Serikali ya CCM na mpango wake wa “Big Results Now”:Tutafanikiwa kweli kwa huu mkakati?

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
1,959
872
Hivi sasa serikali ya CCM imekuja na mpango wake mpya uliobatizwa jina la kizungu la Big Results Now. Binafsi aliyeaanza kunifanya nitazame kwa macho mawili kuhusiana na mpango huu ni Waziri wa Nishati na Madini ambaye amekuwa kwa kiasi kikubwa kama mbunifu mwenyewe wa mpango huo.Mara kadhaa amekuwa akionekana akitoa matangazo ya wito huu wa Tanzania kuja na matokeo makubwa sasa.

Pengine wote kwa pamoja lazima tuulizane huu mpango wa matokeo makubwa sasa una maanisha nini.Mimi sijajua kabisa kuwa malengo makuu ya haya mambo ni nini, lakini nimebahatika kuona kile kinachoendelea katika idara ya elimu.Sijui idara zingine za serikali kama vile Nishati na Madini wao wamepanga kutuonesha nini, lakini niseme tu kama huko nako kuna mpango kama huu wa sekta ya elimu basi tumepotea kabisa katika kubuni “matokeo makubwa sasa”.
Labda niwashirikishe yanayoendelea sasa kwenye elimu ya sekondari.Baada ya mwaka huu serikali kupata aibu ya matokeo mabaya ya kidato cha nne 2012 na baada ya malalamiko mengi kutoka kwa wadau na wananchi wa kawaida juu ya matokeo hayo, serikali iliamua kubatilisha na kuja na matokeo mapya. Hivi sasa serikali imepanga kuondoa aibu hiyo katika mtihani ujao utakaofanyika Novemba 2013, japo haijatamka rasmi lakini kwa macho maangavu utaona ni kama wanataka kujinasua na aibu hiyo.
Serikali hivi sasa imewakusanya baadhi ya walimu wa masomo manne ya kidato cha nne kila wilaya na kila shule ya sekondari, na kuwapa “semina elekezi” juu umuhimu wa masomo hayo kufundishwa kwa” umakini” katika kipindi hiki kilichobaki kabla ya mtihani wa kidato cha nne Novemba 2013. Serikali inataka kuondoa aibu ya mwaka huu isijitokeze tena mwakani.Masomo hayo ni Hisabati, Sayansi(Physics and Chemistry) na Kiingereza. Katika masomo hayo zimechukuliwa mada nne ambazo walimu hawa wanafundishwa. Tukumbuke kuwa walimu hawa wanafundisha haya masomo mashuleni, lakini kwa mujibu wa waelekezi wanasema serikali imesisitiza topics hizo zilizopendekezwa , walimu wafundishwe tena.
Walimu hawa kila baada ya kumalizika kwa topics wanafanyishwa mtihani. Na kituko kikubwa ni kuwa wakufunzi wanasema wazi kuwa maswali ambayo yanaulizwa ndio hayo hayo wakawafundishe wanafunzi wao kwani ndio yatakayotoka kwenye mtihani wa mwisho Novemba 2013.Usisahau kuwa walimu pia katika siku hizi 5 wanazofundishwa wanalipwa posho ya siku shilingi 15,000/=.

Labda kuna mwerevu mwingine anaweza kuuliza kwanini masomo manne tu wakati ufaulu wa mwanafunzi unaanza na masomo 7. Jibu toka kwa wakufunzi ni hili kuwa haya masomo manne ndio yanayoongoza kwa kufelisha wanafunzi.Lakini pia kama mwanafunzi atafaulu masomo haya 4 basi idadi ya sifuri na daraja la nne zitapungua na hivyo kuongeza asilimia ya ufaulu badala ya kila mwaka kushuka.Lakini pia kuna jibu la ziada toka kwa wakufunzi ni kuwa mtu akifaulu somo la hesabu na Kiingereza basi mengine kama historian a civics anaweza kufaulu. Haya ndio matokeo makubwa sasa tunayoyasubiria mwakani. Je huu ndio mpango wa kuzalisha matokeo makubwa sasa?Je sekta zingine kam afya nako wamebuni nini?

Lakini la mwisho ambalo walimu wamepewa kama motisha ya kuipenda CCM baada ya mahusiano yao kudorora ni kuwa serikali imeamua kubadilisha madaraja ya walimu na kuwapandisha na kuwapa mshahara “mkubwa”.Anasema utafiti uliofanywa na serikali ni kuwa walimu wanaichukia sana CCM na serikali yake.Na hivyo wamemwaga “sumu ” sana kwa wanafunzi pamoja na wanachi wengine.Hivyo kwa sasa imeamua kumalizana na walimu ili mwakani uchaguzi wa serikali za mitaa utoe “big results” pamoja na ule wa 2015.

