Serikali ya CCM ijiuzulu sasa hivi!

Rubabi

Senior Member
Nov 30, 2006
170
13
Hakuna hata mmoja asiye mwizi,viongozi wote ni wafanyabiashara kikwete yupo kimya.Pesa za serikali zinaibiwa mchanamchana.Mikataba ya carl peters inasainiwa kila siku! Nchi yetu imebaki kuwa na mashimo tu!Maziwa yetu samaki wameisha tumebaki kula mapanki !Mikataba mibovu inatufunga sisi watoto wetu mpaka wajukuu kwa miaka mpaka hamsini.

Tumekuwa wapole mno,Je mpaka lini tutawavumilia hawa?
 
Lissu Tundu ametwambia tuwakate vichwa kama wale wafalme wa Uingeleza, nafikiri 2010 siyo mbali endapo upinzani utafanya kweli sisi tuko nyuma tutawaka vichwa hao ccm bila kujali sijui JK,EL wala kingunge wote mafisadi tu shenzi type
 
Huruma hawana, last time i checked hawakuwa na mpango wa kuwa nayo...... the oppressed lazima waache tabia ya do nothingism, kama kweli watu wamechoka basi defeat this bastards kwenye next election cycle.FULL STOP!!
 
Wakuu leo nilikuwa ninafuatilia news zote za bongo, ukweli ni kwamba serikali yetu inahitaji a miracle kujisafisha na hizi tuhuma za ubadhirifu, maana nimesikia makanisa, mabalozi wa kutoka nje, World Bank, mapaka mama mmoja ambaye ni mwenyekiti wa Bank ya Afrika, wote wakiwakoromea serikali kuwa waje clean na tuhuma za ubadhirifu, na hasa za BOT,

kwa hiyo tunasubiri kwa makini sana, maana hao wanaofanya uchunguzi BOT wameihimizwa na World Bank, kummaliza mara moja huo uchunguzi, I mean this time somebody is going down na tunasubiri ukweli, ambao ninaamini kuwa hauko mbali!

EU wameshaanza mikwara kuwa bila ya ukweli kupatikana misaada iko mashakani, kwa hiyo subira this time haitavuta shari, bali heri!
 
Hawatajihuzuru hata siku moja.
Sisi tunaoliwa ndo tunatakiwa kuchukua hatua za kuingia kwenye uongozi wa kisiasa ili kuinusuru nchi yetu.
Tugombee nafasi zote kuanzia Udiwani mpaka Ubunge.
Kelele tu haziwezi kuwaondoa SISIEMU asilani
 
CCM haiwezi kujiuzulu hata siku moja,kama hata Katibu Mkuu wake anadiriki kusema tuhuma hizi ni porojo na kuamua kuwatumia "watu Mbumbumbu" kama Tambwe kutoa majibu ya kipumbavu ujue hawajui hata nini kinaendelea.Wako kwenye usingizi wa pono.Sijui,lakini nadhani wao ni kuondolewa tuu, eitha kwa kura au kama watapora kura basi itakuwa hakuna jinsi zaidi ya kutumia nguvu(Mungu aepushie mbali)maana WaTZ hawawezi kuwa kondoo wa kafara MIAKA YOTE.Bahati nzuri ni kuwa vuguvugu hili limeanza mapema sana kabla ya uchaguzi na sio kama zile kampeni walizofanya wapinzani miaka ya nyuma kwa style ya zima moto,wananchi sasa wananafasi nzuri ya kuujua ukweli na kutafakari nini hatima ya maisha yao na vizazi vijavyo ndani ya CCM. Maana hata kama CCM watatumia mtindo wa kugawa kanga na kofia, duu! kwa miaka mitatu kabla ya 2010 itakuwa shughuli kweli. Tujitahidi ujumbe ufike kwa wananchi wale walionyimwa elimu ya uraia watuelewe maana hao NDIO MTAJI MKUBWA WA CCM,wanawatumia vizuri maana wanaelewa kuwa 'kura moja mtu mmoja' na haijalishi kuwa aliyepiga anafahamu umuhimu wa kura yake
 
WE NEED NEW LEADERS WITH VISION,NOT RE-CYCLED LEADERS WENYE ARI MPYA NGUVU MPYA NA KASI MPYA ISIYO NA MUELEKEO.
 
