Serikali ya Dr. Kikwete yaanza kuleta matumaini kwa watanzania

Sioni matumaini yeyote yaani mtu anafanya makosa mwenyewe halafu anajihukumu mwenyewe tena kwa maneno matupu bila hatua, inashangaza waziri anazungumza watu kuiba nguzo,tenda za mataili wengine kupokea rushwa hataji hata mtu mmoja wala kumpeleka kwenye vyombo vya sheria huu ni wimbo ule ule wa miaka nenda kenda kufichiana siri na kulindana huyu waziri ni mpuuzi kama wapuuzi wengine walioongoza wizara hiyo
 
Sijakuelewa msimamo wako. "Muislam akiwa Rais, ni neema tu". Neema ipi? Unasema angali Ali Hasan. Tuangalie nini? Fafanua.
Mimi naona unalengo la kutukuza udini. Ni kama mufilisi wa hoja. Hebu jenga hoja na uitetee watu wakuelewe kama ni udini tu bora uende msikitini sio hapa JF watu watakutoa nduki
 
Matumaini ya kupanda kwa garama za maisha kila kukicha, matumaini ya migomo ya madaktari na waalimu! Matumaini unayosemea ni yapi wewe mtoa mada? Kwanza sidhani kama unaipenda nchi yako wewe!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Acha kutumika wewe! Matumaini yapi? Yani jana tu ushaanza kusema matumaini? Tangia 2005 mpaka 2012 July 27 kafanya nin cha maana? Usitumike hovyo hovyo kwa buku2 mbili mkuu![/QUO

Huyu mdau akili hana, hachambui miongozo , mipango na utekelezaji wa serikali yake kwa miaka kadhaa sasa.Mi nitachambua sekta ya nishati miundo mbinu na kilimo ;tangu JK aingie madarakani alikuta tatizo hili, mpaka akafikia hatua ya kukodi mitambo ya umeme wa dharula , na mwisho dowans inayotutesa.Je, sakata hili litokee, nchi imeshakuwa na nishati ya umeme unaotosha na ulitulia kwa bei nafuu?je kama si hivyo kwa miak kumi kilishindikana nini?je hiyo gas ya songosongo serikali haijaweka dhaman pan africa energy wawezekuchimba na kuuza gas bei nafuu.je kama taifa linanufaika kivipi na umeme huo?na je gas hiyo inatosha? na je srikali ilifanya kipi kuwa na majenereta makubwa ya gas kukidhi tatizo la umeme, kama si ngojera?Kilimo;miak ya nyuma kilimo ilikuwa uti wa mgogo, je kwa sasa bado usemi huo upo?je hakuna malalmiko ya bei katika soko la mazo ya kilimo?si kanda ya ziwa si kusini kwenye korosho tatizo ni kubwa.Je serikali haipo?na kama kunakukatishwa tamaa kwa wakulima, kivipi watahamasika kulima kwa nguvu na ufanisi zaidi?je chanzo cha mfumko wa bei si mojawapo upungufu wa chakula?je kama ni hivyo serikali imefanya nini kuhakikisha chakulima kinapatikan kwa wingi zaidi?je bajeti ya 14 bil matumizi ya kawaida + 50 bil maendeleo ya kilimo inatosha kuleta mageuzi ya kilimo?na je 200 bil za bajeti kuu kwenye kilimo zimeishia wapi , mbona kwenye bajeti kilimo hazionekani?na kama ndo hivyo mageuzi ya kilimo na kuongeza chakula itafanikiwa kivipi?tuache daganya toto, mkuu wa nchi ndo kiongozi muhimu , lakini kama ana dhamira ya dhati ni doto kufikia azima ya maendeleo.
 
Huyu Sospether Muhongo namwonea huruma kwasababu Simbachawene yuko upande wa maslahi ya mafisadi wakati Muhongo anasimamia anachokiamini. Hapa tutegemee kufitiniana kwa hali ya juu na baada ya muda mafisadi wakishirikiana na Simbachawene lazima wamzidi maarifa. Tumpe muda akikatiza basi tumshukuru Mungu.
 
kutokana na kusuka upya baraza la mawaziri na ujio wa mawaziri kama Prof Muhongo,Dr Mgimwa,Dr Mwakyembe na uwepo wa Dr Pombe Magufuli waziri toka awamu ya tatu,hakika sasa serikali ya jk imejipanga kuwatumikia wananchi masikini na hivyo kujipanga vema kwa uchaguzi mkuu wa 2015,TUNAOMBA Mh rais uwaache wafanye majukumu yao kwa kujinafasi na kwa uhuru mkubwa,

Sahihisho:- "kuleta matumiani kwa nwatanzania" si kweli wengi hatuna matumani kwa sababu suala siyo nani waziri, suala ni mfumo dhaifu/mbovu unao ongozwa na chama mufilisi. Kama suala ni uchaguzi 2015 sina uhakika kuwa ni mkakati yakinifu, tusubiri kauli ya wapiga kura. Mimi binafsi SINA MATUMAINI
 
kutokana na kusuka upya baraza la mawaziri na ujio wa mawaziri kama Prof Muhongo,Dr Mgimwa,Dr Mwakyembe na uwepo wa Dr Pombe Magufuli waziri toka awamu ya tatu,hakika sasa serikali ya jk imejipanga kuwatumikia wananchi masikini na hivyo kujipanga vema kwa uchaguzi mkuu wa 2015,TUNAOMBA Mh rais uwaache wafanye majukumu yao kwa kujinafasi na kwa uhuru mkubwa,
Yes kuna matumaini makubwa, ila Mh Raisi ameelemewa na maadui wa kisiasa na kwa staili aliyochakuwa ya kumaintain low profile, anahitaji mtu atakae ziba nafasi ya kumaintain political leadership role wakati yeye ana deal na management and administration of the government.

