Nini tafsiri ya kukusanyika? Nikikaa mahali na mwenzangu mmoja, au wawili, au kumi au ishirini wakakaa karibu na mimi, hata kama siwajui, tumekusanyika? Na kama kukusanyika ni watu kukaa karibu, huo ukaribu ni ukaribu gani, hatua moja, hatua 10, au hatua ngapi?
Kesi nyingi kama sio zote za maandamano na/au mikusanyiko walizoshtakiwa watu wamekuwa wakishinda kwa sababu polisi wanashindwa kudefine maana za haya maneno...
Nadhani ili kwa sheria zilizopo "maandamano" na "mikusanyiko" ni lazima iwe ya kupngwa, na kwa malengo fulani. Ithibitishwe kuna mtu au watu walipanga maandamano au kukusanyika huko, na ithibitishwe maandamano au kukusanyika huko yalisababishwa kufanywa kwa jambo ambalo ni kinyume cha sheria. Vinginevyo makahama zitakuwa zinajaa watu kila siku lakini waendesha mashtaka hawatakaa watibitishe dhamira ya kukusanyika au kuandamana...