Decemba 9, 2011 Kama taifa tutakuwa tuna sheherekea miaka 50 ya uhuru, hii ni nusu Karne. Kuna nchi zimepata uhuru miaka ya karibuni zaidikuliko sisi lakini ukiweka kwenye mizani na Tanzania sisi tuko nyuma kimaendeleo. Zaidi ya 40% ya watanzania wanapata mlo mmoja kwa siku, zaidi ya watanzania 60% hawa wanatumia kiwango cha chini ya USD 1 kwa siku. Vifo na maradhi kwa wakina mama wajawazito na watoto vinazidi kuongezeka kila siku, Malengo ya Millenium Development Goal (MDG) Kamwe hatutafikia labda kama juhudi za kuchakachua zitafanyika.
Umeme bado ni tatizo, hivi serikali inategemea itakuza uchumi kwa minajili hii ya gizani? Uzalishaji wa viwanja na sekata zote za uchumi zinadumaa. Kama kawaida tunapewa ahadi nyepesi na uwongo tunaridhika. Nimeangalia bunge ni usanii tu. Ni watanzania wenzetu wachache sana wanaweza kufikiri na kujua kwanini wako bungeni. Badala ya kuipa changamoto serikali imekuwa ni sehemu ya kupongezana na kutongozana kisiasa.
Binafsi naona CCM ni janga la taifa hili, ili tuendelee basi ifike wakati basi wakubali wameturudisha nyuma sana. Nenda Kigali, Bunjumbura migao ya umeme ni historia, barabara kiwango cha lami. Miji haina foleni sababu miji hiyo imepangwa. Dar es Salaam ni aibu. Kuna siku Mch nimetoka Mlimani City kufika Millenium Tower imenichukua Masaa 3..ningeweza kwenda Morogoro na Kurudi sababu kubwa siku hiyo Mh alikuwa anakwenda fungua bara bara Mwenge ya kwenda Bagamoyo.
Kila siku ni ahadi, uwongo na uzembe unalelewa na hawa waliomadarakani, wamelewa kabisa na wako usingizini...majibu mepesi Tanzania inaendelea sana linganisha na wakati wa uhuru. Huu ni uchuro, wizi na ufisadi wa keki ya taifa uanatudumaza. Mgao wa umeme na foleni si wa CHADEMA, CCM, TLP, CUF, Waislam, Wakristu, waislam, Pagan sote twaathirika. Jamani imetosha sasa Mzee Jakaya huwezi fanya maamuzi magumu pumzika tuanze upya kama taifa.Tumekuwa kama tumelogwa hatuwezi jadiliana kwa tija, ushabiki na ujinga. Soma michango ya wanaJF wengine ni aibu mtu anayejua tumia computer lakini hana fikira za kuchangia maendeleo ya nchi. Slogan za Tanzania ni nchi ya amani lakini maskini zimetuchosha.
CCM ni janga la taifa
Mch Masa K