Elections 2010 Serikali ya Kikwete imeleta maendeleo kwa watanzania

Mwafrika

JF-Expert Member
Nov 20, 2006
5,490
226
Angalia na uamue mwenyewe:

2241536655_540d01c2cf.jpg


Hata mtoto huyu kafurahi kabisa na anapata kinywaji bariiiiiiidi:

Dirty+water.jpg
 
Huyu amelala chini kwa furaha baada ya kupongezwa na jeshi la polisi:

2.JPG
 
Huyu yeye kakimbilia kuwakumbatia mapolisi kwa kazi nzuri wanayofanya ya kulinda maslahi ya wastaafu:

Wazee
 
Barabara ya kwenda nyumbani imejengwa:

472127027_716e1cc066.jpg

Mwafrika unanikumbusha mbali - mbona ume paste njia ya kwenda kwetu? hiki ni kipindi cha uchaguzi, greda limefukua miundogo na kuiweka juu, sasa mvua imenyesha imekuwa kasheshe tupu matope kibao. hii kwa maneno mengine inaitwa kasi zaidi, nguvu zaidi na ari zaidi.
 
Huyu anafurahia huduma nzuri za maji:

Tanzania-192-setting-550W.jpg

hili si banda la mbuzi ni nyumba yetu tunaita mbavu za mbwa, yaani ukiwa ndani unaona nje kupitia kwenye matundu matundu, tumeweka kama msingi huo unaouona ili kukinga maji ya mvua za masika yasiingie ndani, maji ya kuoga, kupikia na kunywa tunachota kwenye madibwi.

Zamani enzi za mwalimu tulikuwa na mabomba ( Magati) tulipata maji safi mara tatu kwa wiki huo ulikuwa mpango wa maji safi vijijini miaka ya 80 wakati huo nikiwa shule ya msingi.

Tangu miaka hiyo hadi leo ndugu zangu tunataabika, shida zinazidi kila kukicha, nyie wa mjini tusaidieni wenzenu huku, tunasikia nyie mpo karibu na wakubwa, waelezeni - mbunge wetu tangu aondoke ndiyo amerudi juzi kuchonga hiyo barabara mmeniona hapa tukimuuliza anasema alikuwa anafuatilia sera cha chama chetu ndiyo ametuletea juzi na kutuomba tumchague tena.

Ila kuna mwingine pia amekuja na chama kingine kinaitwa CHADEMA mmhh anaongea vizuri na mipango safi ila sisi tunaogopa vita - hivi tukimchagua huyu hakuna matatizo yoyote? police hawatatukama? niambieni ili niwaeleze na wenzangu hapa kijijini maana huyu wa zamani tumemchoka wajemeni. Mwandishi nakuomba ufikishe picha hii ya mwanangu anayechota maji kwa wanahabari wenzako na wanajamii wa mujini. ila fanya siri nisije kukamatwa.

Ni mimi Usangule wa kalozya.
 
Mwafrika unanikumbusha mbali - mbona ume paste njia ya kwenda kwetu? hiki ni kipindi cha uchaguzi, greda limefukua miundogo na kuiweka juu, sasa mvua imenyesha imekuwa kasheshe tupu matope kibao. hii kwa maneno mengine inaitwa kasi zaidi, nguvu zaidi na ari zaidi.

Hii picha ni kwa hisani ya mchungaji masanilo, alikuwa amekwenda kubariki ndoa somewhere in Tanzania na yakamkuta hayo .... sikujua kuwa ni karibu na kwenu ningekupa credit mkuu.
 
Kwenye ushirikiano wa kimataifa Kikwete ametufanyia mengi ukizingatia alikuwa foreign affairs kwa miaka mingi! Asante Jakaya

pic10.jpg
 
Back
Top Bottom