Rais Dk. Mwinyi: Elimu ni kipaumbele kikubwa cha serikali

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
478
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ya awamu ya nane imeweka kipaumbele kikubwa katika sekta ya elimu kwa kuongeza bajeti, kuimarisha miundombinu kwa kujengwa shule zenye vifaa vya kisasa, pamoja na kuajiri walimu wa masomo ya sayansi ili kuongeza kiwango cha ufaulu wa wanafunzi.

Rais Dk. Mwinyi amesema hayo katika hafla fupi ya chakula cha mchana na kuwapongeza wanafunzi waliopata ufaulu wa daraja la kwanza kwa kidato cha nne mwaka 2022 na kidato cha sita mwaka huu aliyowaandalia viwanja vya Ikulu Zanzibar tarehe 12 Novemba 2023.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi ameeleza kuwa Serikali itahakikisha inaongeza fedha ili kila mwanafunzi mwenye nafasi ya kuendelea na masomo ngazi ya elimu ya juu anapatiwa mkopo.

Vilevile Rais Dk. Mwinyi ametoa zawadi ya laptop moja kwa kila mwanafunzi aliyefaulu kiwango cha daraja la kwanza wa kidato na nne na sita kwa skuli za Unguja na Pemba jumla 1,450.
IMG-20231112-WA0019.jpg
IMG-20231112-WA0017.jpg
IMG-20231112-WA0018.jpg
IMG-20231112-WA0020.jpg
IMG-20231112-WA0021.jpg
IMG-20231112-WA0022.jpg
IMG-20231112-WA0024.jpg
IMG-20231112-WA0023.jpg
 
Habari hizo awambie hukohuko, sisi huku tunaona kama habari za Malawi na Congo.
Ni kweli. Sasa pilipili usoila yakuwashia nini? Kiherehere cha nini? Wakati mwingine unapaswa kutulia ili unyolewe. Mambo haya yana wenyewe, weye humo.
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ya awamu ya nane imeweka kipaumbele kikubwa katika sekta ya elimu kwa kuongeza bajeti, kuimarisha miundombinu kwa kujengwa shule zenye vifaa vya kisasa, pamoja na kuajiri walimu wa masomo ya sayansi ili kuongeza kiwango cha ufaulu wa wanafunzi.

Rais Dk. Mwinyi amesema hayo katika hafla fupi ya chakula cha mchana na kuwapongeza wanafunzi waliopata ufaulu wa daraja la kwanza kwa kidato cha nne mwaka 2022 na kidato cha sita mwaka huu aliyowaandalia viwanja vya Ikulu Zanzibar tarehe 12 Novemba 2023.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi ameeleza kuwa Serikali itahakikisha inaongeza fedha ili kila mwanafunzi mwenye nafasi ya kuendelea na masomo ngazi ya elimu ya juu anapatiwa mkopo.

Vilevile Rais Dk. Mwinyi ametoa zawadi ya laptop moja kwa kila mwanafunzi aliyefaulu kiwango cha daraja la kwanza wa kidato na nne na sita kwa skuli za Unguja na Pemba jumla 1,450.View attachment 2811817View attachment 2811818View attachment 2811819View attachment 2811821View attachment 2811822View attachment 2811823View attachment 2811824View attachment 2811825
"Kama SSH asingekuwa mwanamke basi Makamo wangu angekuwa Hussein Mwinyi " Late Magufuri

Ila Zanzibar elimu bado sana kwahiyo hao hapo ndio wanafunzi wote wa Zanzibar waliopata div 1 form IV na vi?
 
Back
Top Bottom