WE NEED NEW LEADERS WITH VISION,NOT RE-CYCLED LEADERS WENYE ARI MPYA NGUVU MPYA NA KASI MPYA ISIYO NA MUELEKEO.

Mkuu heshima mbele, maana lako nili ni another million dollars question, je tunao viongozi wa namna hiyo hapa bongo wenye vision na muelekeo?

Mtandao walitumabia hivyo hivyo, lakini angalia tulipo sasa! Maana kuvumbua maovu ya serikali iliyopo kwenye power ni one thing, na viongozi wenye vision ya kuongoza ni absolutely another story, tusije tukachanganya mambo!
 
Hawatajihuzuru hata siku moja.
Sisi tunaoliwa ndo tunatakiwa kuchukua hatua za kuingia kwenye uongozi wa kisiasa ili kuinusuru nchi yetu.
Tugombee nafasi zote kuanzia Udiwani mpaka Ubunge.
Kelele tu haziwezi kuwaondoa SISIEMU asilani

kweli kabisa. lets take an active role in leading our country. Kwa trend iliyopo we need new blood katika uongozi and one of the best ways is for you and me to take interest and part in leadership. LETS DO IT GUYS!
 
Hakuna hata mmoja asiye mwizi,viongozi wote ni wafanyabiashara kikwete yupo kimya.Pesa za serikali zinaibiwa mchanamchana.Mikataba ya carl peters inasainiwa kila siku! Nchi yetu imebaki kuwa na mashimo tu!Maziwa yetu samaki wameisha tumebaki kula mapanki !Mikataba mibovu inatufunga sisi watoto wetu mpaka wajukuu kwa miaka mpaka hamsini.

Tumekuwa wapole mno,Je mpaka lini tutawavumilia hawa?

That easy? I dont think so....
 
sasa wazee mnajua 2010 sio mbali,mikakati ya kuchukua viti zaidi vya ubunge ianze mara moja maana haya mafisadi bila watu kujitoa mhanga yatapigana mpaka last breath...sasa ni vitendo na mkumbuke ushindi haupatikani kwa siku moja so maandalizi ni muhimu sana kuanzia sasa hivi,nitasupport wale wote wenye vision ya kueleweka na ambao hawatoki CCM...lazima tuwachape hawa mafisadi kwa kishindo cha nguvu sana mpaka wakose mlango wa kutokea.
 
Tuna Kura 2000-3000 za JF tayar, sasa zingeni tunapata je na kupitia chama gani cha Upinzani, maana viko vingi zikigawanjwa hazitashinda CCM, a more light please!
 
Field Marshal,
Mie sidhani kama CCM hakuna VIongozi wazuri.Tatizo ni kuwa CCM imeshakuwa genge la Mafia.Either your with them or not. So as long as kiongozi atatoka CCM atatimiza matakwa ya Mafia kwanza.Otherwise wanakukolimba
 
Mkuu Nyangumi,

I know, lakini leo nimejionea wananchi wa vijijini wakiwasakama mawaziri na mikatba ya madini, yaani wananchi wa kawaida sana kwa kweli ni good news, tukishakuwa na wananchi wanaoelewa, basi inatosha pole pole viongozi wataendelea kuzomewa,

Mwishowe tutaanza kuwa tena na maadili ya uongozi ambayo hatukuwa nayo kabisa in the last 15 years, viongozi wabovu wataondoka hivi umemuona Muungwana hivi karibuni alivyochoka mkuu!

Hatimaye tumeanza kuambiwa mpaka mambo ya migodi ya waziri, hatua kubwa sana mkuu!
 
CCM lazima iondoke,just imagine 46yera,but nothing has been done yet,zaidi ya kuitwa among of the poorest country in the world,nina hasira na viongozi hawa,enough is enough,something must be done to take back our nation from these Nyang'aus as soon as possible.
 
Kila siku napinga hili jambo, Serikali siyo ya CCM. Serikali ya wananchi wa Jamhuri ya muungano. CCM wamepewa mamlaka ya kuiongoza. Nimeshaongelea hili nadhani na Zitto huko mnakopita muwaeleze wananchi kuwa kuiondoa CCM kuongoza serikali haimaanishi umepindua serikali au umeiondoa serikali. Umeondoa sera na wasimalizi wa hizo sera. Kama wananchi hawataeleweshwa kuhusu ili basi uoga wa kuiondoa CCM kuongoza serikali hautaondoka.
 
