bampami
JF-Expert Member
- Nov 5, 2011
- 5,697
- 4,107
Wawenzangu,
Kwa sisi watumishi wa serikali, tumekuwa tukisubiri ruhusa ya uhamisho wa watumishi bila mafanikio, kiukweli kukaa mbali na familia ni jaribu lingine katika maisha, kwani:
1.Gharama za maisha zinakuwa juu kutokana na matumizi kuongezeka.
2.Mkikaa mbali kuna uwezekano mkubwa wa kuleta migogoro katika ndoa hasa ya kimahusiano na kimapenzi (ndivyo hali ilivyo sasa)
3. Familia kukosa huduma za wazazi wote wawili.
Na mambo mengi yafananayo na hayo.
Serikali tunaomba sasa mruhusu uhamisho wa watumishi ukizingatia kuwa vyeti vya ndoa tunavyo sidhani kama inaweza kuleta shida au ujanja ujanja.
Naamini ujumbe utawafikia, na mtalifanyia kazi.
Ahsante!!