Is this a big result now from big men and women? Shall we succeed with this strategy? Let us wait for it. Let me borrow words from Jenerali Ulimwengu as written in his Weekly Column in RaiaMwema tabloid, “Where will Big Results come from without Big Ideas, which are born of Big thinking by Big Men and Women? Petty thinking never produced big results anywhere.”
 
Mkuu semina hizo ni kitu cha kawaida kwa walimu. Na semina nyingi kibongobongo zipo ktk masomo ya sayansi na suala hili lipo toka cku nyingi wakati niko olevel miaka hiyo walimu walikuwa wanahudhuria. Suala la mshahara kusema serikali ni kujisogeza kwa walimu unakosea na kuonyesha dharau kwa walimu. Ni haki kuongezewa mshahara.
 
Mkuu semina hizo ni kitu cha kawaida kwa walimu. Na semina nyingi kibongobongo zipo ktk masomo ya sayansi na suala hili lipo toka cku nyingi wakati niko olevel miaka hiyo walimu walikuwa wanahudhuria. Suala la mshahara kusema serikali ni kujisogeza kwa walimu unakosea na kuonyesha dharau kwa walimu. Ni haki kuongezewa mshahara.
Unahitaji nikupenyezee waraka ndipo uamini?Niambie semina za wiki hii yote zina husu nini na lengo ni lipi?Kahudhurie hata kwa kuiba tu kama si mwalimu uone kinachoongelewa.Kesho ni mwisho kumbuka kama unahitaji kuhudhuria.
 
Unahitaji nikupenyezee waraka ndipo uamini?Niambie semina za wiki hii yote zina husu nini na lengo ni lipi?Kahudhurie hata kwa kuiba tu kama si mwalimu uone kinachoongelewa.Kesho ni mwisho kumbuka kama unahitaji kuhudhuria.

Penyeza huo waraka mkuu. Ili tuöndokane na sntofahamu kuhusu maslah ya walimu
 
BIG RESULTS NOW ni kauli tu sawa na kauli zilizowahi kuja zikaondoka kapa kama vile MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA na KILIMO KWANZA isipokuwa hii moja tu ambayo naona imeleta matokeo ya KASI MPYA,MAGARI MAPYA NA UFISADI MPYA.

Hiki mkuu unachokisema ni kweli kipo japokuwa huku nilipo mimi nadhani semina kama hii inayofanyika huko itafika in two or three weeks times.Isipokuwa mimi nilihudhuria semina ya wakuu wa shule waliitwa kupewa maelekezo namna ya kuleta/kusababisha MATOKEO MAKUBWA. Waliambiwa mwaka huu ni lazima ufaulu upande/uwe 60%, kisha mwakani 2014 uwe 70% na ifikapo 2015 ufaulu kidato cha nne sharti uwe 80%.

