G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,593
- 36,012
Kuna vitu vingine mtu au watu kuvifanya ni lazima wajiulize mara mbilimbili na kutafakari kwa kina madhara yake.
Serikali tukufu ya rais John Magufuli kwa mwaka wa fedha ulioanzia July moja, ilianza kutoza VAT kwa "on transit goods" mizigo ambayo inatoka bandarini eidha ya Dar es Salaam ama nyingine za hapa nchini kupitia ardhi ya Tanzania kwenda nchi jirani hasa za Congo (DRC) na Zambia. Hii bila kumung'unya maneno ni jambo lisilo sahihi kabisa!
Mzigo unakotoka (kule kiwandani) umelipiwa tayari VAT na wenzetu wakienda kuuza nchini mwao wanalipa VAT, sasa wewe Tanzania unataka VAT kwa biashara gani uliyofanya?
Isitoshe jambo hilo limetokomezea mbali uhusiano mzuri wa kibiashara baina ya Tanzania na mataifa hayo, mambo sasa yanaenda ndivyo sivyo. Mimi kama mdau wa Maendeleo ya nchi napinga utozaji holela wa VAT usiofuata tararibu za kikodi hivyo napingana na mipango ya waziri Mpango juu ya VAT.
Tusipoiangalia hii VAT tunayotoza kiholela tutajikuta tukiwapa mzigo mkubwa watu wengi huku tukiishia kupoteza fursa muhimu.
Rai yangu ni kuwa swala la ulipaji VAT lishughulikiwe kwa umakini na serikali isione kama ni sehemu ya kupatia ahueni bila kufuata taratibu za kodi.
Niliwahi kutoa maoni humu kuwa sasa serikali ya Magufuli iwe na "sites" maalum za kukusanyia VAT. Kuwa na EFD nyingi zilizozagaa mtaani siyo suluhisho la ukusanyaji mapato bali nyingi ni zile zinazoumiza nakuzorotesha biashara pamoja na maisha ya kila siku.