Greenwhich
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 1,337
- 968
Hai. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameingia matatani baada ya Mahakama ya Wilaya ya Hai kuona ana kesi ya kujibu katika mashtaka ya kumshambulia mwangalizi wa ndani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Uamuzi huo ulitolewa jana na hakimu mfawidhi wa wilaya hiyo, Denis Mpelembwa mbele ya Mbowe, wakili wake, Issa Rajabu na mwendesha mashtaka, Inspekta Marwa Mwita.
Mpelembwa alisema mashahidi saba wa upande wa mashtaka wameishawishi mahakama kuwa siku hiyo kuna tafrani ambayo ilitokea na ambayo Mbowe
atatakiwa kutoa ufafanuzi wa kuhusika kwake.
Alisema ingawa upande wa utetezi ukiongozwa na wakili Albert Msando na baadaye Rajabu, ulitoa hoja kuwa ushahidi wa Jamhuri uliacha mashimo mengi, yeye anaona Mbowe ana kesi ya kujibu.
"Katika hoja zao (utetezi) wanaona ukiacha ushahidi wa Nassir Yamin, hakuna shahidi mwingine aliyethibitisha kushuhudia Nassir akipigwa," alisema akinukuu hoja za mawakili wa utetezi.
Hakimu aliongeza kusema: "Utetezi pia walitoa hoja kuwa upande wa mashtaka ulishindwa kuwaita akina mama ambao wanaodaiwa kushuhudia, hivyo kuacha mashimo mengi katika ushahidi wao."
Hata hivyo, hakimu alisema katika hoja zao ambazo ziliishawishi mahakama, upande wa mashitaka ulijibu kuwa sheria haiwabani kuleta kila shahidi kujenga msingi wa kesi yao.
"Ni rai yao (mashtaka) kuwa mashahidi wao saba wameweza kuthibitisha shtaka dhidi ya mshtakiwa pasipo kuacha mashaka ama mianya kama utetezi walivyodai," alisema Mpelembwa.
Hakimu Mpelembwa alisema baada ya kupitia hoja za mawakili wa pande zote mbili, anaona upande wa Jamhuri umeweza kuishawishi mahakama kuwa mshtakiwa ana kesi ya kujibu.
Kutokana na uamuzi huo, Hakimu alisema mahakama inampa nafasi Mbowe kujitetea na kesi hiyo imepangwa kutajwa Julai 17, siku upande wa utetezi utakapotoa orodha ya mashahidi wao.
Katika uchaguzi huo mkuu wa 2010, Mbowe aliibuka mshindi kwa kupata kura 28,585 akifuatiwa na Fuya Kimbita (CCM), kura 23,349, Hawa Kihogo (UDP) 258 na Petro Kisimbo (TLP) 135.
pamoja na kumuongezea umaarufu kwa sababu atashinda kesi hiyo pia ndivyo ccm wanavyozidi kujivua ngozi na wanachi wa kada ya chini wanazidi kuufahamu mzimu wao unaowala taratibu ingawa miaka ya hivi karibuni wamepongeza kasiMbowe asijali kwani anazo kesi kibao.Hii moja haitamfanya kushindwa kutekeleza majukumu ya ukawa
Bawacha wote mnapotoshana kila kukicha nani kakwambia kuwa mbowe ni marufu kwenye nchi hii,kwa tarifa yako umarufu wa mbowe pengine upo kwenye uharifu na uendeshaji wa disco za usiku.pamoja na kumuongezea umaarufu kwa sababu atashinda kesi hiyo pia ndivyo ccm wanavyozidi kujivua ngozi na wanachi wa kada ya chini wanazidi kuufahamu mzimu wao unaowala taratibu ingawa miaka ya hivi karibuni wamepongeza kasi
Alifungwa muda gani?
sibishani na haja kubwa mimi! na wala sijashikiwa akili kama wewe unapanukwa tuBawacha wote mnapotoshana kila kukicha nani kakwambia kuwa mbowe ni marufu kwenye nchi hii,kwa tarifa yako umarufu wa mbowe pengine upo kwenye uharifu na uendeshaji wa disco za usiku.
miaka yote4 walikiwa wapi?Chadema mnapaswa kutii sheria bila shuruti...!!
It's non of your business.Mbowe alimpiga vibao wakala wake kwa kuhisi kuwa anapanga kumsaliti.
Yaambie maccm yatii sheria ya mabadiliko ya katiba.Chadema mnapaswa kutii sheria bila shuruti...!!
madhara ya kutumia kichwa kufugia tu nywele yameanza kukutesaQuote: CCM. - CHAMA CHA MACHUMA ULETE - duh! ... hakika hakuna haja ya kubishana nao!!!
Mbowe anapaswa kutii sheria bila shurutiYaambie maccm yatii sheria ya mabadiliko ya katiba.
Kwa kujadili maoni ya wana nchi
Kweli kabisa Mkuu.madhara ya kutumia kichwa kufugia tu nywele yameanza kukutesa
Sheria ni sheria tu haijalishi kosa limetendeka linimiaka yote4 walikiwa wapi?
Sheria wameijua leo? UKAWA hawatorudi bungeni kwa style hii ng'o
sheria ni msumenokatika kile kinachoonekana kumweka bussy mwenyekiti wa chadema freeman mbowe tayari kesi iliyofunguliwa miaka minne huko nyuma imefufuliwa.
Kesi hiyo iliyoratibiwa na ccm alifunguliwa mbowe kipindi cha uchaguzi mkuu uliopita kwa madai kwamba alimshambulia msimamizi wa uchaguzi huko hai.
Hapo jana kesi hiyo iliibuka na hakimu akasoma kile kilichosemwa ni hukumu ya awali kwa kusema kwamba mbowe ana kesi ya kujibu na anapaswa kujitetea.
Ikumbukwe kwa sasa mbowe mbali ya kuwa mwenyekiti wa chadema ndiye mwenyekiti pia wa ukawa na ndiye kinara wa mapambano ya katiba ya wananchi.