Serikali (TAKUKURU) yakamata Tani 4,900 za Sukari iliyofichwa Mbagala na Tabata jijini Dar

Zama za kugaiwa maind imesha sasa ni sukari. Tunaelekea nchi yenye maziwa na asali. Tutagaiwa lini hiyo sukari
 
wewe haya matusi na mapovu yote ya nini?hauwezi kujibu hoja bila kutukana?
chanzo cha sukari kuhadimika ni serikali yako na chanzo cha sukari kupanda bei ni serikali yako.
serikali ingedhibiti kwanza ongezeko la bei la bei na ufufuaji wa viwanda vya sukari,kagera &mtibwa sugar hali mbaya.
serikali haiko makini na wananch wake zaidi ya kufanya maigizo tu,likitoka la sukari litakuja la mchele na likija la mchele ndio wakati wa kupiga pesa store nina gunia 900

Acha kutoa hojoa za kipuuzi,,sukari imeadimika siku chache zilizopita,upanuzi wa viwand siyo jambo la usiku mmoja kama unavyokula la kwenda chooni,,hapa serikali inashughulikia tatizo la muda mfupi ambalo liko wazi kabisa,watu wameficha sukari hiyo ambayo inapatikana kwa uchache viwandani ambayo ingeweza kutusaidia bila kulanguliwa,,nyinyi wajinga mlio msafisha lowasa nani amewaroga?
 
Kwani unajua sukari imeadimika kwa ajili gani?
Kuna shortage ya sukari hilo halina ubishi... Lakini kuficha sukari ukisubiri bei iende juu uuze pia kupo..

Kumbuka Magufuli alivyopiga ban ya sukari kuagizwa nje aliweka wazi kuwa kuna upungufu wa kama Tani laki moja na hizo vitatolewa vibari maalumu kuagiza.. Sasa wanachofanya hawa wafanyabiashara ni kuhaminisha tatizo sio hizo Tani laki moja bali zaidi ili wapewe order ya kuagiza sukari. Na serikali imefanya vizuri kwa wao wenyewe kuagiza na sio kuwapa wafanyabiashara ambao wanaenda kununua iliyoharibika..
 
Kule mtibwa au huko kilombero siwalikuwa wanalalamika sukar haitok kwa kuwa ya injee inabei nafuu sasa hawazalishi kwan? Siwauze tu kwa uhuru nw
 
Mkuu huko ulaya ni mbali sana, umeshaangalia bunge la Kenya wakiamua kusimamia mambo ya msingi linavyokuwa?? Sisi wabunge wanaacha kujadili mambo ya msingi wanaanza kutukanana na kususa na kutoka nje ya bunge.. Yaani mimi ndio maana hata sioni wabunge wanachofanya, wote tu wa upinzani na CCM.. Mpaka tutakapoamua kuwa serious ndiyo hii nchi itakimbia kwenye maendeleo.. Huwa naona ni bora Rais Magufuli na watendaji wake wapige kazi hawa wabunge waache waendelee kupigana vijembe huko bungeni..
Mimi sikuweka matumaini yoyote kwa wabunge wengi wa CCM kuhusu kuisimamia serikali kikamilifu lakini hata wale ambao nilitegemea kuwa mfano kwa wabunge wa CCM kumbe ni wala rushwa wakubwa.

Mbunge wa CCM kama Kangi Lugola nilidhani ni mzalendo kumbe nilijidanganya sana.

Nadhani Mnyika hataniangusha katika kusimamia maslahi mapana ya nchi.

Siasa za vyama kwa sasa zinakuwa ni zaidi ya maslahi ya taifa.
 
Mimi sisikilizi mtu, natumia akili yangu.. Sikwenda shule kucheza au kukua..

Siwezi kukaa kusikiliza mtu, nang'amua kwa akili yangu mwenyewe.. Wewe unakaa kusikiliza nani kasema kipi, ndio maana wengi humu kila mnachoongea mnamaliza na Lissu kasema sijui Mbowe alisema yaani hamna vision kabisa..

Lowassa akiwa Waziri Mkuu alikuwa anafukuza wakandarasi na wakurugenzi tukawa tunasifia ni Mzee wa maamuzi magumu, JK alikuwa anaunda tume kuchunguza tukasema watu wanafanya makosa wanaacha kuwajibishwa wanaundiwa tume na tume inatumia kodi za wananchi.. Huyu wa sasa akifukuza mnasema anavunja sheria sasa Lowassa alivyokuwa anafukuza alikuwa havunji sheria??

Tukija kwenye sukari, wewe unaona ni sawa mtu kuweka sukari ndani akisubiri bei iwe juu ndio auze?? Naomba hili unijibu kwa akili yako usiseme Lissu au Lema kasema....

Sijui kama atakujibu..!
 
Ungeweka hapa na matumizi ya sukari kilo moja inaweza kutumiwa na watu wangapi na kwa siku ngap? Alafu tuendelee na hoja..!
Ton 4900 X 1000 =4,900,000 kgs
Tuchukulie watu 40m kati ya 50m wanakula sukari kwa siku..
4,900,000 / 40,000,000 = 0.01225 gramms kwa kila mwananchi na kwa siku moja na kesho imekwishaaaa...
hiyo ilofichwa kama imefichwa sio tatizo
 
Nchi inakoelekea dah serikali na wafanya biashara, serikali wangetumia busara tu kupunguza vikwanzo vya kuingiza sukari nje ya nchi nadhana hata hizo stock zao zisingekuwa na faida.Wafanya biashara wana mchango mkubwa sana kuinua uchumi wa nchi wakigoma hata Sera ya kutumbua majipu itawekwa kando.
 
Kuna shortage ya sukari hilo halina ubishi... Lakini kuficha sukari ukisubiri bei iende juu uuze pia kupo..

Kumbuka Magufuli alivyopiga ban ya sukari kuagizwa nje aliweka wazi kuwa kuna upungufu wa kama Tani laki moja na hizo vitatolewa vibari maalumu kuagiza.. Sasa wanachofanya hawa wafanyabiashara ni kuhaminisha tatizo sio hizo Tani laki moja bali zaidi ili wapewe order ya kuagiza sukari. Na serikali imefanya vizuri kwa wao wenyewe kuagiza na sio kuwapa wafanyabiashara ambao wanaenda kununua iliyoharibika..
Upungufu ni tani laki 3. Kwa mwaka sio laki moja, kwa nn hajaagiza kwanza ndo apige marufuku? Wewe unaona ni sawa watu wapate shida kwanza ndo aagize anavotaka yeye? Kumbuka hakukuwa na uhaba wa sukari kabla ya agizo lake, halafu unasema wafanyabiashara wanaleta sukari ilioharibika!!? Au unaota saa hizi!?
 
Cha ajabu hutamsikia mwenye mzigo akitajwa
Ni sawa na yule mfanyakazi wa TRA aliekuwa akibeba mshahara wa watu 17
Hajatajwa kisa kesi iko mahakamani, hivi serikali hii ipendavyo sifa isimtaje huyo mtu kweli?
 
Ton 4900 X 1000 =4,900,000 kgs
Tuchukulie watu 40m kati ya 50m wanakula sukari kwa siku..
4,900,000 / 40,000,000 = 0.01225 gramms kwa kila mwananchi na kwa siku moja na kesho imekwishaaaa...
hiyo ilofichwa kama imefichwa sio tatizo

Kwa iyo kwako wew siyo tatizo kwa mtu mmoja kuficha sukari ambayo ingeweza kutumiwa na familia za watanzania wote kwa siku moja? Yani tuseme kesho nchi nzima hakuna mtu atakae kunywa chai kwakuwa sukari kuna jamaa kaificha ndani? vipi hawa wafanyabiashara wakawa kumi au hamsini nchi nzima? Unaiona impact yake?
 
Watu wameficha mapesa huko bank tunashuhulika na sukar hahahahahaha tutumie asali tu sasa
 
Hivi kumbe kuna sheria inamlazimisha mtu kuuza bidhaa yake?
Siyo yake, hakuitengeneza wala kuilima yeye. Kasome sheria ya uhujumu uchumi.
Hivi kweli mtu mmoja ana withold tani 4,900! Maana yake ni kuwa tukiwa na watu 100 tu wa aina hii maana yake ni kuwa sukari tani laki 490 witheld. Uwezo wa production wa viwanda vyetu kwa mwaka ni tani laki 350 na mahitaji ya nchi ni tani 500! Maana yake ni kuwa hata serikali iagize kiasi gani cha sukari kutoka nje kufidia uhaba, hawa watu wana uwezo wa kui withold.
Wanaweza fanya hivyo kwa bidha yo yote watakayopenda: nyama, bia, dawa nk.
Hata huko benki angalao huwa kuna witholding tax.
 
Mimi sikuweka matumaini yoyote kwa wabunge wengi wa CCM kuhusu kuisimamia serikali kikamilifu lakini hata wale ambao nilitegemea kuwa mfano kwa wabunge wa CCM kumbe ni wala rushwa wakubwa.

Mbunge wa CCM kama Kangi Lugola nilidhani ni mzalendo kumbe nilijidanganya sana.

Nadhani Mnyika hataniangusha katika kusimamia maslahi mapana ya nchi.

Siasa za vyama kwa sasa zinakuwa ni zaidi ya maslahi ya taifa.
Mnyika ni smart sana.. Huwa naona huyu jamaa ni zaidi hata ya Lissu kwa kuisaidia nchi..

Lissu ni smart ila anakupanic flani na ni mtu anayependa ubishi na majibizano yasio na msingi. Mnyika alinikosha sana kipindi kile analeta mswada wa manunuzi wakati wa Werema alafu akaishia kukashfiwa lakini Magu alipoingia aliamrisha Sheria ya Manunuzi itazamwe upya..

Wabunge wa CCM na Serikali wakubali kutumia vipaji walivyonavyo Mnyika na Lissu vinaweza kuwa msaada. Lakini na wao waache ujinga wa kumtuhumu Rais kwa kila anachokifanya hata kama ni kizuri.. Mara nyingine ndio maana naona serikali inaamua makusudi kukataa hata mambo ya msingi yanayoletwa na upinzani kwasababu hata wao wenyewe wanavyopeleka mambo hayo wanatumia lugha ambazo si nzuri na kejeli.. Mfano; huwezi kumtukana Rais ni legelege hadharani mbele ya Watanzania alafu kesho ukamwomba Rais huyo huyo kupitia cabinet yake ilireview ushauri wako... Hapa ndio tunatakiwa tuwe na siasa za staha na kujenga hoja..
 
Nchi inakoelekea dah serikali na wafanya biashara, serikali wangetumia busara tu kupunguza vikwanzo vya kuingiza sukari nje ya nchi nadhana hata hizo stock zao zisingekuwa na faida.Wafanya biashara wana mchango mkubwa sana kuinua uchumi wa nchi wakigoma hata Sera ya kutumbua majipu itawekwa kando.

Wafanyabiashara wa aina hii ni hasara kwa taifa..!!
 
Rais Magufuli aache ubabe bhana biashara huria kwan lazma nitoe stoke yangu yote? Aboreshe viwanda vya kuzalisha sukar iwe nyng sio kuingilia biashara za watu subir serikali italipa hili km mtataifisha hiyo sukar iwe km zile samak
Mdogo wangu, Sheria ipo Wazi unaponunua mzigo unaotakiwa kuuzwa ndani ya nchi kwa jumla na kutoka kiwandani moja kwa moja moja lazima uiweke sokoni ili kuzuia mfumuko wa bei, na kunufaisha Serikali + upatikanaji wa bidhaa husika kwa wananchi wote.
Unatetea hilo, OK mbona kipindi wafanya biashara wanaficha Mafuta/Petrol kusudi wauze kwa faida uliwalalamikia Wale wafanyabiashara wa Mafuta?
Kwanini hawa unawatetea?
 
mkuu hawanaga hoja za maana wanajifanya wapenda nchi kumbe wameweka mbela vyama vyao kwao serikali ha

Back
Top Bottom