Binafsi sina tatizo na mpango mzima kwani ni mzuri tu iwapo utawekewa mikakati sambamba na raslimali watu na fedha ya kutosha. Hofu yangu kubwa kwamba mpango huu ni vigumu kufanikiwa kwa sababu zifuatazo;
  1. Kama nilivyosema awali hakuna raslimali watu (walimu) wa kutosha pamoja na fedha. Mfano ni utani uliopitiliza kumchukua mwalimu toka kwake na kuacha familia yake na mishemishe zake zingine za kipato unamweka mahali kutwa nzima kwa posho ya Tsh. 15,000=!!
  2. Baadhi ya shule nyingi za kata za vijijini hazina kabisa walimu wa masomo hayo (Maths,Biology,English Language na Kiswahili).Kama anayeleta ubishi ktk hili atembelee shule za vijijini atathibitisha hili kwa urahisi kabisa kwani hata wale waliopangiwa mwezi machi mwaka huu walio wengi wameshaingia mitini kutokana na ugumu wa waliyokumbana nayo huko!! km vile ukosefu wa nyumba za kuishi walimu,maji na umeme na sehemu zingine hata mawasiliano ya simu tu!
  3. Wanasiasa hasa madiwani na wenyeviti wa vijiji kuingilia uendeshaji wa shule hizi ni tatizo na kero kubwa inayowaudhi walimu.Mfano unaweza kukuta maeneo mengine hawa jamaa wanasiasa kwa sababu ya ujinga wao wanawashawishi wazazi na wanafunzi kugomea kulipa ada na michango mbalimbali halali ya shule iliyowekwa na serikali yenyewe ambayo ndiyo inaendesha shule hizi km kulipa walimu wanaojitolea wa kidato cha sita,wale wanaofundisha kwa muda wao wa ziada na wakati huohuo serikali haitoi fedha ya ruzuku kwa ajili ya shule hizi kujiendesha ili kuleta MATOKEO MAKUBWA!!
  4. Kuna baadhi ya watendaji katika ngazi za juu kama wakurungezi na Maafisa Elimu maamuzi yao ni kipuuzi na kijinga sana na kukera sana walimu.Niwape mfano mmoja kuna DED wa wilaya moja kanda ya ziwa(anajijiua atakaposoma uzi huu kwani kesi iko CWT) amehamisha walimu 12 wa sekondari tena walimu hawa ni wa Wakuu wa Shule(Head of Schools) toka mwezi wa Machi mwaka huu.Inasiktisha kuwa mkuerungezi huyu alichukua uamuzi huu wa kuhamisha huku akitambua kuwa hana fedha za uhamisho za kuwalipa walimu hawa kwani mpaka leo hawajalipwa na utwaonea huruma wanavyohangaika kila siku kufuatilia pesa yao ya uhamisho zaidi ya miezi mi3!!.....Utapata wapi BIG RESULTS NOW katikati ya mazingira haya na watendaji wabovu kma hawa??.Funny enough alipobanwa kwanini amehamisha walimu hawa huku akitambua hana fungu la kugharamia hilo alijibu kuwa alilazimishwa na Baraza la madiwani kwani walimu hao waliokuwa ni chanzo cha CCM kupoteza umaarufu katika maeneo hayo.Aidha alisema pia walitegemea pesa ingeingia kabla ya mwaka wa fedha kwisha lakini wanaamini pesa ambayo ilikuwa ije kama OC na kuwalipa walimu imetumika kugharamia ugeni wa Rais Obama wa Marekani!!...kituko
  5. Walimu wengi wanaidai serikali madeni ambayo mengine yanatia hadi kichefuchefu kwani ni ya miaka kibao mpaka walimu walishachukia kiasi ambacho chuki hiyo imeshafikia kiwango cha kuwa-frustrate na kukata tamaa na wanatafuta sehemu tu ya kuja kuitua chuki hiyo ili wapumue....ambayo nina uhakika kabisa ni kufutilia mbali CCM kupitia sanduku la kura na ni mwaka 2015 tu!!.....It is a day dream and almost impossible to get the so called "BIG RESULTS NOW" in education sector under such circumstances!!
  6. Ukosefu wa miundo mbinu bora ya kufundishia na kujifunzia kama vile Maabara,nyumba za walimu,madawati,vitabu vya kiada na ziada katika mashule yetu ya sekonadari mengi hasa hizi za kata za vijijini kunakoambatana na upungufu mkubwa wa walimu...How can you get BIG RESULTS under this condtion??
  7. Utoro ni tatizo jingine kubwa kabisa ambalo linasumbua shule za sekondari nyingi za kata. Kuna shule moja niliitembelea wilaya shinyanga (V).Shule ina jumla ya wanafunzi 467 kidato cha I - IV lakini wanaohudhuria shule tena kwa kubipubipu ni kama wastani wa wanafunzi 120 kila siku!! nilpomuuliza mwalimu mkuu sababu ni nini hasa zinazopelekea tatizo hili la utoro,alisema ni mimba,wazazi/walezi kuwa na mwamko mdogo wa elimu ambao wengi huhonga watendaji wa kata na vijiji ili wasiwasumbue ili watoto wao waache shule na wengine huozesha mabinti zao!!..BIG RESULTS IN EDUDATION NOW.........HOW??

Mwisho nikubaliane na Jenerali Ulimwengu kuwa BIG RESULTS NOW haiwezi kuja iwapo tutakuwa na watawala wenye fikra zilezile,sera zilezile na mazoea yaleyale. Na kibaya zaidi wanabuni vitu huku wakiamini kabisa kuwa ni vigumu kutekelezeka ktk mazingira na mfumo walioujenga.....mfumo wa kifisadi, mfumo ambao emeathiri kila eneo la maisha. Sisi tumewaacha tu wahangaike na tunatambua kabisa mwisho wa siku ni mwalimu anayebaki na mwanafunzi huyu wala si wao. Labda kama wanaandaa mazingira ya kuwaibia mitihani vijana hawa ili sifa zao kisiasa zivume....na huu utakuwa ni ujinga na upumbavu uliopitiliza na chini ya CCM hili linawezekana bila chenga!!
 
