Serikali ya Dr. Kikwete yaanza kuleta matumaini kwa watanzania

Muislamu akiwa Raisi basi nchi itaingia neema tu ,mkitaka msitake ,Angalia Nyerere angalia Ali Hasan Angalia Mkapa na Kikwete huyo japo walokole wamemsakama.
Mmmh! wewe acha kuharibu hali ya hewa kwa haya madudu yako. Halafu sio lazima uchangie kama unajijua kichwa chako kimebunguliwa.
 
Kweli matumaini yapo:walimu wametangaza mgomo,madaktari wanaenda kufanya kazi nje ya nchi,mfumuko wa bei hamna,viwanda vimefufuliwa hivyo ajira si tatizo tena,shilingi imeanza kupanda thamani n.k Mpuuzi kweli,unafikiri kama maisha ni nafuu kwenye familia yenu basi sote?
 
Hakuna matumaini yoyote zaidi serikali inazidisha mateso kwa raia wema na kuhujumu uchumi wa nchi na kuwalinda mafisadi kwa gharama yoyote.
 
Mpaka mukurupushwe na chadema ndio mnafanya kazi? Tutawaaminije kama mtakuwa consistent? Kwa mfano tuseme chadema leo haipo si CCM watagawana hii nchi kabisa! Sidhani kama kuna matumaini yoyote subiri baada ya muda tu huyo waziri ataambiwa 'kijana taratibu, usiende pupa hii nchi ina wenyewe! Unafikiri kikwete hajui madudu yaliyokuwa yanafnyika Tanesco?

kutokana na kusuka upya baraza la mawaziri na ujio wa mawaziri kama Prof Muhongo,Dr Mgimwa,Dr Mwakyembe na uwepo wa Dr Pombe Magufuli waziri toka awamu ya tatu,hakika sasa serikali ya jk imejipanga kuwatumikia wananchi masikini na hivyo kujipanga vema kwa uchaguzi mkuu wa 2015,TUNAOMBA Mh rais uwaache wafanye majukumu yao kwa kujinafasi na kwa uhuru mkubwa,
 
DSC09159.JPG

Banda la maonyesho ya 8 8

Mkuu Mungi wakati mwingine napata tabu kuamini kama ume-comment wewe haya maneno.
 
Last edited by a moderator:
Muislamu akiwa Raisi basi nchi itaingia neema tu ,mkitaka msitake ,Angalia Nyerere angalia Ali Hasan Angalia Mkapa na Kikwete huyo japo walokole wamemsakama.

Kweli nimeamini, you can't think in an empty stomach!, hadi tuumalize mwezi huu tutakuwa tumesikia pumba nyiingi sana!
 
kutokana na kusuka upya baraza la mawaziri na ujio wa mawaziri kama Prof Muhongo,Dr Mgimwa,Dr Mwakyembe na uwepo wa Dr Pombe Magufuli waziri toka awamu ya tatu,hakika sasa serikali ya jk imejipanga kuwatumikia wananchi masikini na hivyo kujipanga vema kwa uchaguzi mkuu wa 2015,TUNAOMBA Mh rais uwaache wafanye majukumu yao kwa kujinafasi na kwa uhuru mkubwa,

Matumaini? Actions Speaks launder than Words My Friend... Wanaongea tu humo BUNGENI; Tunataka Utekelezaji

Kwanza wawataje hao Wanakamati wa Madini Wabunge waliokuwa wanachota Fedha Kiufisadi za kuomba rushwa

Pili wawataje wale wabunge walioshiriki kupata pesa za Tanesco wakati umeme ukikatwa ili wasirudi 2015

Tatu tuone Mikataba yote inatajwa kwa wananchi kabla ya kusainiwa sio kusainiwa kisiri-siri kama Kikwete alivyokuwa

anapenda, na Kamati ya Mawaziri wake... ili tusijue ni kina nani wanabeba hizo 10%; transparency

Nne Tuone kweli Wananchi walala hoi wanafaidika na Mapesa ya GAS, GOLD na huko GEZAULOLE hiyo Ardhi inarudishwa

kwa walala hoi waliotoa pesa zao kwanza sh. 30,000.00 na Sio kina Miraji Kikwete, Ngeleja kids n.k

