Serikali, shughulikieni akina 'Sheikh Ponda' haraka sana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali, shughulikieni akina 'Sheikh Ponda' haraka sana

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by thatha, Jun 4, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Naiasa serikali ichukue haraka hatua za kudhibiti siasa kali za kidini huku bara kama ambazo tayari zimezusha vurugu Zanzibar. Sheikh Ponda na mujahidina wenzake pia wanakusudia kuleta vurugu kama za Zanzibar kwa kisingizio cha NECTA na sensa ya watu na makazi. Nimewaona leo asubuhi CHANNEL TEN katika kipindi cha baragumu ponda na mwenzie simkumbuki jina wakitoka mapovu na alot of unfounded claims.

  Kwa kifupi ni watu waliokusudia kuivuruga nchi kwa udini, ninaloweza kuwaambia na nina hakika nalo haitatokea siku nchi hii ikaongozwa kidini kama anavyotaka ponda na wenzie. Tatizo lililopo NECTA kwa mujibu wa waheshimiwa hawa ni uwepo wa katibu mtendaji mkristo na mwenyekiti wa bodi mkristo, lakini waziri wa elimu na katibu mkuu wake kuwa waislamu si tatizo hata kidogo.

  Dini zetu zinakuwa na maana na manufaa kwa waumini wake na taifa kwa ujumla kama zinajishughulisha na masuala ya maendeleo ya kijamii ya waumini wake. Kama dhehebu linafumbia macho masuala ya elimu na afya za wafuasi wake ni wazi litakumbwa na matatizo, mi mwislamu lakini sisiti na siogopi kuwasifia wenzetu wakristo na hasa wakatoliki kwa jinsi wanavyowekeza katika masuala ya afya na elimu kwa kujenga hospitali na shule na vyuo kadha wa kadha. Sisi tuna chuo kikuu kimoja tu na si cha kujenga wenyewe bali kupewa bure na serikali wenzetu wamejenga wenyewe vyuo takribani kumi, ni vipi tunataka tufanane na watu kama hao? Angalia uendeshaji wa shule zao mfano Kifungilo, marian, St Francis hivi kweli unaweza linganisha na uendeshaji wa Kinondoni muslim, haramain au jumuiya? Waislamu wenzangu tunaokitakia mema kizazi chetu tupeleke wanetu kwenye shule za kweli zenye walimu,vifaa na usimamizi wa kutosha bila kujali wamiliki wake ni wa ibada gani.

  Tuwaandalie wanetu mazingira mazuri ya ushindani hapo baadaye kwa kuwapa elimu bora. Mwenzie Ponda anadai eti hospitali za kikristu zinabagua, katoa mfano wa KCMC kuwa mgonjwa ukifika unaaulizwa unatoka usharika gani, uongo wa mwaka huu. Mzee wangu kalazwa zaidi ya mara tatu hospitali hiyo na kupatiwa huduma nzuri sana za upasuaji wa kibofu na hata mara moja hakuwahi kuulizwa dini yake.

  Mtu anayejiita kiongozi wa kidini kutoa madai ya uongo kama haya anajifedhehesha binafsi ambalo si jambo baya sana bali anafedhehesha dhehebu analojidai kulipigania.
   
 2. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mwenye masikio atakuwa amekusikia na kukuelewa. Kuna watu wamevimbiwa amani iliopo.
   
 3. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Huyu sheikh ni mwepesi mno,
   
 4. Lyceum

  Lyceum JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2012
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  Akawaulize kina Makamba na wengine wengi walisoma wapi. Ponda anakosea kujitafutia umaarufu kitoto.
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  Jun 4, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Kuna maandishi yanasema wazi tu atakayeua kwa upanga naye atauwawa kwa upanga. Tuendelee na hizi mbio zetu za kuichafua Tanzania tuone nani atakayekuwa muathirika mkubwa wa matokeo yake. Sifikirii kama kweli nia yetu ni kueneza dini ya Mwenyezi Mungu tutatumia uongo kukidhi haja ovu za mioyo yetu.
   
