Serikali ya haki

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Hisia hii ya kumuona mtu mwingine kama sehemu yako, ambaye mna sehemu katika taifa, mna haki na wajibu ndio msingi wa uraia.

Kujitambua huku ndiko kutakako tufanya kuwa taifa lililo kamilika, kumuona raia mwenzako kama ndugu yako ambaye mnachangia Taifa.

Uraia ni kujitambua wewe ni wa kundi gani (Taifa ), ambalo kwa pamoja mna haki na wajibu.

Ambao kwa pamoja mko chini ya uongozi mmoja. Na ndoto zenu ni moja. Pamoja na matumaini yenu kama taifa.

Lakini msingi wa taifa lolote ni haki. Pale haki inapotendeka watu huwa wamoja na hufurahia uraia wao.

Hasa pale rasilimali za taifa zinapotumika kwa manufaa ya wengi.

Na dhamira ya viongozi inapokuwa kwenye kuendeleza watu walio wengi badala ya wachache. Serikali ambayo iko kwa maslahi ya wengi ni imara.

Watu hufurahia na kuipenda serikali ya namna hii. Inayosimamia haki na kuhakikisha rasilimali za taifa zinagawanywa kwa usawa.

Serikali ambayo inatia juhudi kuona watu wengi zaidi wanaendelea. Na haki inalindwa.
 
Back
Top Bottom