* MATUMAINI hayatakuja kwa miezi 2 wakati Uharibifu ulianza tangu Kikwete achukue Ungwe na hata kabla hajabeba

Urais - Tangu AZIMIO LA ZANZIBAR; CCM kukumbatia MATAJIRI na kujiita CHAMA CHA MAFISADI
 
Ni ngumu kumfundisha mbwa mzee mbinu mpya.Sioni kama ndio suruhisho.Hatuoni fisadi papa kufungwa maisha ,,tunasikia kele na mipasho za waheshimiwa wabunge.
 
Kwa miaka hii iliyobaki naamini serikari ya JK itafanya makubwa na kurudisha imani kwa wananchi.
Tatizo aliwaamini sana hawa jamaa zake ndio waliomwangusha.Alikuwa na nia nzuri sana kwa nchi yake.
Kaeni mkao wa kula makubwa yanakuja.
LWLNLW
 
Mmuuuphuuuu! Huwa nakasirika sana nikisikia mtu anasifia serekali ya DHAIFU! Atakachojivunia ni kule kujamb..a viti vya magogoni tu hakuna kingine!
 
Usitudanganye matumaini yatapatikana iwapo waziri mwenye dhamana na serikali ya JK itataifisha mali walizojilimbikizia na kurudishwa serikalini na kutumika kwa ajili ya manufaa ya Taifa, Fedha walizohifadhi Uswisi zikowapi, Fedha za EPA tunaambiwa wamerudisha nani karidisha na ziko wapi, Fedha za chenji ya RADA ziko wapi? hatudanganyiki kusafishika kwa serikali hii inahitaji kuchukua maamuzi magumu ambayo hayawezekani kwa sababu full system inahusika.
 
Tatizo lenu wanajamii mnahangaika na wanywa gongo humu mtu kalewa zake gongo huko kigogo na kuja hapa kupost vitu visivyo na utafiti wa kutosha nanyi mnahangaika nae.
 
kutokana na kusuka upya baraza la mawaziri na ujio wa mawaziri kama Prof Muhongo,Dr Mgimwa,Dr Mwakyembe na uwepo wa Dr Pombe Magufuli waziri toka awamu ya tatu,hakika sasa serikali ya jk imejipanga kuwatumikia wananchi masikini na hivyo kujipanga vema kwa uchaguzi mkuu wa 2015,TUNAOMBA Mh rais uwaache wafanye majukumu yao kwa kujinafasi na kwa uhuru mkubwa,
Mkuu BMT ni kweli mwanga umeanza kuonekana. Kwa sasa ni hakika watanzania wanaanza kuona kuwa serikali inawatumikia kuliko hapo nyuma. Twende mbele turudi nyuma kwenye umeme huko sasa tunaanza kuona nuru.
 
Last edited by a moderator:
Umesahau lingine ambalo ni "mjinga"hajui kinachoendelea hapa nchini na ameridhika na kurubuniwa na kofia,kanga,chumvi n.k na kuwa ngazi ya kupandia ya wanasiasa.

Asante sana mkuu kwa kunikumbusha na nlishamjibu Poyoyo mmoja hapo juu ambaye amekimbia bila kujibu hoja.

Pamoja tunaweza.
 
kutokana na kusuka upya baraza la mawaziri na ujio wa mawaziri kama Prof Muhongo,Dr Mgimwa,Dr Mwakyembe na uwepo wa Dr Pombe Magufuli waziri toka awamu ya tatu,hakika sasa serikali ya jk imejipanga kuwatumikia wananchi masikini na hivyo kujipanga vema kwa uchaguzi mkuu wa 2015,TUNAOMBA Mh rais uwaache wafanye majukumu yao kwa kujinafasi na kwa uhuru mkubwa,

Na wale mafisadi walioambiwa warudishe wenyewe mabilioni ya shilingi waliyokwapua, je walirudisha? Hivi kauli mbiu ya maisha bora kwa kila mtz umeanza kuisikia tangu lini? Hakuna jipya!
 
Back
Top Bottom