 6. t

  thatha JF-Expert Member

  #6
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Kweli mkuu hata mi nimewaona, ni pumba mwanzo mwisho. Ila namsifu sana mtangazaji wa channel ten jina simjui. Alijitahidi sana kuwabana kwa maswali mazito mazito wakawawanaishia kujikanyaga. Huyo aliyekuwa na ponda ndiyo mufilisi kabisa na kujitia kuongea maneno kadhaa ya kidhungu ambayo kumbe hajui ni lugha ya haohao asiowapenda.

  Jamaa wamechoka mpaka wanatia huruma eti kipengere cha kuulizwa dini kisipowekwa kwenye sensa waislamu wote wagomee sensa. Kama unaamini dini yako ndiyo kubwa zaidi nchini onyesha hilo kivitendo (hospitali, shule na vyuo)kama anavyoshauri kisimajongoo na si wingi wa wapiga ramli Mbagala na kwingineko ambao wanafahamika ni wa dini gani. Nyambafu!!!
   
 7. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #7
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 25,563
  Likes Received: 16,531
  Trophy Points: 280
  Pale pa kukosoa tukosoe na pale pa kuelimisha tuelimishe.Kisima jongoo unastahili pongezi kwa kuelimisha umma.Tusiangalie dini gani tunatoka tuangalie tunafaida gani kwa jamii yetu tuwe wakristu au waislamu.Ukristu na uislamu ziwe ndio chachu ya kuleata ushirikiano na amani sababu tunaamini wote kwa mungu mmoja hakuna mwenye mungu tofauti na yule aliyetuumba.
   
 8. t

  thatha JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Mkuu I salute, umeliweka vizuri sana! cha kuongeza waambie wagomee na vitambulisho vya taifa maana fomu haziulizi dini na bosi wake ni mkristo Dickson Maimu.
   
 9. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #9
  Jun 4, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Badala ya kupendana na kuheshimiana sababu ya tofauti hiyo, naona kuna nguvu kubwa inatumika kuonyesha kuwa moja ya dini ina nguvu kuliko nyingine...sijui wanapima kwa kutumia kigezo gani? watanzania wenzangu, hivi lini tumeanza kujenga urafiki na shetani? Naona tumeanza kucheka naye kwa kujidanganya tutakuwa safe na tutakwenda mbinguni...sijui kama hilo litawezekana kama tutaanza kupigana na kuuana kwasababu ya akili za watu wachache wapuuzi.
   
 10. Mohamed Said

  Mohamed Said Verified User

  #10
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 2, 2008
  Messages: 10,763
  Likes Received: 5,753
  Trophy Points: 280
  TUJIKUMBUSHE
  “Baada ya kupatikana uhuru, Kanisa lilipohisi wasiwasi, limeweza kwa urahisi kabisa kuwazuia na kuwadhibiti Waislam. Serikali imeweza kutumia nguvu iliyokuwanayo katika kudhibiti siasa kuzuia harakati za Waislam kudai fursa sawa na Wakristo katika kugawana madaraka katika serikali. Kanisa limehakikisha kuwa kupinduliwa kwa ukoloni si kizingiti kwa Ukristo, ingawa ingetegemewa kuwa Kanisa lingeathirika kwa kuanguka kwa ukoloni. Katika miaka yake zaidi ya mia moja, Kanisa lilikuwa limestarehe kama muokozi wa nafsi na watu wenyewe. Kanisa lilikuwa salama na halikupambana na msukosuko wowote kutoka kwa serikali kwa kuwa lilikuwa Kanisa ndilo lilishika hatamu ya serikali.

  Baada ya kueleza hayo yote ni muhimu sasa kuangalia jinsi ukereketwa wa Kikristo unavyofanya kazi katika serikali na jinsi kazi hiyo inavyoathiri Uislam. Wizara ya Elimu inachukuliwa kama mfano kwa sababu ya umuhimu wake katika jamii. Katika wizara hii, inaweza kuonekana kwa uwazi kabisa jinsi Ukristo unavyofanya kazi na jinsi udini ulivyoshamiri katika kugawa nafasi muhimu kati ya Waislam na Wakristo. Ilikuwa katika wizara hii katika historia ya Tanzania ndipo kwa mara ya kwanza waziri Muislam alipochaguliwa kuongoza wizara, Kanisa likaingilia kati waziwazi kumpiga waziri vita na kuhoji nafasi nyingine za juu ambazo zilipewa Waislam. Serikali haikuweza kupingana na Kanisa na waziri huyo, marehemu Profesa Kighoma Ali Malima aliondoshwa katika wizara hiyo. Mwaka 1987 Profesa Malima aliteuliwa kuwa Waziri wa Elimu akiwa Muislam wa kwanza kushika nafasi hiyo. Mawaziri 8 waliopita walikuwa Wakristo. Kulikuwa na malalamiko kutoka kwa Waislam kuwa wizara hiyo imegeuzwa jimbo la Wakristo, hasa pale padri alipoteuliwa na Julius Nyerere kuongoza wizara hiyo. Profesa Malima aliposhika wizara hiyo aliona upo umuhimu wa kufanya marekebisho kadhaa ili kurejesha imani ya Waislam katika serikali na wizara hiyo.

