Macos
JF-Expert Member
- May 12, 2008
- 1,979
- 1,416
Naiasa serikali ichukue haraka hatua za kudhibiti siasa kali za kidini huku bara kama ambazo tayari zimezusha vurugu Zanzibar. Sheikh Ponda na mujahidina wenzake pia wanakusudia kuleta vurugu kama za Zanzibar kwa kisingizio cha NECTA na sensa ya watu na makazi. Nimewaona leo asubuhi CHANNEL TEN katika kipindi cha baragumu ponda na mwenzie simkumbuki jina wakitoka mapovu na alot of unfounded claims.
Kwa kifupi ni watu waliokusudia kuivuruga nchi kwa udini, ninaloweza kuwaambia na nina hakika nalo haitatokea siku nchi hii ikaongozwa kidini kama anavyotaka ponda na wenzie. Tatizo lililopo NECTA kwa mujibu wa waheshimiwa hawa ni uwepo wa katibu mtendaji mkristo na mwenyekiti wa bodi mkristo, lakini waziri wa elimu na katibu mkuu wake kuwa waislamu si tatizo hata kidogo.
Dini zetu zinakuwa na maana na manufaa kwa waumini wake na taifa kwa ujumla kama zinajishughulisha na masuala ya maendeleo ya kijamii ya waumini wake. Kama dhehebu linafumbia macho masuala ya elimu na afya za wafuasi wake ni wazi litakumbwa na matatizo, mi mwislamu lakini sisiti na siogopi kuwasifia wenzetu wakristo na hasa wakatoliki kwa jinsi wanavyowekeza katika masuala ya afya na elimu kwa kujenga hospitali na shule na vyuo kadha wa kadha. Sisi tuna chuo kikuu kimoja tu na si cha kujenga wenyewe bali kupewa bure na serikali wenzetu wamejenga wenyewe vyuo takribani kumi, ni vipi tunataka tufanane na watu kama hao? Angalia uendeshaji wa shule zao mfano Kifungilo, marian, St Francis hivi kweli unaweza linganisha na uendeshaji wa Kinondoni muslim, haramain au jumuiya? Waislamu wenzangu tunaokitakia mema kizazi chetu tupeleke wanetu kwenye shule za kweli zenye walimu,vifaa na usimamizi wa kutosha bila kujali wamiliki wake ni wa ibada gani.
Tuwaandalie wanetu mazingira mazuri ya ushindani hapo baadaye kwa kuwapa elimu bora. Mwenzie Ponda anadai eti hospitali za kikristu zinabagua, katoa mfano wa KCMC kuwa mgonjwa ukifika unaaulizwa unatoka usharika gani, uongo wa mwaka huu. Mzee wangu kalazwa zaidi ya mara tatu hospitali hiyo na kupatiwa huduma nzuri sana za upasuaji wa kibofu na hata mara moja hakuwahi kuulizwa dini yake.
Mtu anayejiita kiongozi wa kidini kutoa madai ya uongo kama haya anajifedhehesha binafsi ambalo si jambo baya sana bali anafedhehesha dhehebu analojidai kulipigania.
tatizo lipo NECTA...kila mwaka kuna kufuta matokeo..nani kachukuliwa hatuwa? nani kawajibika? kwanini wasi juuzulu?kwa nini kimya cha vyombo vya habari kuhusu hili? kwa ufupi kuna zengwe ndani ya NECTA..sasa kama ni uchunguzi si ufanywe tu ? kuna big deal gani?
wao wanahisi kuna namna..ni wajib wa NECTA itoke safi wajibu ni kwa vipi kuna wana funzi kweli wlibadilishiwa alama zao baada ya kuu apeal?
ni madai ya halaali yanayopaswa kuchukuliwa kwa uzito....
kuna ushahidi wa kutosha ya kwamba shule ya Millenium ya Kikatoliki ambao walitokea wa 2 kwenye mitihani iliyopita waliweka text books chooni na wanafunzi wakienda ku copy na kuwapa wanafunzi wenzao...jawabu zao wote zina fanana lakini NECTA hawakuthubutu kuumudhi Pengo...walifaulu wote!!!! lakini nawajua ambao wamefaulu lakini hamna kitu kichwani..na katika shule hiii msimamizi wa mitihani alikua na mimba na alikua akilala tu ....kama mtu anabisha kutoka hiyo shule aje hapa nitoe ushahidi
sasa madai haya ya kina ponda ni ya kweli kwa minajali hii sasa kufanya uchunguzi huru ni jambo la kawaida sio issue...lakini kukataa ni kuhalalisha yanayosemwa na ndio mwanzo wa vurugu
kwa nini watu wanao gopa vivuli?