Serikali tunaomba mruhusu uhamisho wa watumishi

Serikali tunaomba mruhusu uhamisho wa watumishi

Hawa watu huwa hawana huruma na maisha ya watu wengine...wanatesa sana binadamu wenzao....tunamwachia mungu atajua anashughulika vipi na watu wanaonyanyasa binadamu wenzao
 
Huwezi kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja. Chagua mmoja kati ya mwajiri na mme au mke.
 
Wakiendelea kuzuia wanatengeneza tatizo lingine kubwa. Sijui kwann wanajiamini kupita kiasi!?.
 
Kuwanyima watumishi uhamisho kwakweli serikali imewaumiza kuliko hata nyongeza ya mishahara
 
Wa[emoji1241]wenzangu,
Kwa sisi watumishi wa serikali, tumekuwa tukisubiri ruhusa ya uhamisho wa watumishi bila mafanikio, kiukweli kukaa mbali na familia ni jaribu lingine katika maisha, kwani:

1.Gharama za maisha zinakuwa juu kutokana na matumizi kuongezeka.

2.Mkikaa mbali kuna uwezekano mkubwa wa kuleta migogoro katika ndoa hasa ya kimahusiano na kimapenzi (ndivyo hali ilivyo sasa)

3. Familia kukosa huduma za wazazi wote wawili.

Na mambo mengi yafananayo na hayo.

Serikali tunaomba sasa mruhusu uhamisho wa watumishi ukizingatia kuwa vyeti vya ndoa tunavyo sidhani kama inaweza kuleta shida au ujanja ujanja.

Naamini ujumbe utawafikia, na mtalifanyia kazi.

Ahsante!!
Kwa hio serikali pia irudi Dar????
Mana waliohamishiwa Dodoma wengi wao wamekumbwa na hayo uliyosema
 
Wanasema wanaweka system kwenye kila computer ya serikali ili kila mtumishi aombe online. Sasa ukiangalia mpaka waweke hiyo system ni lini, fedha zitoke, zipitishwe, mchakato uanze tena tanzania yote hiyo si 2025? Ndicho kituumizacho hicho.
Zamani walikua wanaruhusu sema watumishi wakatumia nafasi hiyo kuwa wanahamia mijini na kuacha sehemu nyingi zikiwa na uhaba wa huduma.

Hapo labda uhamishie familia ulipo... maana sioni kama wataruhusu hivi karibuni kama wanaongelea mambo ya kutengeneza online system

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom