Serikali, Wenye Hisa za NICOL ndio wameliwa au...?

Ikena

JF-Expert Member
Oct 24, 2007
553
393
Kila nikitaka kuuza hisa zangu naambiwa haziuziki, sasa ndo kusema nimeliwa au nivute subira?

Sasa kwanini wasiturudishie fedha zetu kabla hisa hazijazidi kushuka thamani zaidi? Hvi nitawezaje kupata fedha zangu iwapo kampuni hii itaingia mitini?

Naombeni mchango wenu wa mawazo.

========
UPPDATES:
========

Taarifa kwa vyombo vya habari kutoka mkutano wa NBAA, CMSA, BRELA na DSE kuhusiana na NICOL

Katika Mkutano uliofanyika tarehe 27 Octoba 2009 ukishirikisha Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Wakala wa Usajili na sheria za Biashara (BRELA), and Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) zikiwa ni taasisi zinazosimamia shughuli za kampuni chini ya sheria mbalimbali, mambo yafuatayo yalijitokeza.

I. Yaliyojitokeza
1. Kukiuka Kanuni za Kimataifa za Kihasibu (IFRS)
Baada ya NICOL kuwasilisha taarifa ya hesabu za fedha zilizokaguliwa kwa mwaka ulioishia tarehe 31 Desemba 2008, katika kupitia taarifa hizo, CMSA ilibaini kuwa utayarishaji wa taarifa hizo haukuzingatia kanuni za kimataifa za uandishi wa vitabu vya hesabu za fedha (uhasibu) yaani International Financial Reporting Standards (IFRS) na pia ilibainika kuwa hesabu hizo zinapotosha hali halisi ya kifedha ya Kampuni ya NICOL (financial position) na faida ambayo NICOL iliripoti. Mkutano huo ulithibitisha kuwa:

(a) CMSA na NBAA kwa pamoja walitoa maagizo kwa Wakaguzi wa hesabu wa Kampuni ya NICOL wamtake mteja wao, NICOL kuwa:-
(i) aondoe taarifa za hesabu za mwaka unaoishia tarehe 31 Desemba 2008 kwa kuuarifu Umma (press release)
(ii) atayarishe upya taarifa hizo kwa kufuatana na kanuni za kimataifa za kihasibu na kuziwasilisha kwa ukaguzi kulingana na Kanuni za kimataifa za Ukaguzi wa hesabu yaani International Standards on Auditing (ISAs)..

Sababu kubwa ya kuitaka NICOL iondoe taarifa za hesabu zake ni kuwa taarifa hizi za hesabu za fedha zilikuwa hazitoi ukweli kuhusu hali halisi ya kifedha ya kampuni na hivyo kupotosha Umma.

(b) Wakaguzi wa Hesabu wa NICOL walikiri kufanya makosa kwa kutoa hati safi (unqualified audit opinion) kuhusiana na taarifa hizo za hesabu za kampuni ya NICOL na Kumtaka mteja wao atayarishe upya hesabu hizo kufuatana na kanuni za kimataifa za Kihasibu na kuziwasilisha kwao kwa ukaguzi kabla ya kuzitoa kwa Umma.

(c) Endapo taarifa za hesabu za Kampuni ya NICOL zingetayarishwa kuendana na kanuni za kimataifa za uandishi wa vitabu vya hesabu za fedha hali ya kifedha ya NICOL na faida iliyoripotiwa ingekuwa tofauti kabisa na ripoti yao potofu inavyosema.

2. Kuitisha Mkutano Mkuu wa Wanahisa Kinyume na Matakwa ya Sheria ya Makampuni
Katika kulinda maslahi ya Wanahisa wa NICOL, CMSA na DSE waliiagiza Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya NICOL wasifanye mkutano wa Mwaka wa Wanahisa (AGM) bila kuwa na Taarifa za Hesabu sahihi na zinayokubalika kwa mwaka unaoishia tarehe 31 Desemba 2008 kama Sheria ya Kampuni ya mwaka 2002 inavyoelekeza. Kwa mujibu wa sheria ya Makampuni, uwasilishaji wa taarifa za fedha zilizokaguliwa ni moja ya kipengele cha lazima katika ajenda za Mkutano wa Mwaka wa Wanahisa.

3. Kukaidi Kutekeleza Maagizo na Kutoa Taarifa Potofu kwa Wanahisa
(a) Wakurugenzi wa kampuni ya NICOL pamoja na kutakiwa na Mamlaka tatu za usimamizi, NBAA, CMSA and DSE walikaidi agizo la kutayarisha upya taarifa za fedha za Kampuni kwa Mwaka Ulioishia tarehe 31 Desemba 2008.

(b) Pamoja na kukumbushwa mara kadhaa na kushauriwa na Wakaguzi wa Kampuni, Wakurugenzi wa NICOL walikaidi agizo la kuondoa taarifa hizo za hesabu. Kibaya zaidi Wakurugenzi wa NICOL waliweka kwenye ripoti ya Mwaka Maoni ya Wakaguzi (audit opinion) huku wakijua kwamba tayari wakaguzi hao walishaondoa maoni yao.

(c) Wakurugenzi wa NICOL waliendelea kuitisha mkutano tarehe 24 Octoba 2009 na wakagawa kwa Wanahisa pamoja na nakala nyinginezo, Ripoti ya Mwaka ambayo ina mahesabu ambayo Mamlaka za usimamizi ziliagiza ziondolewe kwa sababu zilikuwa zikitoa taarifa potofu kwa Wanahisa.

(d) Wakurugenzi wa NICOL wamekaidi kurekebisha taarifa zao kama Mamlaka za Usimamizi zilivyoelekeza. Wakurugenzi wa NICOL walitakiwa kutekeleza kwanza maagizo waliyopewa kabla ya kuitisha Mkutano Mkuu wa Wanahisa ili wasiwape wanahisa taarifa potofu.

4. Wakaguzi Kuondoa Maoni yao Kuhusiana na Mahesabu na Hatima yake
Kutokana na kukosekana ushirikiano kutoka kwa Wakurugenzi wa NICOL, Wakaguzi wa Hesabu kupitia barua yao nambari MACO/NICO/10/09 ya tarehe 8 Octoba 2009 waliondoa maoni yao (audit opinion) juu ya taarifa hizo za hesabu za Fedha za NICOL kwa mwaka ulioishia tarehe 31 Desemba 2008 na kumtaka mteja wao arudishe kwao nakala zote zilizosainiwa za mahesabu hayo. Kuondolewa kwa Maoni kuhusiana na hesabu maana yake ni kuwa NICOL haina taarifa za hesabu za fedha zilizokaguliwa kwa mwaka ulioishia tarehe 31 Desemba 2008.

5. Kampuni ya NICOL Kufanya Maamuzi ya Uwekezaji Bila Kufanya Uchunguzi Yakinifu
Baada ya zoezi la ukaguzi lililofanywa na CMSA (onsite inspection), ilithibitika pia kuwa, Wakurugenzi wa Kampuni ya NICOL wamefanya maamuzi mbalimbali ya Uwekezaji bila ya kufanya uchunguzi yakinifu (Due Diligence) na hivyo kuwa na uwekezaji wenye ubora hafifu kama ilivyowekeza kwenye makampuni ya Interchem Pharmaceutical and Beverage Limited (IPBL) na Twiga Feeds Ltd na hivyo kuhatarisha maslahi ya wanahisa. Wakurugenzi wa NICOL waliagizwa waajiri Mtaalamu wa Mambo ya Uwekezaji (Fund Manager) ili awashauri katika kufanya maamuzi ya uwekezaji. Mpaka sasa hawajatekeleza agizo hilo pamoja na kukumbushwa mara kadhaa.

II. Maoni na Mapendekezo ya Mamlaka Zinazosimamia Kampuni kwa Mkutano wa Wanahisa Uliopangwa Kufanyika Tarehe 31 Octoba 2009
Kufutia maelezo hayo hapo juu, ni wazi kuwa Wakurugenzi wa kampuni ya NICOL wamekuwa wakaidi na wameshindwa kutimiza wajibu wao. Wanahisa wana haki katika Mkutano Mkuu kuteua Wakurugenzi na inapoonekana muhimu kuwaondoa. Mamlaka zinazosimamia shughuli za kampuni tuna maoni na mapendekezo yafuatayo kwa Mkutano wa Wanahisa uliopangwa kufanyika tarehe 31 Octoba 2009.

Wakurugenzi wa kampuni kwa kipindi kinachoishia tarehe 24 Octoba 2009 hawana sifa ya kuendelea kuwa wakurugenzi na hivyo wajiuzulu au waondolewe. pia hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni ya mwaka 2002.
Bodi mpya iahidi kwamba itatekeleza maagizo yote yaliyotolewa na Mamlaka za Usimamizi.

III. Kushindwa kwa Wanahisa Kutekeleza Mapendekezo ya Mamlaka za Usimamizi
Wanahisa wanatakiwa watambue kwamba wakishindwa kutekeleza kwa ukamilifu mapendekezo ya Mamlaka za Usimamizi itapelekea Mamlaka hizo Kuchukua hatua kali dhidi ya Kampuni kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zilizopo.

More updates:
 
Ikena

Mkuu naona umeingia wasiwasi, sifahamu vizuri perfomance ya hisa za NICOL lakini sijapata tetesi ya kuteleleka kwake kwenye soko! Hivyo kama umejaribu kudispose hisa ulizonazo na hupati mteja, inaweza kuwa na sababu nyingi tu not necessary ikawa thamani yake imeshuka, kwa mfano inaweza kuwa watu wanaisikilizia hii Financial crisis kama itakuwa na madhara kny makampuni na ya hapa kwetu, so wako reluctant kuachia cash au broker unayemtumia si mzuri kumake deals pale DSE au zipo hisa chache sana zinazouzwa sasa (pengine za kwako tu) na watu wanataka nyingi kwa mkupuo mmoja etc

Nakushauri mtumie broker mzuri kwa ushauri na kuuza hisa zako hope utafanikiwa!
 
Last edited by a moderator:


Mkuu sidhani kama crisis hii ipo kwenye nico pekee, ukiangalia masoko mengine ya hisa yanakwenda vizuri.
Hapo DSE ndio hawazipokei kabisa, na wanadai tangu mwezi wa 8 hazinunuliki kabisa, na thamani inazidi kushuka.

Sasa ndio ndio nauliza tutakuwa tumeliwa @ the end of the day ama vp?
 

Ikena,

Ndo maana nikasema itabidi uwaone watalaam wa stock exchange kama kina Orbit, Solomon etc wako wengi sana, watakupa ushauri wamaana zaidi!

Ila kama umeona thamani ya hisa za NICOL pale DSE zinashuka is true kwamba thamani ya uwekezaji wako inapungua as well, yaani unapata hasara...lakini haya mambo huwa yanatokea itabidi uvute subira zianze kupanda tena ili uweze kuziuza kwa faida, ukiuza sasa (kama utafanikiwa) utapata hasara!

Angalia kama hawa jamaa wa TOL, hisa zao zilikuwa down kama kwa miaka mitatu hivi consecutively, lakini baadaye zilianza kuwa stable tena!

Hiyo ndo business mkuu...ups and downs huwa zipo!
 

Kuuza hisa mpaka upate mtu wa kumwuzia, kwa DSM nadhani wanunua hisa sio wengi sana labda ndo maana unapata shida kuziuza, pia labda wanunuzi wanaamini bei yake ni kubwa kuliko inavyotakiwa kuwa.

Sijui ni nani unataka akurudishie hela, kampuni hailazimiki kununua hisa zake kama mtu anataka kuziuza, labda waamue wenyewe.

Kushuka kwa thamani ya hisa na hata kampuni kufilisika ni moja ya risk za kununua hisa. Kampuni ikifilisika ndo umekula hasara kabisa, kwa sababu shareholders wanakua wa mwisho kufikiriwa kwenye kugawa mali za kampuni.

Note: Sijui anything specific kuhusu NICOL!!
 
Hata mimi ukiniambia ninue share za NICOL kwa sasa nitasita-- afadhali ninunue za Viwanda vya Cementi au Bia.. maanke watu wanakunywa bia na kujenga kila siku
 
Ikena kwa kweli Hisa za nikola kwa sasa hivi huwezi kuuza hata ukimtumia broker wa namna gani watu kila siku wanalalamika ziko kwenye Q tangu october hazijanunuliwa na wahusika hawajatangaza gawio na bei yake imeshuka sana sasa hivi ni sh,285/= kuhusu swala la wewe kupata hasara sijui labda usubiri kupata gawio lakini swala la kuuza sahau.

Mimi nafanya kazi huko hisa za tol, nicol, dcb sasa hivi hazina soko kabisa na nmb zinashuka kabisa japo wametangaza gawio la sh, 30 ni kwa wale wenye hisa nyingi ndo watapata faida wale wenye hisa kidogo bora wauze tu kwa bei iliyopo ya 900 maana zimeover supply na bei itazidi kushuka.
 
Dada Joyceline vipi kuhusu hisa za TWIGA hali ikoje? Nina vi hisa vyangu huko na kwa sasa niko nje ya nchi.
 
Samahani, naomba niulize hivi NICOl imeorodheshwa katika soko la hisa au bado ni over the counter kama CRDB?

Maana kama ni OTC basi hawawezi ku-deal nazo madalali wa hisa, inabidi mkuu usubiri mpaka ikiorodheshwa katika soko la hisa ndo uweze kununua na kuuza.

Kama imeorodheshwa basi ni lazima wanahisa mpewe taarifa.

lakini kama una mashaka yoyote kawaone CMSA - wako PPF wakupe information zaidi.
Asante
 
Susuviri

Wao walijiadvertz kuwa wanampango wa kujiunga DSE baada ya kuchukua machinjio ya Dodoma, sina uhakika kwasasa kama washajiunga.
 
Last edited by a moderator:


Sidhani kama bei ni kubwa, nimegundua kampuni haina mvuto na niliuvaa mkenge
 
Sidhani kama bei ni kubwa, nimegundua kampuni haina mvuto na niliuvaa mkenge

Pole Ikena, ndiyo bongo land ilivyo.
Waambie wazee wa uzawa (Mengi, Idd Simba, Felix na wenzao wengine) wakupe jibu.

Tanzania ni kulizwa kwa kwenda mbele. Ukigeuka kulia unalizwa na wazee wa uzawa ukigeuka kushoto unalizwa na wazee wa vijisenti na richmonduli, ukiangalia makaratasi unalizwa na waandishi ukiangalia juu unalizwa na mzee wa mahujaji (Mattaka na Atcl yake). Hiyo ndiyo Tanzania bwana kula uliwe.
 
R mashuri hisa za kununua kwa sasa ambazo huwezi kupata hasara ni TBL, TTC, TWIGA CEMENT, TANGA CEMENT TATEPA NA EAST AFRICA BREWERIES
 
R mashauri: Twiga kwa sasa ni sh. 1600 mpaka leo sasa sijui mpaka hiyo siku utakayouza kutakuwa na badiliko lolote
 
Sidhani kama bei ni kubwa, nimegundua kampuni haina mvuto na niliuvaa mkenge

Namaanisha bei ni kubwa ukifananisha na kiasi ambacho watu wako teyari kulipa, nina uhakika ukiamua kuuza at a big loss kuna mtu atanunua. Yaani hakuna uwiano kati ya supply na demand.

Labda jaribu kuangalia long term, kama unaamini campuni itafanya vizuri baadae basi kaa nazo, otherwise uza for a loss.
 
Biashara ya hisa siku zote ni mchezo wa wakubwa, yaani watu wenye mipesa mingi. Kwa watu wadogo wadogo, ujanja huwa ni kwenye Initial Public Offer (au IPO). Unanunua halafu zikianza kuuzwa immediately unauza usisubiri. Ukisubiri dividend mara nyingi huwa ni amount ndogo sana.

Taratibu na sheria za masoko au uendeshaji wa biashara unatoa nafasi ndogo sana kwa wamiliki. Wameliki wenye mkono katika uendeshaji ndo wanafaidika. Wamiliki wadogo wadogo kama wewe mnakuwa watu wa mwisho kufikiriwa. Kwa mfano kampuni likitengeneza faida, makolokolo yooote hukatwa, kiwango kinachobaki ndo hulipwa kama gawio kwa wenye hisa. Waendeshaji hawalazimiki kulipa gawaio na mara nyingi huwa wanazua visa kibao kama uwekezaji, n.k. ili kuacha kulipa gawio. Gawio hata likilipwa inakuwa kigogo mno kiasi cha kuleta tofauti yoyote kwa mwenye hisa chache. Kampuni ikifirisika wenye hisa ni watu wa mwisho kufikiriwa na mara nyingi hawaambulii chochote na sheria na taratibu zinaruhusu hilo.

Maana yake ni kuwa kujiingiza kwenye soko la hisa inabidi uwe na fedha za kutosha kukuwezesha kuingilia utendaji wa kampuni. Vinginevyo ni sawa na kucheza chekundu na cheusi. Outcome mara zote huamliwa na mchezeshaji anaweza kuruhusu ule, au uliwe tuu. Waendeshaji wa makampuni (wenye shea nyingi) huwa wanaamua watoe gawio au wasitoe. Wao wanazo jinsi nyingi za kupata fedha yao kupitia michakato mbali mbali ya uendeshaji wa makampuni.

Kwa hiyo kabla ya kununua hisa kitu cha kwanza unachotakiwa kujiridhisha nacho, ni uendeshaji wa kampuni. Hiza kama za NICOL kwa kweli ilikuwa ni kama mchezo wa karata tatu. Hivi ulikuwa unajua NICOL inafanya biashara gani in the first place? Ulikuwa na uhakika wa jinsi inavyoendeshwa? Sasa hivi rekodi yao ya utoaji wa gawio ndo itakayofanya share zako zinunuliwe au zisipate mnunuzi. Ikiwa kampuni haieleweki eleweki, hakuna atakayekuwa tayari kununua share hizo kwa sababu hiyo hali ya kutoeleweka eleweka inaongeza kitu ambacho kinaitwa RISK.

Wanaojua biashara za hisa hawawezi kununua hisa zenye RISK KUBWA ikiwa hazina mapato makubwa!! Hiyo ndo kanuni ya masoko ya hisa.

Hisa zako zisiponunuliwa mwambie dalali wako ashushe bei. ikiendelea kushuka itafikia kiwango ambacho wale wenye hisa nyingi au wanaoendesha kampuni wataamua kuzinunua za kwako kwani kuendelea kushuka kwa bei za hisa kunashusha thamani ya kampuni.
 
Kipimapembe, u have some valid points ila kumbuka mkuu, watu waliokuwa wana-back NICOL walikuwa ni watu wazito sana kama vile Felix Mosha nadhani hata Mengi yumo, sasa wananchi lazima watawaamini.
Kwanza unafahamu kuwa neno risk kwa maana yake halisi halipo katika vocabulary ya Kiswahili, sasa utamweleza vipi mwananchi wa kawaida kuwa share fulani ina risk?
 
Hilo ni kweli kuwa RISK watu wengi hawaelewi ni kitu gani. Lakini ndo hivyo kwenye masoko ya mitaji RISK MARA nyingi haiwezi kuhesabiwa with absolute certainity. Hata marekani watu bado wanaliwa kwenye hisa. Fikiria kina Madoff!!! Kwetu sisi hii ndo nafasi ya watu kujifunza. Lakini ukikumbuka TOL imewala sana watu na share zake. Watu hawakujifunza kwa TOL??

Wanunuzi wadogo wadogo kwenye hiki kinachoitwa masoko ya mitaji siku zote ni kama dagaa. Samaki woote wakila wakashiba dagaa hubaki. Kinachowafanya waendelee kuwepo ni wingi wao tuuu. Lakini ukweli halisi hawafaidiki na chochote.

Vivyo hivyo kwenye soko la mitaji. Tena kwa nchi maskini kama yetu ambayo hata serikali ni rahisi kununuliwa, you can't trust soko la mitaji. Watu inatakiwa wajue kuwa hakuna fedha ya dezo. Hakuna mtu atakayefanya kazi halafu mwisho wa mwaka akulipe kitita.

Ni afadhali tuzame katika SME kuliko kuwaingiza watanzania kwenye hili gubeli linaloitwa soko la mitaji. Ukiwa na vimilioni vyako vitano, sita, au ishirini ni afadhali ufungue kibiashara chako na ukisimamie. Ukiwekeza kwenye soko la mitaji ni sawa na kuipoteza kwani hiyo ni kuwapa gawio wenye mipesa mingi.

Watu wakishaliwa sana, hatimaye watajua. Of course ujinga huwa ni kitu muhimu katika masoko ya mitaji, huwa wakati mwingine share zinapanda bei sana hata kama hakuna cha maana. Hapo ndo wajanja wanakulaga bingo, halafu wengi wanazamishwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…