alafu hata hivyo Si kwa kustukizana namna hii. Ndani ya siku tatu tu umeanza kutoza kodi!? Kwamba kazi zilizokwisha kupataniwa Gharama hasara hiyo iwe ya nani!? Biashara haifanywi kwa kuviziana namna hii
 
Kama hawataki wakapitishe beira msumbiji
 
Huo ufafanuzi wa kwamba mzigo Ukiisha kuvuka Mwenye Mali atadai kodi aliyoitoa unautoa wewe Au!?? Maana kwenye sheria ya makusanyo Yaani bajeti halijazungumzwa hivyo Au kuna yaliyoachwa ili kuja kuyatolea ufafanuzi
 
Kwa kukusaidia, VAT imeanza kutozwa tokea Julai 2015.

Kwa nini wanaanza kulalamika sasa kuhusu VAT wakati sheria ilikuwepo kuanzia mwaka 2015?

Serikali ya Rais Magufuli inachofanya ni kusimamia kwa ukamilifu sheria ambayo imeanza mwaka mmoja uliopita.

Kwa kukusaidia zaidi, VAT is charged on all ancillary transit cargo handling services like wharfage, stuffing, handling charges, stevedoring, agency fee, stripping etc.

Kikubwa zaidi, VAT waliyolipa huwa wanarudishiwa wakifika mipakani. Hawa wanaopiga kelele kuhusu VAT inawezekana ni wale walikuwa wanadanganya kama mizigo wanaipeleka nje wakati sivyo.

Fanya kwanza utafiti kabla ya kuja na thread isiyo na ukweli.
Kubuni tukio ili kujenga hoja Si tabia ya kiungwana. Hiyo vat unayosema umeanza kutozwa toka July2015 ipi!? Na ni kwa mzigo wa transit!? Au unacheza mdundo tu bila kujua mashairi yanamaanisha nini!?
 
Unajua kuna VAT wageni wanarudishwa kwenye exit border mfano airport kama walinunua bidhaa au huduma yenye VAT hapa nchini?

Lakini kuna point ya kuwa watu walikuwa wanatumia kama njia ya ukwepaji kodi. Mzigo wa burundi unaishia hapa msamvu. Morogoro.

Kama unashindwa ku-control halafu unakuja kuleta usumbufu usio na maana hasa kwa wasio na hatia.
 
Back
Top Bottom