Serikali Tatu ni mhimu. Katiba ya Warioba iendelee

Salam zangu ziwafikie Kabudi, Warioba na Polepole.

Sasa nawaelewa rasmi kwamba maoni ya wananchi yalikuwa sahihi.

Muundo wa Serikali tatu Sasa unaanza kuonekana ni mhimu ukawepo. Serikali Moja na hii ya Sasa zinamapungufu mengi.
Kwanini sio ya Chenge?
 
Serikali 3 si takwa la watanzania walio wengi bali la WANASIASA...kwa ajili ya UPANA wa wigo wa madaraka tu....
 
Eti serikali 3 iwe na rais wa JMT na wa Tanganyika....vile vichekesho vya misigano ya WAKURUGENZI NA WAKUU WA WILAYA.....
 
Muungano uvunjike tuu hauna faida kwetu bara zaidi ya hasara tupu
Ajabu ni kuwa kila anapokuwa Rais Mzanzibari...baadhi yetu wabara tunataka muungano uvunjike

G55 kipindi cha mzee Mwinyi

Kuna yasiyo na afya kwa taifa nyuma ya "pirika" hizo....
 
Burundi....

Hussein Rajab(CHAIRMAN) wa CNDDFD alipata kuingizana misukosukoni na Rais wake hayati Pierre Nkurunzinza.....sababu ya kila mtu "kuvimba" eneo lake...na kweli walikuwa mafahari...

Eti leo Rais wa JMT amvimbie Rais wa Tanganyika ilihali JESHI /MAJESHI yake siku zote yatamtii kwa kukumbuka kuwa UHURU uliopatikana 1961 una KUMBUKUMBU nzito mno zaidi ya makubaliano ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Uhuru wa 1961 unaanzia VITA VYA MAJIMAJI...unakuja harakati za wazee kule Bandarini.... kupatikana AA...ikaja TAA hadi TANU...historia ya moto hii....eti huyo rais wa JMT ya kuchanganya udongo amtambie mwamba wa "TANGANYIKA"..

MUUNGANO HAUPO IKIWEPO SERIKALI 3
 
Ccm acheni kujivika mamlaka ya kuamulia wananchi muundo wa serikali..... wananchi walishasema wanataka 3.
Wananchi gani ?!!!

Ile katiba ya Jaji Warioba ilikuwa na "jaggons za kisheria" zaidi ya UHALISIA wa historia ya taifa hili....

Hayati Nyerere aliona mbali zaidi ya aonavyo mh.mzee Warioba.....

Nilifuatilia mchakato wa ile iitwayo "katiba ya wananchi"....utashangaa kabisa....

Mchakato uliporwa na WANASIASA...kila wapitapo....Chadema ,CUF na wenzao walikuwa wanajazana kupata nafasi ya kutoa MAWAZO YAO(makada watupu)

Kule Zanzibar ndio hatari zaidi....UAMSHO na COMPATRIOT wao waliiteka mikutano ya kukusanya maoni ya wananchi...

Katiba ya "wananchi" chini ya mzee Warioba ilijaa MANYAGO mengi sana.....
 
Salam zangu ziwafikie Kabudi, Warioba na Polepole.

Sasa nawaelewa rasmi kwamba maoni ya wananchi yalikuwa sahihi.

Muundo wa Serikali tatu Sasa unaanza kuonekana ni mhimu ukawepo. Serikali Moja na hii ya Sasa zinamapungufu mengi.
Mhimu = muhimu. Nadhani katiba mpya iweke mkazo kwenye mambo ya elimu ili tupunguze idadi ya watu wasioweza hata kuandika vizuri kiswahili.
 
Una faida gani zaidi ya kutuletea mikelele tu hapa. Watu wenyewe hawana adabu ubishi tupu.
Nje ya Muungano kuna haya :-

-Ugaidi wa kidini

-Ugaidi wa kikomunisti

-Siasa za kidini

-Uhafidhina uliotopea wa siasa za kikabila na kikanda
 
Back
Top Bottom