  Kulikuwa na tuhuma kuwa Wizara ya Elimu ilikuwa ikiwabagua vijana wa Kiislam kupata nafasi katika vyuo vya elimu ya juu na ilikuwa ikizuia kupanda vyeo kwa Waislam.
  Profesa Malima alipoona dhulma ile iliyokuwapo katika wizara ile dhidi ya Waislam, Profesa Malima aliwateua Waislam 4 kushika nafasi katika kurugenzi mbalimbali na akaandika taarifa ya siri kwa Rais Ali Hassan Mwinyi kumtaarifu udini alioukuta katika wizara ile. Katika taarifa ile kwa rais, Profesa Malima alieleza kuhusu kudumazwa kwa Waislam katika mgao wa elimu. Taarifa hii ilivuja kwa vyombo vya habari na kwa Wakristo wengine. Katika watu walioipata taarifa hii ni Rais Mstaafu Julius Nyerere wakati ule akiwa Mwenyekiti wa chama tawala CCM.”Kutoka kitabu: “Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes…”


  Kutoka kitabu "Mwembechai Killings" cha Prof. Hamza Njozi:

  "In 1987 the then Minister for Education and Culture the late Professor Kighoma Malima discovered that deserving Muslim candidates were deliberately being denied access to secondary education.(It is curious to note that throughout his 25 - year rule, Nyerere had always appointed a Christian to head the Ministry of Education and a Muslim to head the Ministry of Home Affairs.)

  The trick used by the Christian dominated panel was to select the candidates after decoding their examination numbers. Professor Malima directed the panel to select and announce the results using examination numbers only. In that year the percentage of selected Muslim candidates rose by 40 per cent! He alerted the president about the matter and suggested a thorough investigation be carried out. He was branded “Mujahidina” and removed from that portfolio and the selection panel reverted to its old system. He repeated those charges at a public rally in Dar es Salaam in 1995. Any government which is “fiercely secular” would certainly wish to know the truth of the matter.

  Apparently there was no need for the government to investigate the obvious. On July 7, 1999 Muslim leaders paid a courtesy call to President Mkapa at the State House in Dar es Salaam. In the course of their informal discussions Muslims raised the issue of decoding examination numbers. According to my informant the president was clearly surprised. When he asked his Minister for Education and Culture who also attended the talks, the minister confirmed the Muslims’ account. As a result one of the numerous but supposed “isolated” cases came to light in January 1999.

  A Muslim candidate one Adam Ramadhani Kindenge of Gilman Rutihinda primary school was not selected. His father disputed the fairness of the selection process and demanded to be shown the scripts. It was an embarrassing case. Christian candidates with lower points were selected and Adam who had higher points was left out. No one in the ministry could hazard an explanation. The case was disconcerting in view of Kitwana Kondo’s question in Parliament. But it was a case which like others in the past the ministry managed to suppress. For details see Ramadhani Kindenge’s two letters to the Ministry of Education and Culture (1999).

  Despite protests from Muslims, the same ministry had also successfully managed to hide from many unsuspecting Tanzanians another discomfiting letter bearing Ref. No. E10/MMC-1/183 of 9 June, 1998 from the Morogoro Municipal Education Officer directing all Headteachers to submit to that office the names of all Standard Seven Catholic students! When a weekly Muslim newspaper An-Nuur confronted the ministry with that letter the spokesperson was too embarrassed to comment. He promised however to investigate the matter. A time-tested device of dropping a hot potato!

