Nauli za daladala Dar zinabadilishwa badilishwa makusudi, LATRA tusaidieni

Vn6

New Member
Dec 2, 2023
1
2
Ni wiki kadhaa tangia mamlaka zitangaze ongezeko la nauli( kulingana na kilometers). Lakini kuna mchezo mchafu unaendelea unaofanywa na makonda na madereva wa daladala ambapo wanapandisha nauli zaidi ya viwango tajwa.

Wananchi wanashindwa kutetea kutokana na kuwa na ufahamu tofauti, unakuta daladala za route moja unapanda unakuta wanatofautiana nauli, mimi ni shahidi tena wengine wana ticket zenye bei mbili tofauti za nauli wakiona unawabishia wanakupa tiketi ya nauli iliyozidi ili usibishe

Serikali iliangalie sababu pamoja na kupanda hizi gharama bado kuna manyanyaso makubwa abiria wanapitia

Baadhi ya route ambazo nimekuwa shahidi ni G/mboto-Mnazi Mmoja Bunju-Sim2000, G/mboto-Kawe, M/rangi3-Mawasiliano, M- rangi3-G-mboto.
 
nchi ishakuwa gari bovu hii,wacha kila mtu ale kwa urefu kwa kamba yake.

route ninayopanda mimi nauli imeongezeka 400.
watu wako ofisini wamevaa mashati ya ccm na matumbo makubwa kama mifuko ya shangazi kaja.
 
Back
Top Bottom