Serikali: Ukitaka kukaa mita 200, uwe na kibali

Serikali: Ukitaka kukaa mita 200, uwe na kibali

Polisi: Piga kura kisha rudi nyumbani

Rais: Piga kura kisha rudi nyumbani

Tume: Piga kura kisha rudi nyumbani

Mahakama: Itasema mkae mita 200 kwa kufuata sheria

Sheria inasemaje: Ili ufanye mkusanyiko nje ya mita 200 lazima uwe na kibali cha polisi

Polisi walisemaje: Piga kura rudi nyumbani

...Do I need to say anymore!?
Mbona sokoni, bar, hotelini na stand ya daladala watu wanakusanyika bila kibali cha polisi? Hatuishi kwa sheria tu
 
Piga kura, hesabu mita 200 na ongeza zingine 50, piga kambi hapo kusubiria matokeo (kulinda kura).
 
Polisi: Piga kura kisha rudi nyumbani

Rais: Piga kura kisha rudi nyumbani

Tume: Piga kura kisha rudi nyumbani

Mahakama: Itasema mkae mita 200 kwa kufuata sheria

Sheria inasemaje: Ili ufanye mkusanyiko nje ya mita 200 lazima uwe na kibali cha polisi

Polisi walisemaje: Piga kura rudi nyumbani

...Do I need to say anymore!?

You don't. You have embarrassed yourself enough already!
 
Mimi ninayependa kwenda kuangalia mechi za mchangani, ninawasiwasi kuna siku tutakamatwa kwa kukusanyika kuangalia mechi bila kibali
 
Hakuna waache kutuhadaa wanataka kuiba kura hatutakubali bora tufe tukiipigania haki yetu ya kikatiba kabisa
 
Mbona sokoni, bar, hotelini na stand ya daladala watu wanakusanyika bila kibali cha polisi? Hatuishi kwa sheria tu

Au kanisani, misikitini, mahali ilipotokea ajali, harusini, etc. Hawa jamaa Yaani serikali, CCM, Polisi na mashoga zao wote wana nia ya kuvuruga amani. Wana Nia ya kucheza faulo kwenye uchaguzi na wanawatisha Watu ili wapate mwanya wa kufanya hivyo.

Mwaka 2010 yapo maeneo kura zililindwa. Hatukushuhudia machafuko, ila tulishuhudia CCM wakijaribu kuingiza kura vituomi. Hili ndilo Rais, Polisi, CCM na NEC wanataka lisigundulike mwaka huu.
 
wenye sherehe zao za sijui kipaimara au komunyo ambao wako mita 200 wanatakiwa waahirishe siku au wakaombe kibali polisi, sasa hii sifa kwelilkweli.

Na bahati mbaya kukatokea msiba kwenye nyumba ndani ya mita miambili, hakuna ndugu kukusanyika siku hiyo ya tarehe 25 mpaka kibali cha polisi. Makubwa haya.
 
Hivi miccm ni mipumbavu namna hii?

Aliyewaambia kwamba tunakusanyika ni nani? Mimi nimetoka nyumbani mimi kama mimi, Napiga kura mimi kama mimi, nasubiri matokeo mimi kama mimi. Sijaja na mtu wala sitaondoka na mtu!! Hicho kibali nikachukue cha kukusanyika na nani? Jamani hata kama ninyi ni wajinga, msifunue midomo yenu kuthibitisha Upumbavu wenu aaaaah.!!

Hivi nikitoka nyumbani naenda kazini, nikakutana na waenda kwa miguu njiani wanaenda makazini kama mimi, inatakiwa niende Polisi nikachukue Kibali cha maandamano..!!!??? Huu ujuha hata Mfalme wa Majuha ataushangaa sasa..!!

BACK TANGANYIKA
 
Tanzania ni nchi pekee ambayo chama cha siasa(ccm) kinachotawala kinachoweza kutoa amri kinyume cha sheria na uzoefu rejea(precedence) na mamlaka za kidola zikafuata
 
Jana nilimsikia Chaulembo sorry Bulembo naye akitamka ya kwake kwenye mkutano wa kampeni za mgombe wa ni ile ile.
 
