1. Kwa kulea ufisadi wa Epa, Kagoda, Meremeta, Tangold, Deep Green, ICS, IPTL, Rada,TRL, TICTS, Kiwira, mikata mibovu ya madini, nk, nk
2. Kwa kuanzisha Richmond/Dowans, kuwakingia kifua wezi wote, kuchakachua, elimu ya watoto wetu kura zetu, majeshi yetu, usalama wa Taifa letu, TAKUKURU yetu (kwa kuzigeuza kuwa taasisi za CCM),na kufifisha kabisa moyo wa utendaji kazi miongoni mwa watumishi waaminifu wa umma
3. Kwa kuruhusu uporaji wa mchana wa rasilimali za Taifa letu (madini, magogo, ardhi, samaki, nk, nk) na hivi sasa mchakato wa malipo ya DOWANS
4. Kwa kuwakosesha mamilioni ya watanzania huduma bora za Barabara, Maji (achilia mbali safi na salama), Umeme, Huduma za afya na elimu bora, na biashara ya ulanguzi wa haki inayoendeshwa hadharani na idara za Mahakama, usalama wa raia, idara za ardhi, nk, nk
Na mengine mengi ambayo sijayafahamu bado, vinanifikisha mahali ambapo nabaki sina uchaguzi mwingine zaidi ya kumtangaza rasmi JK, Makamba na CCM yao ambayo imetutawala kwa miaka 50 (nusu karne!) sasa kuwa JANGA LA KITAIFA! Watanzania tafakari.