Kingine ni kuwa kuanzia mwez wa 8 kutakuwa na remedial kwa form 4 kwa kipindi kimoja(1 hr)mwalimu husika atalipwa tsh 2000.na ratiba ishatolewa nchi nzima!j'3 ni engl and phy kila siku masomo ma2.buku 2 si utani uu......big result now
 
BIG RESULT NOW! imehamusha hasira za walimu kwani kituo cha mkoa wa ruvuma walimu wamelipwa tsh 40000/= tu kwa siku zote walizohudhuria pamoja na mateso yote waliyoyapata.BIG RESULT NOW bado ni kitendawili kikubwa shame kwa CCM na ujinga wao.
 
kinachotakiwa ni mazingira ya kufundishia kuwa rafiki na walimu kutambuliwa. Cho chote nje ya hili ni kutwanga maji kwenye kinu.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Kingine ni kuwa kuanzia mwez wa 8 kutakuwa na remedial kwa form 4 kwa kipindi kimoja(1 hr)mwalimu husika atalipwa tsh 2000.na ratiba ishatolewa nchi nzima!j'3 ni engl and phy kila siku masomo ma2.buku 2 si utani uu......big result now

c afadhal nyie wa buku 2, wenzenu mpango ushaanza na 2nalpwa buku only.
 
Mkuu semina hizo ni kitu cha kawaida kwa walimu. Na semina nyingi kibongobongo zipo ktk masomo ya sayansi na suala hili lipo toka cku nyingi wakati niko olevel miaka hiyo walimu walikuwa wanahudhuria. Suala la mshahara kusema serikali ni kujisogeza kwa walimu unakosea na kuonyesha dharau kwa walimu. Ni haki kuongezewa mshahara.

Hebu ongea kwa data au nyaraka ili tukuelewe.
 
Labda tungekuja pia a suluhuhisho badala ya kuanisha matatizo kila siku!
 
BIG RESULT NOW! imehamusha hasira za walimu kwani kituo cha mkoa wa ruvuma walimu wamelipwa tsh 40000/= tu kwa siku zote walizohudhuria pamoja na mateso yote waliyoyapata.BIG RESULT NOW bado ni kitendawili kikubwa shame kwa CCM na ujinga wao.


Nina wasiwasi kama tumeielewa vizuri hii vision, sidhani kama inamaanisha results za mitihani. Hii Nathani itakuwa imezizika zile za kilimo kwanza, ari mpya,...., na ari zaidi, kasi zaidi,.... Ni vision and mission statements zisizokuwa na indicators wala visible outcomes ama impacts
 
BIG REVERSE NOW.
Huku kwetu Mpwapwa wanalipa kila mshiriki sh 100,000 kwa semina yote. Na shule ishaoa cheki jana. Halaf hiyo remedial class mkuu katangaza Tsh 5000 kwa kipindi. Lakin kuna post humu naona kama kuna mkanganyiko! Au ndo tayari hizo Bil 25 zimeshaanza kutafunwa?
 
Yani hiyo BIG RESULT NOW ni kituko wametoa pre national kwa primary yani maswali kumi na mbili majibu yamekosewa yani nchi hii kwa kauli mbiu huiwezi mikwara kibao!
 
Huu ni msamiati kama ilivyo mingind kama, kilimo kwanza lakini pembejeo bei juu, maisha bora kwa kila mtanzania mikakati hakuna. Kilimo cha kufa na kupona.

Utofauti kwamba hii ipo kwa kiingereza

angalia grade mpya
0 - 39 F
40 - 54 D
55 - 64 C
65 - 79 B
80 - 100 A
 
Masahihisho kidogo;
1.Masomo yaliyolengwa ni:mathematics,kiswahili,english na biology.
2.kuhusu walimu kupandishwa madaraja bado ni kizungumkuti,usiwape walimu matumaini yasiyokuwepo.Unaouhita
walaka kila mtu anaukana.

Mkuu kama unavoeleza ni kweli kabisa lengo la hizi semina ni kuwaandaa walimu wawaandae wanafunzi katika haya masomo manne tu,na lengo si wanafunzi kuyaelewa haya masomo bali wakaririshwe kwa yale tu yatakayoletwa kwenye mitihani ili kuondolea aibu serikali.

Lakini kwa hali ilivyo hata kama wanafunzi hawa wangepewa majibu kuyaamishia kwenye karatasi watashindwa tu
 
Back
Top Bottom