Amekurupuka! Nampa pole! Logic sifuri! Mimi binafsi bila mawasiliano na yeyote yule nitabaki si kwa lengo la kulinda kura Bali kusubiri kutangaziwa matokeo ya kura kwenye kituo changu! Kwa hiyo lengo langu si kukusanyika Bali kusubiri tangazo husika! Sasa hapo kibali cha nini wakati sheria imetoa nafasi ya kutangaziwa matokeo!
 
Waziri kuna kitu kasau Wanatakiwa pia wawe na kibali cha mwenye eneo hapo wanapokusanyika kama karuhusu eneo lake litumiwe kwa kukusanyika ambacho lazima kiindhinishwe na mwenye nyumba au eneo, mjumbe wa nyumba kumi ,na serikali ya mtaa au kijiji husika.

Viwanja vyote kama vya Jangwani ukitaka kufanya mkutano huendi tu polisi kuomba kibali cha kufanya mkutano Jangwani lazima uonyeshe na kibali cha wenye kiwanja kukuruhusu utumie huo uwanja.

Hivyo Polisi wasilisahau hilo pia ili kuepusha watu wasije kukusanyika mahali pa mtu bila kibali chake
 
Ndugu zangu wa Tanganyika, Nchi yetu bado ina sheria nyingi mno kandamizi na katiba yetu nayo inaminya sana uhuru wa Watanganyika. Kama alivyowahi sema Mwl J.K.Nyerere"....Katiba hii ni kiifuata inaweza kunifanya kuwa dikteta...". Kwa hali niliyoiona kwenye mkutano wa kampeni wa CCM inanitia shaka huko tuendako.

JPM bado ni mgombea lakini tayari kashaanza na mahakama kuzipangia muda wa kusikiliza na kutoa hukumu....amesema "....subirini niingie madarakani mtaniona..."

Vijana wote mtarudishwa vijijini kwani sheria ya Nguvu Kazi ya mwaka 1983 haijafutwa. Kipaimara, haruzi , misiba lazima mpate kibali kutoka polisi kwani sheria hii ipo ilitungwa na bunge la mkoloni na haijafutwa. hii ndo anayoitumia waziri wa mambo ya ndani


yangu macho
 
Piga kura, Linda kura...!!! Full stop..!!🐯🐯😨😨😨

Utumwa mwisho jpili...!!!
 
Polisi: Piga kura kisha rudi nyumbani

Rais: Piga kura kisha rudi nyumbani

Tume: Piga kura kisha rudi nyumbani

Mahakama: Itasema mkae mita 200 kwa kufuata sheria

Sheria inasemaje: Ili ufanye mkusanyiko nje ya mita 200 lazima uwe na kibali cha polisi

Polisi walisemaje: Piga kura rudi nyumbani

...Do I need to say anymore!?

Hapana inatosh tumekuelew..! Hapo ni kurud nyumbani tyuuu..!
 
Wakati Taifa likisubiri uamuzi wa kesi ya mita 200 iliyofunguliwa Mahakama Kuu ya Tanzania na Amy Patience Kibatala, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe, ambaye Wizara yake inasimamia jeshi la polisi ametoa tamko. Chikawe amesema kuwa zipo Sheria zinazoruhusu kuwapo kwa maandamano na mikusanyiko, zikiwataka wanaotaka kufanya hivyo kupata kibali cha polisi.

"Ikiwa kituo cha kupigia kura kipo nyumbani kwako huwezi kuhama nyumba, ila hupaswi kufanya sherehe. Piga kura na tii Sheria ya Uchaguzi. Kwa watakaotaka kukusanyika, waombe kibali cha Jeshi la Polisi kama Sheria inavyowataka. Tunachohitaji ni kuwepo kwa amani wakati na baada ya kumalizika uchaguzi mkuu" alisema

Chanzo: Mwananchi la leo, ukurasa wa 1 na 3

Swali langu binafsi: Polisi watatoa vibali hivyo?


Nchi yetu inayo viongozi wa ajabu sana.
 
Watanzania wamesahau nchi inavyoliwa..escrow mwaka Jana iliumiza mioyo ya watu sana na viongozi walibebana sana bungeni wapiganaji walipigana..Leo wanataka kuendelea na kuwapa nchi hii hatufikiri yaliyotokea ? Can't blv this is happening
 
Back
Top Bottom