Serikali (TAKUKURU) yakamata Tani 4,900 za Sukari iliyofichwa Mbagala na Tabata jijini Dar

samsun

JF-Expert Member
Feb 9, 2014
7,386
5,962
Baada ya muda mfupi wa rais kusema kuwa kuna wafanyabiashara wameficha Sukari, muda huu imeripotiwa kuwa huko Mbagala kuna Sukari ya zaidi ya tani 4,900 kwenye ghala la mfanyabiashara mmoja na imeelezwa zitachukuliwa hatua stahiki.

Chanzo: TBC, habari mpasuko.

==========
Updates:
==========

Taasisi ya kuzuia na Kupambana na rushwa (TAKUKURU) yabaini kuwepo kwa sukari iliyofichwa tani 4,579.2 iliyonunuliwa toka Kiwanda cha Sukari Kilombero.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Valentine Mlolowa Taasisi hiyo imeanza uchunguzi dhidi ya swala hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa mnamo tarehe 05 Mei, 2016 timu ya uchunguzi ilitembelea maghala yaliyopo Tabata Jijini Dar es salaam na kubaini uwepo wa sukari hiyo.

TAKUKURU tayari imetembelea Maghala ya mfanyabiasha Haruni Daudi Zacharia ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Al-Naeem yaliyoko Mbagala na Tabata ambaye ni miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa wa sukari hapa nchini na anayetuhumiwa kuficha bidhaa hiyo. Ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha uchunguzi uliofanywa na Taasisi hiyo ulibaini kuwepo kwa njama za dhati za kutouza sukari iliyokutwa katika maghala hayo kulikofanywa na mfanyabiashara huyo kwani hata sehemu ya Maghala ilipo sukari hiyo hapakuwa na dalili za upakiaji wa sukari hiyo ili iweze kusambazwa.

Taarifa hiyo imeendelea kufafanua kuwa katika eneo la Kitumbini kumekuwa na wananchi wengi wanaohitaji bidhaa hiyo na wachache sana waliweza kuuziwa licha ya ukweli kwamba sukari ilikuwepo.

Katika uchunguzi wake TAKUKURU pia imebaini kuwepo kwa mikakati ya dhati iliyokuwa ikifanywa na mfanyabiasha huyo kwa kununua sukari yote toka viwanda vya ndani na kisha kuihifadhi na kuuza bidhaa hiyo kidogo kidogo kwa wastani wa tani 250 kwa siku wakati alikuwa na uwezo wa kuuza zaidi jambo lililochangia uhaba wa sukari katika soko.

Kuficha bidhaa ni kosa la uhujumu uchumi na ni kinyume na Aya ya 3 Jedwali la kwanza Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 [Chapisho la Mwaka 2002]. Serikali haitavumilia hujuma za namna hii na itachukua hatua kali dhidi ya mfanyabiashara yeyote ataekwenda kinyume na sheria hii.

TAKUKURU imetoa wito kwa wafanyabiashara wote wa sukari kuacha vitendo vya kuficha sukari na vyombo vya uchunguzi vinafuatilia kote nchini na yeyote atakayebainika kufanya hujuma hizo atakabiliwa na mkondo wa Sheria.

======
Kuna mdau amewahi kudokeza hapa mwaka jana juu ya mienendo ya mfanyabiashara huyu. Soma Zakaria Haruni ndiye muagizaji pekee wa sukari na halipi kodi
 
Kuna ushahidi gani kama hiyo sukari ilikuwa imefichwa? ama kweli Nchi inaendeshwa kwa mizuka
Una uhakika sukari aijafichwa kama haijafichwa kwa nini mtaani imeadimika na wakati kwenye magodown ipo,au wameweka uko kwa ajili ya urembo sasa apo mzuka upo wapi/si mlikiwa mnalalamika sukari imeadimika au siyo nyie ukawa?sasa bado mnalalamika tena sukari kikamatwa kwenye magodown
 
sukari ya kwangu mnalazimisha nini?wakati nateseka kulima,kupanda na kuvuna mlikuwa kimya leo mnaikomalia sukari kilazima,huu ni ujinga.
kama mambo yakiendelea hivi itafikia kipindi watu walio na pesa nyingi kwenye account zitachukuliwa kilazima ili kusaidia wengine
 
Hii movie imetengenezwa.Ngoja muone kama kutakuwa na serious case katika hili.



Huyu ndiyo Raisi bhaana, mtetezi wa Wanyonge!
kat4.jpg



kat5.jpg
 
Rais Magufuli aache ubabe bhana biashara huria kwan lazma nitoe stock yangu yote? Aboreshe viwanda vya kuzalisha sukar iwe nyng sio kuingilia biashara za watu subir serikali italipa hili km mtataifisha hiyo sukar iwe km zile samak
 
Back
Top Bottom