Kimsingi Taifa lenye vijana wasomi ambao wanaichukia serikali yao kutokana na mapungufu ya serikali hiyo ndio Taifa hai zaidi kwasababu wao wanatarajiwa kuja na mbinu mbadala bora zaid ya ile ya Serikali. Kosa la elimu ya kiafrika ni lilelile, kutilia mkazo academic side na kupuuzia vocational training. Hata katika huu mkopo, sidhani kama wanafunzi hao wachache wanaosoma vocational training colleges wanapata. Tukiwa na vijana wengi wenye elimu ya academics inayoizidi ile ya ufundi itakuwa tunatengeneza taifa la walalamikaji na wapiga porojo tu ambao wanadhani kupitia wanasiasa wanaweza kutimiza mahitaji yao. This is very wrong. Ni sababu hii iliyoleta mapinduzi Libya, Egypt, na maeneo mengineyo yenye migogoro inayofanana na baada ya kufanya hivyo wanakuja kubaini kwamba waliowaingiza serikalini kumbe pia hawatatimza mahitaji yao. Kitakachoendelea kwa taifa hilo "total destabilization"