Serikali: Ukitaka kukaa mita 200, uwe na kibali

Serikali: Ukitaka kukaa mita 200, uwe na kibali

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
Wakati Taifa likisubiri uamuzi wa kesi ya mita 200 iliyofunguliwa Mahakama Kuu ya Tanzania na Amy Patience Kibatala, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe, ambaye Wizara yake inasimamia jeshi la polisi ametoa tamko. Chikawe amesema kuwa zipo Sheria zinazoruhusu kuwapo kwa maandamano na mikusanyiko, zikiwataka wanaotaka kufanya hivyo kupata kibali cha polisi.

"Ikiwa kituo cha kupigia kura kipo nyumbani kwako huwezi kuhama nyumba, ila hupaswi kufanya sherehe. Piga kura na tii Sheria ya Uchaguzi. Kwa watakaotaka kukusanyika, waombe kibali cha Jeshi la Polisi kama Sheria inavyowataka. Tunachohitaji ni kuwepo kwa amani wakati na baada ya kumalizika uchaguzi mkuu" alisema

Chanzo: Mwananchi la leo, ukurasa wa 1 na 3

Swali langu binafsi: Polisi watatoa vibali hivyo?
 
Wameishaona mahakama itatoa tasfasiri sahihi. Kwa hiyo chikawe ametoa altenative nyingine ambayo wanafikili itawasaidia. Nafikiri wangetumia muda mwingi kuhimiza watu walinde kura zao kwa amani.
 
Polisi ndio wataondoa amani mwaka huu
 
Nini tafsiri ya kukusanyika? Nikikaa mahali na mwenzangu mmoja, au wawili, au kumi au ishirini wakakaa karibu na mimi, hata kama siwajui, tumekusanyika? Na kama kukusanyika ni watu kukaa karibu, huo ukaribu ni ukaribu gani, hatua moja, hatua 10, au hatua ngapi?

Kesi nyingi kama sio zote za maandamano na/au mikusanyiko walizoshtakiwa watu wamekuwa wakishinda kwa sababu polisi wanashindwa kudefine maana za haya maneno...

Nadhani ili kwa sheria zilizopo "maandamano" na "mikusanyiko" ni lazima iwe ya kupngwa, na kwa malengo fulani. Ithibitishwe kuna mtu au watu walipanga maandamano au kukusanyika huko, na ithibitishwe maandamano au kukusanyika huko yalisababishwa kufanywa kwa jambo ambalo ni kinyume cha sheria. Vinginevyo makahama zitakuwa zinajaa watu kila siku lakini waendesha mashtaka hawatakaa watibitishe dhamira ya kukusanyika au kuandamana...
 
Polisi: Piga kura kisha rudi nyumbani

Rais: Piga kura kisha rudi nyumbani

Tume: Piga kura kisha rudi nyumbani

Mahakama: Itasema mkae mita 200 kwa kufuata sheria

Sheria inasemaje: Ili ufanye mkusanyiko nje ya mita 200 lazima uwe na kibali cha polisi

Polisi walisemaje: Piga kura rudi nyumbani

...Do I need to say anymore!?
 
Yaani hawa wanaharibu mambo! Kwa magari waliyopewa na ile dhana ya ulinzi shirikishi! Wanashidwaje kulinda amani kwa wale watakao kuwa mita miambili kutoka kituoni?
 
Huyu waziri ndio mjinga kabisa.
Kila mtu ana haki ya kupiga kura, kulinda kura yake. Hii haihitaji kibali cha mtu yoyote.
Sasa anachotaka kusema kukaa mita 200 baada ya kupiga kura kunahitaji kibali?
 
Polisi: Piga kura kisha rudi nyumbani

Rais: Piga kura kisha rudi nyumbani

Tume: Piga kura kisha rudi nyumbani

Mahakama: Itasema mkae mita 200 kwa kufuata sheria

Sheria inasemaje: Ili ufanye mkusanyiko nje ya mita 200 lazima uwe na kibali cha polisi

Polisi walisemaje: Piga kura rudi nyumbani

...Do I need to say anymore!?

Na CCM ilianza kusema piga kura rudi nyumbani.
Kumbuka kuwa na CCM imejiandaa kwa goli la mkono pia.
 
Waziri anapingana na amri halali ya rais? JK timua huyu hata kama zimebaki siku tatu, maana hakuna namna!
 
Polisi: Piga kura kisha rudi nyumbani

Rais: Piga kura kisha rudi nyumbani

Tume: Piga kura kisha rudi nyumbani

Mahakama: Itasema mkae mita 200 kwa kufuata sheria

Sheria inasemaje: Ili ufanye mkusanyiko nje ya mita 200 lazima uwe na kibali cha polisi

Polisi walisemaje: Piga kura rudi nyumbani

...Do I need to say anymore!?

Hujasema ya jaji lubuva na ya othman chande au hukuwaelewa?
 
Kwanza hatuna waziri technically, Rais alipovunja bunge mawaziri walipaswa kuwa hawapo. Kwa kuwa huwezi kuwa waziri bila kuwa mbunge. Hizi ndio baadhi ya sheria za kijinga za kuwa na watendaji ambao ni wanasiasa. Mawaziri wasiwe wabunge period.
 
Back
Top Bottom