Sam,
Naona umegusa swali muhimu: Serikali ya Tanzania ni ya CCM ama inaongozwa tu na CCM? Na CCM wenyewe wanachukulia kwamba serikali ni yao, au wanaiongoza tu?

Hapana shaka kwamba CCM ndiyo imeunda serikali. Matatizo tunayokabiliana nayo sasa ya uporaji wa mali ya uma, serikali kukataa kupata ridhaa ya bunge kabla ya kuingia mikataba na wawekezaji, kutokuweko na haki sawa mahakamani (eg Nyari and Ditto cases), kudidimia kwa hali ya maisha ya mwananchi wa kawaida, etc, ni matatizo ya serikali kuongozwa vibaya na CCM tu au hata serikali yenyewe ni mbaya?

Itatosha kubadilisha uongozi wa serikali na kuacha katiba kama ilivyo? Haitabidi kubadilisha katiba ya serikali? Kwa mfano, tukiacha mfumo uliopo sasa wa kuthibiti rushwa tutafanikiwa kweli kwenye kuithibiti?

Hatua ya kwanza itabidi iwe kuiweka CCM benchi (yaani CCM iwe chama cha upinzani). Likikamilika hilo (na ni gumu kweli maana watu wenyewe wanaiba hata kura, sio mali ya uma tu), itabidi viongozi wapya wabadilishe katiba ya serikali ili TUWE NA UTAWALA WA KISHERIA.

Mwishowe, itabidi wale wote wanaolindana ndani ya CCM katika kupora mali ya uma wafikishwe kwenye vyombo vya sheria. Ni tumaini langu kwamba vithibitisho vya uporaji wa mali ya uma unaofanywa sasa na viongozi wa CCM vinawekwa vizuri. It is my considered opinion that hawa miungu wadogo wataishia jela badaye.
Hata watu kama Nyari na Ditto watashughulikiwa upya baadaye.
 
Kila siku napinga hili jambo, Serikali siyo ya CCM. Serikali ya wananchi wa Jamhuri ya muungano. CCM wamepewa mamlaka ya kuiongoza. Nimeshaongelea hili nadhani na Zitto huko mnakopita muwaeleze wananchi kuwa kuiondoa CCM kuongoza serikali haimaanishi umepindua serikali au umeiondoa serikali. Umeondoa sera na wasimalizi wa hizo sera. Kama wananchi hawataeleweshwa kuhusu ili basi uoga wa kuiondoa CCM kuongoza serikali hautaondoka.

By their actions and inactions governments can induce prosperity or suffering. They can raise the pace of modernization or brake the the economy to the halt ( See waht is happening in Zimbabwe).
They can bring hope or despair. There is scarcely an aspect of economic life which does not lie within the ambit of the state. Consider, for example, the budget. Its tax proposals alter the living standard of the bulk of population. They alter the profitability of busness and attractiveness of saving and inversting etc. When 4th gvt came with their slogan of Hari mpya, nguvu mpya na kasi mpya" people received it with two hands and one heart but gvt did not take it as an opportunity.
 
Ndugu yangu Augustine Moshi!! vyombo vya dola na vya sheria, sijui mahakama, polisi, TAKUKURU you mention them.. havina meno zidi ya hao wasilikale. kuwapeleka huko ni sawa na kesi ya nyani uwapelekee tumbili jamani hakutakuwa na fair trial. Suala kubwa ni kuelimisha wananchi hasa wapiga kura, waihukumu sisiem 2010. Zile Tshirt na makapelo yasiwaghalimu maisha yao. Sisiem ni lazima iwekwe rehani tuweze pata viongozi mahiri watakao tufikisha kwenye karne ya 22. Kila sehemu ni kero tu, vyuoni, mahospitali, wafanyakazi, mifumuko ya bei kila kitu jamani ni machungu, huwa najiuliza hivi sisi watanzania tunalaana? ama tumelogwa hebu angalieni rasilimali tulizo nazo.... napata hasira
tofauti ya matajiri na masikini inakuwa kubwa mno....tunajenga jamii yenye watu matajiri sana kwa gharama za masikini....
 
Back
Top Bottom