Serikali ya CCM inahofia nini ACT Wazalendo?

Ashasembeko

JF-Expert Member
Dec 14, 2017
225
910
Tarehe 14 Julai, siku moja baada ya picha za Bernard Membe kuwa na viongozi wakuu wa ACT Wazalendo kusambaa mitandaoni, msajili wa vyama vya siasa aliwaandiki barua viongozi wa chama kukusudia kukichulia hachua chama hiko kwa kile msajili anachokiita ukiukwaji wa sheria ya vyama vya siasa.

Kwenye barua hiyo Msajili amewahakikishia kuwachukulia hatua kali hivi karibuni ili "wawe fundisho kwa vyama vengine".

Kwa mwenendo wa hali ya kisiasa nchini katika UTAWALA (sio uongozi) wa Rais Magufuli, mambo kama haya hayashtui wala kidogo. Ni mwendelezo wa ukandamizaji wa demokrasia ya ushindani na fikra huru.

Uoga wa nini?
Hivi inaleta maana gani, mtu - na chama chako - umekua unafanya siasa peke yako kwa miaka mitano ila bado una hofu ya vyama vengine. Umevifanya vyombo vya habari vya serikali (vinavyolipiwa kodi na kila mtanzania) kama TBC, Daily News na Habari Leo kuwa vyombo vya kukusifu wewe binafsi na chama chako. Ukaona haitoshi ukaingilia uhuru wa vyombo huru, kuvitisha na kuvifungia vengine. Nina rafiki ambae ni mhariri katika moja ya magazeti maarufu hapa nchini alinisimulia jinsi yule Dr. Abbas anavyowapigiaga simu kuwatisha wakipublish habari za vyama vya upinzani au zile zinazokosoa serikali.

Vyombo vyote vya dola vipo mkononi mwako. Polisi wanafanya kazi kwa matamko yako na si kwa maadli. Takwimu umeminya, enzi hizo za Kikwete na Mkapa muda kama huu tungeshaona baadhi ya taasisi zikibashiri nani atashinda au kushindwa ila sasa hizi hamna atakaedhubutu kufanya hivo. Kwenye tume ya uchaguzi, Director of elections ni kada wa CCM na inajulikana, ukaona haitoshi ukaamua kupeleka maafisa wa usalama wa taifa kwenye tume. Ukamtuma mkurugenzi wa tume abadilishe guidelines za uchaguzi kufanya iwe HIARI kuwaalika wasimamizi wa kimataifa wa uchaguzi yaaani international election observers.

Mipango yote hii ila bado kuna uoga, kitu ambacho nashindwa kuelewa. Yaaani una vifaa vyote vya ushindi ila bado unaogopa? Ninaamini kuna kitu tusichojua. Either, Ni chuki binafsi ya vyama vya upinzani na fikra huru au ana taarifa kuwa ni kweli hapendwi na inabidi atumie nguvu zote alizonazo ili kupata ushindi.

Nini kitatokea ACT kikifutwa au kuzuiwa kufanya uchaguzi?
Kwanza tunafahamu kuwa ACT ndio nguzo kuu ya upinzani Zanzibar kwa sasa. Tunajua Wazanzibari walivyo, wao hawataki mchezo na siasa zao, ukimnyima Maalim fursa ya kugombea, unataka kuvuruga uchaguzi Zanzibar.

Hiyo ni kwa Zanzibar tu, ila tukihuisha taifa kwa ujumla, utaona jinisi kukifuta ACT kutakavyoleta unnecessary distraction ya uchaguzi. Kwanza vyombo vikubwa vya habari vya kimataifa kitarepoti hili tukio (najua hawajali hili), ila watakachojali ni jinsi wadau wa maendeleo wakakavyotoa matamko na kusimamisha misaada.

Tunajua nchi nyingi duniani ikiwemo Tanzania, zipo katika hali mbaya ya uchumi kwa sababu ya janga la corona, sidhani kama Magufuli atataka aanze awamu mpya bila kupewa ushirikiano na wadau wa maendeleo, kama ilivotokea uchaguzi wa marudio wa Zanzibar 2016, amabapo wadau karibu wote wa maendeleo walimsusia Shein, ikiwmo marekani kufuta msaada wa billion moja nchini.

Kingine, na hii najua Mkuu ndicho anachotaka, kutakua na voter apathy. Hapa namaanisha, watu hawataona haja ya kwenda kupiga kura maana tayari watakua wanamjua mshindi. Hii ni mbaya, maana itaonyesha kabisa demokrasia ya nchi IMEKUFA! Pia unajenga chuki kwa wananchi. Siku zote hata ufanye mazuri yapi, binadamu hapendi kuona mtu anaonewa. Ndio maana unaona Afrika Kusini walidahi uhuru wao hata kama wazungu walijenga vitu.

Ni hayo tu!!
 
Hofu sio ACT WALA ZITTO.. Hofu ni Membe kwakuwa huyu ana wafuasi ndani ya CCM. Na hofu nyingine ni kama ataunganisha nguvu ma Lissu
Sawa sawa mkuu, mkutano wa jana wa ACT uliwapa pressure kubwa. Lakini hofu nyengine pia ni Maalim Seif Zanzibar washaona kumewakalia vibaya!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom