Serikali, Wenye Hisa za NICOL ndio wameliwa au...?

Serikali, Wenye Hisa za NICOL ndio wameliwa au...?

Bulesi ndugu yangu pamoja na wewe kuwa na an entrpreneurial spirit nisingetaka kukuvunja moyo, lakini the writing is on the wall. Biashara wanayofanya NICOL ni karibu sawa na kile alichokuwa akifanya Madoff kule Marekani, lakini at a lower scale.

Kwanza kabisa biashara kufanywa na wanasiasa ni mwiko nambo moja-they have no entrepreneurial potential pamoja na kuwa na uwezo wa uhamasishaji.

Pili,kwa yule aliyewekeza katika NICOL hana say yoyote wapi pa kuwekeza, mahali penye high return, na ndio maana tunaona kampuni za Interchem(mali za hoa wahamasishaji).

Tatu, there is a conflict of interest katika kuwekeza katika kampuni ambayo ni mali ya mmoja wa wahamasishaji
Nne kutotoa mwenendo wa thamani ya hisa za wawekezaji ni KOSA kubwa sana, kwa sababu hisa zinapanda na kushuka within the hour not months and years.

Kimsingi kuwekeza ni sawa na duka, lazima kuweka duka lako penye wateja wengi, kubadili wauzaji duka (wale wtendaji) bado kunaweza kutobadilisha uchanganyaji wa duka hilo kama haliko sehemu ya wateja wengi.
 
Last edited by a moderator:
Mtu wangu mbona hiki kitu NICOL ikotaka fanana na DECI !! To the investors count yourselves as "Choka Mbaya" your money has gone down the drain and the drain itself is nothing else but Interchem Pharmaceuticals in Moshi which was owned by Ben Mengi.
 
Lole Gwakisa

Mkuu, sawa uwekezaji ni sawa na duka; unaweza ukaweka duka sehemu ya wateja wengi lakini kama wauzaji wako wanaulimi wa pilipili[ hawajui customer care] pia unaweza kufulia!

Pia unaweza kuwa na duka lenye wauzaji wazuri ukapata wateja wengi kwahiyo watendaji ni muhimu sana. Hawa wazee wa Nicol inabidi wakubali kuwa kazi ya uendeshaji wawaachie professionals ili wawekeze kama walivyowekeza NBC na sio kwenye kampuni kama ile ya Mengi mndogo!!
 
Last edited by a moderator:
Hii kampuni ovyo kabisa.

Walisema watawekeza katika kilimo, viwanda, mawasiliano, madini na mahoteli na kuwa hizi "sectors" zitakuwa ndio principal business activities! lakini hadi leo hamna kitu.

Nimejaribu kuingia katika link ifuatayo ya watu wanaoitwa "Credit Risk Monitor" ambao wana makazi pale New York nchini Marekani.

Unaweza kulipa fwedha kidogo na kupata taarifa zinazohusu kampuni hii.

http://www.crmz.com/Report/ReportPreview.asp?BusinessId=11896173
 
Lole Gwakisa

ndugu yangu ungeuliza uwelezwe niko ni nini sio kusema niko haina mradi yeyote kwa hiyo haifai

kwa kifupi NICOL ni equity fund, wananunua shares za makampuni mbalimbali na pia wanawekeza kwenye kampuni mbalimbali ambayo hayako listed kwenye stock exchange.

siyo hayo makampuni mawili tu bali wamewekeza hata NMB, wanamiliki 6.6% ya NMB click hapa

hata hivyo hii habari ni ya zamani na ishajadiliwa humu
 
ndugu yangu ungeuliza uwelezwe niko ni nini sio kusema niko haina mradi yeyote kwa hiyo haifai

kwa kifupi NICOL ni equity fund, wananunua shares za makampuni mbalimbali na pia wanawekeza kwenye kampuni mbalimbali ambayo hayako listed kwenye stock exchange.

siyo hayo makampuni mawili tu bali wamewekeza hata NMB, wanamiliki 6.6% ya NMB click hapa

hata hivyo hii habari ni ya zamani na ishajadiliwa humu
Sawa mkuu, kwa vile habari inajirudia maana yake kuna jambo.

Hivi nieleze kunagaubaga share ya NICOL inapanda au inashuka? Na je wamelipa dividends kwa wanahisa?
 
WANA JF MNA MAONI GANI JUU YA UFISADI ULIOFANYWA NA WAKURUGENZI WA NICOL?

Wana JF ilikuwa sahihi kwa wananchi kununua share za kampuni ambayo ilikua hewa ya makaratasi tuu kwa vipande vya hisa? Au watanzania wana pesa nyingi za kutapeliwa kila kukicha eg DECI NICOL JACKPOT BINGO DOLLAR JET LOTTO KITITA etc wakati huo huo kuna wananchi wanaishi maisha ya dhiki.

NAFIKIRI KILA MMOJA WETU BADALA YA KUCHEZEA FEDHA AANGALIE NDUGU, JIRANI, MASIKINI, YATIMA, VILEMA, WATOTO WANAOMZUNGU WENYE MATATIZO ASAIDIE KABLA YA KUFANYA UWEKEZAJI HEWA!

Sasa pesa zetu zimenunua makampuni mufilisi ya ndugu zao wakurugenzi wa NICOL!
 
haya ni yaleyale ya Wahanga wa makosa ya Ufisadi Tanzania, Hawa ni kina Rostam na Lowassa, na michezo yao ya visasi.
HATUDANGANYIKI.
 
BONGOLALA

Uendeshaji wa hii kampuni ulinitia mashaka siku nyingi sana.

Hii ni kuzidi kujidhalilisha kwamba WaTz peke yetu hatuwezi kuendesha mashirika au makampuni yetu wenyewe kwa ufanisi, uwazi na uwajibikaji!!!!

Pata Habari zaidi kwa kufungua hito attachment.

Source ni: http://www.cmsa-tz.org/news/market.php
 

Attachments

Last edited by a moderator:
Alipotujilisha Rostam miezi kadha ilopita kuhusu Ufisadi Nicol wengi humu walikataa eti haiwezekani haya kataeni ripoti ya tume ya soko la mitaji.
 
Wakuu

Haya ni mambo ya kitaaluma kidogo na ndio maana NICOL wanapata kiburi ya kuitisha AGM ilhali NBAA, CMSA and DSE wamewashauri kuziondoa reports zao. Na wamepata kiburi cha kuwakatalia Mangeso kuondoa account zao maana NICOL ndo wanandaa accounts na Mangesho kazi yake nikutoa Independent Opinion tu. Kama awali walisema ziko poa iweje wabadilishe? Je standards zilibadilika karibuni? Je Tanzania imeanza kufata IFRS leo? Kunamambo mengi ya Kujiuliza katika hizi nenda rudi.

Issue iko kwenye presentation ya Financial statement zao kwa kuzingatia tafsiri sahihi ya IFRS ( International Financial Reporting Standards). Kutofautinana kwenye presenation haiwezi kutafsiriwa kama ufisadi labda maamuzi ya uwekezaji wenye utata ndio inahitaji zaidi kufuatiliwa. Jambo ambalo limewekwa mwisho kabisaa kwenye hii release ikionyesha kwamba halina uzito sana na/au mamlaka husika haina uthibitisho wa kutosha juu ya kukosekana umakini katika uwekezaji huo.

Kwa waliowahi kuufatilia mgogoru huu, swala kubwa niko kwenye presentation ya thamani halisi ya mali ambazo NICOL inamiliki hasa ukizingatia uwezekano wa kufilisiwa kwa baadhi ya invetsments. Mtazamo ambao MGT ya NICOL inatofautiana na CMSA hasa kwakua wanaamini wana basis yakuriport kile wanachoreport.

Kwakua standards hizi zipo na Board zilizosibitiswa kutafsiri hizi standards zipo hili litapatiwa ufumbuzi.
 
Yetu Macho

Je huoni kama Financial statements zikikosewa zinaharibu decision making ya potential shareholder???!!
 
Last edited by a moderator:
hawa wakaguzi wao wamechukuliwa hatua gani kwa kukiri kosa walilofanya kama inavyoonesha hapo chini?

(b) Wakaguzi wa Hesabu wa NICOL walikiri kufanya makosa kwa kutoa hati safi (unqualified audit opinion) kuhusiana na taarifa hizo za hesabu za kampuni ya NICOL na Kumtaka mteja wao atayarishe upya hesabu hizo kufuatana na kanuni za kimataifa za Kihasibu na kuziwasilisha kwao kwa ukaguzi kabla ya kuzitoa kwa Umma.
 
Je huoni kama Financial statements zikikosewa zinaharibu decision making ya potential shareholder???!!
Upo sahihi na moja ya challenge ya auditing ni collussion ya management. Hawa wapuuzi wanajua fika mchezo waliokuwa wanaufanya. na ukweli ilikuwa lazima wakati wao ufike. Hii haina tofauri na Ponzi Scheme ile ya kina Madoff maana shareholders walikuwa wanataraji return kubwa.

Hawa ni wezi wakubwa. Hebu watoke mbele na wao tuwasikie. Jamani ukisoma majina ya hawa watu!!! Kina Rostam na Mengi wanafahamiana fika katika madudu yoote.


Hii ni mahakamani pia kama ile ishu ya DECI. They have to pay back the money.

Ni mchezo mchafu kupita na kukusanya pesa za walalahoi halafu wanajifanya wanailist company. Na ukianzishwa uchunguzi, wale waliowekeza huko nadhani watazirai kama sio kufa kabisa
 
Yetu Macho

Mbona unaandika kama vile linalotokea ni jambo dogo tu, na kama vile unajua sana? Si ufafanue basi tukuelewe?

Kama imebainika NICOL walidanganya, unaona ni sawa tu kuwa na presentation ya uongo, ili mradi ni ya kwao? Kununua hisa kwenye kampuni inayofilisika, wewe unaona ni umakini huo? Unahitaji kuthibitishaje ili ujue si umakini huo?

Jambo hili linahuisu upotevu wa mabilioni ya shilingi za wanahisa, kama wewe unajua lolote si ueleze jukwaa, badala ya kusema "Jambo ambalo limewekwa mwisho kabisaa kwenye hii release ikionyesha kwamba halina uzito sana na/au mamlaka husika haina uthibitisho wa kutosha juu ya kukosekana umakini katika uwekezaji huo.?"
 
Last edited by a moderator:
Mbona unaandika kama vile linalotokea ni jambo dogo tu, na kama vile unajua sana? Si ufafanue basi tukuelewe?

Kama imebainika NICOL walidanganya, unaona ni sawa tu kuwa na presentation ya uongo, ili mradi ni ya kwao? Kununua hisa kwenye kampuni inayofilisika, wewe unaona ni umakini huo? Unahitaji kuthibitishaje ili ujue si umakini huo?

Jambo hili linahuisu upotevu wa mabilioni ya shilingi za wanahisa, kama wewe unajua lolote si ueleze jukwaa, badala ya kusema "Jambo ambalo limewekwa mwisho kabisaa kwenye hii release ikionyesha kwamba halina uzito sana na/au mamlaka husika haina uthibitisho wa kutosha juu ya kukosekana umakini katika uwekezaji huo.?"
Huyo alitaka kutudanganya na financial statements. Atulie pembeni tena ili si suala la press release, we would like to see the guys appearing in the court. Hawa jamaa wanajua fika mchezo walioufanya and only independent investigation can uncover that. Waliimarket vizuri na wakaendelea kutajirika for the expense of poor Tanzanians. We have to dig deep down and I am sure alot of stuff will emerge.
 
Kazi kweli kweli. Kwa nini Rostam alikuwa na more less majibu ya haya tunayaona leo?? Hivi inawezekana kuwa pesa ina nguvu?? Nahitaji kuelimishwa zaidi!!!!
 
Kazi kweli kweli. Kwa nini Rostam alikuwa na more less majibu ya haya tunayaona leo?? Hivi inawezekana kuwa pesa ina nguvu?? Nahitaji kuelimishwa zaidi!!!!
Unaweza ukawa sahihi. Lakini kuna swali linabaki hapo. Ilikuwaje Mengi akajiuzulu juzi baada ya kuona hali si shwari na kutoa visingizio visivyo na maana. Hili linahitaji uchunguzi. I do respect some organs like NBAA etc. We would definitely like to see what there in. Na hii si ishu ya Mengi tu maana wapo na wengine pale walishakuwa na tuhuma kadhaa.
Shortly hii ni ile scheme kama Deci. Haiwezekani wachungaji pekee waende mahakamani this time tunataka kuona na kondoo nao wakifika huko
 
Back
Top Bottom