A
Anonymous
Guest
Watumishi walioajiriwa mwezi Juni 2022 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe tunaomba haki yetu ya msingi itendeke. Pamoja na kutimiza wajibu wetu wa kazi kwa uaminifu, hadi sasa wengi wetu hatujafanyiwa utaratibu wa kupandishwa madaraja kama sheria na taratibu za utumishi wa umma zinavyoelekeza.
Aidha, watumishi wengi bado hawajalipwa malimbikizo ya mishahara ya kipindi cha mwanzo wa ajira zetu. Madai yaliwasilishwa tangu mwezi Disemba mwaka 2022 lakini mpaka leo hayajaingizwa kwenye mifumo husika ili yapitiwe na kufanyiwa malipo.
Hali hii imesababisha usumbufu mkubwa kwa watumishi, huku tukikosa majibu ya kueleweka licha ya kufuatilia kwa muda mrefu.
Tunaiomba serikali, viongozi wa utumishi na mamlaka husika kuingilia kati suala hili ili watumishi wote walioathirika wapatiwe haki zao kwa wakati. Tunahitaji haki, usawa na uthamini wa kazi tunayoifanya kwa wananchi.