Ni shida maana maadui wame penya mpaka Ikulu na wanatumia mwanya wa security systems na watu washauri wa karibu kutoa advise na kumshauri afanye directives ambazo hazina tija Kitaifa, utaona jinsi Mh Raisi wakati mwingine anapogeuza maamuzi ghafla au kuwa na msiomamo tofauti na kiongozi wake hii ni kutokana na hao waliopo hapo wanajua wanalolifanya. Yes Mawaziri wazuri bado, iko shida kwenye leadership, iko gap.

Na huyu angefaa sana kuwa Waziri Mkuu, ila si Pinda, maana Pinda ana utii na nidhamu ya woga ya hali ya juu na nadhani asingeweza kumwambia kwa uraihisi Mh Raisi, wazo hili si sawa. Unajua hawa wawili Raisi na Waziri Mkuu mmoja wao lazima awe the agresser au anaetoa kauli zenye msukumo wa mara mara na mwingine kuweka na kusimamia mikakati kiutendaji si lazima aongee sana, au basi mmoja akiwa weak mwingine anakuwa strong ili kucomplement each other. Hilo litawatafuna bado CCM, wanahitaji kuweka mambo sawa na ukizingatia na hili tatizo la uchumi (wa mabua) unaopaa, nma sijui unapaa kuelekea wapi wakati budget deficit iko juu na budget za Wizara ziko hovyo tu (Kuongezeka kwa tarakimu au idadi ya pesa hakuna maana iwapo pesa hiyo ilishuka thamani kulinganisha na kipindi kilichopita).
 
kutokana na kusuka upya baraza la mawaziri na ujio wa mawaziri kama Prof Muhongo,Dr Mgimwa,Dr Mwakyembe na uwepo wa Dr Pombe Magufuli waziri toka awamu ya tatu,hakika sasa serikali ya jk imejipanga kuwatumikia wananchi masikini na hivyo kujipanga vema kwa uchaguzi mkuu wa 2015,TUNAOMBA Mh rais uwaache wafanye majukumu yao kwa kujinafasi na kwa uhuru mkubwa,

Mkuu, hao uliowataja ndio wanaoongoza jumla ya wizara zote ishirini na kitu za serikali ya Mhe. JK?
Kama sivyo basi ni tone la maji ndani ya bahari.
Kwa maoni yangu, alitakiwa aweke sura mpya nyingi ili ambao wangesuasua wangekuwa na uoga wa kung'olewa.

Wengi wa mawaziri wake wanaongoza kwa mazoea "business as usual".
Samahani kama nitakuwa nimeku-demoralize, lakini ndio ukweli kwa jinsi niuonavyo mimi.
 
hivi kama isingekuwa ile kura ya kutaka kumng'oa pinda JK angebadili baraza hili kweli...huyu mgimwa anapiga mikelele tu ile wizara haiwezi..mwakyembe ndo hata sipotezi muda kujadili mambo yake maana yeye wizara ya uchukuzi kwake ni treni na ATC..hana upeo na anaugua so hawezi mbio ndefu...
 
Sina hakika km mtoa uzi kamaanisha hyo heading au kafanya km gazet kuweka heading front pg isiyoendana na habari yenyewe!Haoni migomo ya drs,walimu,mafao kuibiwa au anamaanisha serikari imepiga hatua kukimbilia mahakamani?
 
jk amekengeuka huu muda uliobakia katka awamu yake,nina akili timamu na wala situmiki,najua jk miaka mitano ya awamu ya kwanza hakuna alilofanya,lakini kwa baraza ili jipya atleast ni baraza la kumjengea heshma katka awamu yake hii ya mwisho,ni kiasi cha muda na tuvute subira,TIME WILL TELL
 
Kikwete anaingia kwenye vitabu vya historia kama rais mchovu na mbovu aliyeliingiza taifa kwenye matatizo kutokana na kupenda kwake kuzurura na kutumia vibaya madaraka na fedha za umma. Hata angefanyaje hawezi kurejesha imani wala hayo matumaini. Watanzania waliahidiwa maisha bora na siyo matumaini. Tuache mawazo mgando ya kusifia hata upuuzi na sanaa. Yako wapi maisha bora kwa wote zaidi ya genge dogo la wezi kuwateka wananchi na kuwaibia mchana kweupe?
 
Acha kupoteza mda na wezi ccm wewe, ni wachafu huwezi kuwa tambala lao la deki utajikuta na wewe unachafuka kama wao
 
Back
Top Bottom