Serikali tafadhali rudisha Fao la Kujitoa

Mfia nchi

Member
Jul 18, 2019
89
162
Rais, najua huamini kama maisha ni magumu labda kwa sababu wewe una kila kitu, hujawahi kukosa hela ya kuilisha familia yako, mbaya zaidi wanaokuzunguka hawakuambii ukweli, pengine nao kwa sababu nao wana kila kitu kama wewe.

Ukweli ni kwamba maisha ni magumu sana iwe kwa wasomi waliokosa ajira na kwa Watanzania wengine. Ndugu Rais ajira hakuna, basi turudishie fao la kujitoa tupate hela zetu tujiajiri.

Tunakosa hata hela ya kulisha Familia zetu wakati hela tunazo ila zimeshikiliwa na hii mifuko. Hivi huoni kama ni uonevu kutuacha tuteseke kwa njaa wakati kuna mamilioni yetu yameshikiliwa kimabavu?

Rais tunaomba hela zetu tuweze kujiajiri maana ajira hakuna.

Siku zote umekuwa ukijipambanua wewe ni rais wa wanyonge, wanyonge turudishie fao la kujitoa.
 
Kama huna ajira unawezaje kudai fao la kujitoa?

Lakini kumbuka fao la kujitoa linapitishwa bungeni hivyo mweleze Mbunge wako apeleke hoja bungeni Rais Magufuli hapo haingii ni kazi ya wabunge.
 
Hata wakirudisha fao la kujitoa bado tutateseka tu. Mifuko ya Hifadhi ya Jamii imebaki mitupu, haina pesa. Pesa za michango toka sekta binafsi zimelambwa na CCM na nyingine zilishatumika kununulia ndege kwa cash siku nyingi tu. Uchaguzi wa mwaka huu ilibidi CCM ikombe pesa kutoka Bima ya Afya (NHIF). Usione foleni za wazee kule NSSF Ubungo na mahli pengine. NSSF haina uwezo wa kulipa. Wengine wana miaka mitano toka wastaafu hawajaambulia hata senti tano. Sifa za midege, mafly over, standard gauge na nyinginezo zinatumaliza. Kilangila.
 
Mitano tenaaa , na ikiisha hii walioshiba mpk wakavimbirwa wanampa mingine isiyo na ukomo kwa niaba yako.
 
Kama huna ajira unawezaje kudai fao la kujitoa??!!
Lakini kumbuka fao la kujitoa linapitishwa bungeni hivyo mweleze Mbunge wako apeleke hoja bungeni Rais Magufuli hapo haingii ni kazi ya wabunge.
Mkuu samahani! Umewahi kuajiriwa? Huoni kama unajidhalilisha kwa hii comment yako? Unadhani mleta mada ni mjinga kuomba fao la kujitoa lirudishwe wakati hajawahi kuajiriwa?
 
Back
Top Bottom