Ibinzamata
Member
- Nov 16, 2007
- 12
- 0
Ndugu zangu, tutafakari kidogo.
Kwa miaka mitano ya utawala wa JK, nchi yetu imekumbwa na balaa la hali ngumu sana ya maisha. Leo Watanzania tunakabiliwa na balaa kubwa la mfumuko wa bei katika kila bidhaa tuinunuayo. Takwimu zinaonyesha kila bidhaa imepanda bei mara mbili ya ilivyokua miaka mitano iliyopita. Hii inamaana gani? Uwezo wa mtanzania kununua bidhaa unapungua, hivyo biashara zinadorora, serikali inakosa mapato, ajira zinapungua, vipato vya watanzania vinapungua, uwezo wa watanzania kujikimu unapungua hivyo njaa, maradhi, umaskini vinaongezeka.
Watu wanaripotiwa kula mlo mmoja, familia kushindia uji, kusaga ubuyu na unga wake kuwa mlo, Matukio ya watu kuuana, kujeruiana, kukatana mapanga, kuchomana viganja nk., kwasababu tu ya kuiba mboga, kupoteza pesa za kuhemea dukani, kuunguza mboga nk yanaongezeka kila siku. Watu wanakata tamaa.
Haya yanatokea JK wetu yuko busy kuendeleza mzaha IKULU. Kila kitu kwake Ucheshi na burudani. Hajui nini afanye kukomboa Taifa ili. Akipewa nafasi na vyombo vya habari kuelezea mikakati yake ya kukomboa Taifa ili, yeye hupata kigugumizi wkt wa kujibu maswali, (tuna tuna tuna tuna jipanga, nina nina nina nina mpingao... mare mare mare mare marekani wameahidi....) Lkn akiwa kwenye mizaha yake huwezi kusikia hicho kigugumizi. Anaongea kama watu wa mipasho.
Karudi madarakani kwa ila, na marafiki zake ambao Taifa limewanyooshea vidole kwa kuliangamiza na ufisadi, sasa wameshika kasi kurudi kwenye hatamu za uongozi na wala JK hashtuki. Keshokutwa ataondoka na atawaachia madaraka wao. Tena kwa mabavu haya haya ya kuchakachua maamuzi ya wananchi.
Kuondoka na aondoke, lkn, kwanza atawaacha wananchi katika hali mbaya sana ya maisha baada ya utawala wake mbovu, na pia ataiacha nchi mikononi mwa majangili ambao ndio watapingilia misumari ya mwisho mwisho kwenye majeneza mengi ya watanzania watakaokua wanakufa kwa umaskini wa kutupa, njaa, ujinga, maradhi, magomvi, chuki, nk. Nchi iko katika janga. Janga ili ni RAIS wetu mwizi wa KURA. Tunakwisha. Tusipotafakari na kufanya maamuzi ya haraka kama waTZ, jua lazama