Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,900
- 944
Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini na Waziri Cosato Chumi ameshauri serikali kuona namna ya kuangalia ili iweze Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kupungua kidogo ili kuwawezesha watu wengi zaidi kulipa na kulipa kwa hiyari.
Mhe. Cosato Chumi ametoa ushauri huo leo Alhamisi Novemba 09, 2023 bungeni jijini Dodoma akichangia Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa pamoja na Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti kwa mwaka 2024/2025.
"Sisi pale Mafinga tuna shule ya msingi inaitwa Mwongozo ilikuwa na wanafunzi takribani 1,800, serikali ya awamu sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia imetupatia fedha za kutuwezesha kujenga shule nyingine pembeni yake inaitwa Muungano na imesaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi uliokuwepo hapo awali, kupitia hili nampongeza sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan" - Mhe. Cosato Chumi, Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini.
"Katika ukanda wa bahari kuna kitu kinaitwa Blue Carbon, inasiadia udhibiti katika hali ya hewa. Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kila mwaka anahudhuria mkutano wa mazingira, kama mkuu wa nchi tayari ameshatoa support katika hili la hewa ya ukaa. Kuna fedha nyingi katika biashara ya hewa ya ukaa" - Mhe. Cosato Chumi, Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini.
"Nawapongeza JKT Queens ambao wanatuwakilisha kwenye klabu bingwa ya Afrika, wanahitaji alama moja tu waingie nusu fainali, tuwaunge mkono, na tusiishie kuziunga mkono Simba na Yanga. Kitu kizuri wachezaji wa JKT Queens ni wazawa kwa 100%" - Mhe. Cosato Chumi, Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini.