Serikali tafadhalini wasaidieni abiria wa daladala wa Dar es salaam

Msukuma Original

JF-Expert Member
Oct 2, 2018
928
3,330
Sasa hivi kuna wizi wa kulazimishana unafanywa na makonda wa daladala. Makonda na madereva wanaweka mazingira ya kulazimisha watu walipe nauli mara mbili ya nauli halali.

Wanachokifanya ni hivi: wakifika kituo cha mwisho wa gari wanawatoza abiria kulipa nauli ya kuzunguka. Yaani ukipandia upande wa pili wa kituo cha daladala wanakuambia ulipe nauli mara mbili kisa eti unazunguka na gari.

Na ukisema usubirie gari upande wa pili huwezi kupata gari maana tayari gari itakuwa imeshajaa kutokea ule upande wa pili.

Cha ajabu zaidi ni kwamba ikifika mida ya jioni wanakuwa hawataki kupeleka daladala kituo cha mwisho. Wanatega kituo kimoja kabla ya kituo cha mwisho ili abiria apandie pale wapate justification ya kudai nauli mara mbili.

Utakuta magari kibao yapo tupu (kwa mfano kituo cha goldstar) yanaitia abiria wakati abiria kibao wasiokuwa na hela ya kulipa mara mbili wanasubiria kituo cha mnazimmoja ambacho ndio kituo cha mwisho.

Kwa hiyo abiria mwenye nauli kamili ya kumrudisha nyumbani hawezi kupata usafiri mida ya jioni kwa sababu makondata wanayaweka magari kituo cha goldstar ili wapate nauli mara mbili.
 
Back
Top Bottom