Phd Hewa
JF-Expert Member
- Oct 3, 2016
- 572
- 466
Kumekua na Sintofahamu Juu ya ununuzi wa korosho mwaka huu.
Kutokana na utaratibu wa ununuzi wa korosho inasemwa kwamba mkulima atakwenda kuuza korosho zake galani lakini pesa atakwenda kupokelea bank.
Kwa utaratibu huo maana yake mkulima atatakiwa afungue account ya bank.
Lakini wengi wamekua wakijiuliza maswali ikiwa unatakiwa kupokelea bank je yule wa kg 20
au kg 10 nae akafungue account au kuna utaratibu Mwingine juu ya malipo kwa mkulima ambae amepata mavuno madogo?
Kwani siyo wote ambao wanapata mavuno makubwa wengine kufeli kwa kukosa mazao ya kutosha kutokana na pembe jeo kuwa duni au hali ya hewa au ukata wa kifedha kutokana na kushindwa kuihudumia etc.
Pia kama utaratibu ndiyo huo mbona hatuoni elimu ikitolewa kwa wakulima?
Wengine wakaenda mbaaali na kusema tunapelekwa bank ili wakatukate kodi sina uhakika na hilo.
Lakini kwa hili la mkulima wa zao la korosho kutakiwa akapokelee bank tafadhali serikali tupeni ufafanuzi juu ya suala hili.