  Adam Kindenge’s case above is not an isolated one. Muslims have a long list of such cases. The name of a selected Muslim candidate, Kopa Abdallah of Kichangani primary school, in Kilosa was in 1983 unfairly cancelled out in favour of a Christian, Mr. Anthony Samirani who scored less points. Mr. Kopa is today employed as a driver. Was it merely a case of corruption? In his long career as a Secondary School Headmaster and later as a high ranking civil servant, Mr. Bori Lilla was twice confronted with incredible discoveries of religious discrimination in the country. Mr. Bori Lilla is today one of the highly respected Muslim elders in the country and is affectionately referred to as “Mzee Lilla”.

  He told me and he has repeated this account to many others that he was once in the marking and selection committee and was mistaken for a Christian. After marking the scripts he decoded and recorded the names according to their pass marks, and there were as many Muslims as there were Christians. A fellow panelist who was a Christian saw the list and was very furious, he said in a loud voice, “Wewe huoni kama orodha yako ina Waislamu wengi sana, au wewe ni mgeni nini hapa?” (Don’t you see that your list has so many Muslims, or could it be that you are a new comer here?). Mzee Lilla says that he responded in an equally loud voice, “Mimi siyo mgeni, mimi ni Muislamu”. The room was gripped with an eerie silence.

  Mzee Lilla witnessed the second revelation of deliberate religious discrimination when he was in the selection panel for allocating High School places for deserving Ordinary Level candidates. It was during the Islamic holy month of Ramadhan and they had almost finished their task when Christian panelists broke for lunch. The panel had only two Muslims who stayed behind. The other Muslim panelist, Mr. Abdulrahman Mwalongo, was writing something and needed a ruler which was in the Chairperson’s draw.

  When he opened it he found along with the ruler, a list of 25 First class Muslim candidates who had not yet been allocated any place in High Schools while all their Christian counterparts had already been placed. And the panel’s chairperson who was also a Reverend had not even hinted that there was such a list. Mwalongo is from the Hehe ethnic group. And the Hehe are known in Tanzania as fierce warriors. When their colleagues returned, Mwalongo reminded the chairperson about the list in his draw. He brushed aside Mwalongo’s concern saying that those candidates would be taken care of later.

  Quite unexpectedly,Mwalongo banged his table so forcefully that all members were taken aback. Shaking with rage Mwalongo told the chairperson no business would take place in that room before the allocation of the 25 Muslim students. The chairperson backed down and those students were placed. In July 1997 I cross-checked Mzee Lilla’s account with Mwalongo himself. He confirmed the story. As I am writing this book, both of them are still alive and can easily be contacted for further details."

  Baada ya kuonekana ukweli huu katika kitabu serikali ya Benjamin Mkapa ilikipiga marufuku.

  Ndugu yangu mambo ya kushughulikiwa siyo akina Ponda utakuwa unamuua mjumbe mambo ya kushughulikiwa ni haya haya hapo chini kwani hayo ndiyo yaliyowaleta Sheikh Ponda, Ali Basaleh, Prof. Hamza Njozi, Warsha, Uamsho, Baraza Kuu la Jumuia na Taasisi za Kiislam na vikundi lukuki. Hebu soma hii uone dhulma na haya yamesemwa kabla ya haya yaliyofichuliwa hivi karibuni katika NECTA:
   
 11. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #11
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Nilisikia mhadhara wa Ponda pale UDOM pale walikuwa wanaonyesha wako karibu kabisa na viongozi wakuu wa serkali. walitaja baadhi ya mawaziri. Binti mmoja aliuliza ikiwa rais ana taarifa ya mikakati hii muhimu ya kuwainua waislamu akasema anayo.
   
 12. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #12
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ukoo wa Ishmail una balaa mama we acha tu. Kuna siku nilisikia wakisemea ndani ya nyumba yao ya ibada kuwa ile chanjo ya POLIO ni janja ya USA ya kutaka kuwawekea watoto dawa za kuwafanya wasizae kwa hiyo wazazi wawe makini. The same to NGAO na vyandarua vya msaada.

  Bado sijajua ni sifa gani mtu anapata ikifahamika kuwa yeye ndio anaongoza kwa kuzaa bila mpango
   
 13. t

  thatha JF-Expert Member

  #13
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Kesho utaina kwenye gazeti la tzdaima. Hii imekaa kama tamko la mnyika
   
 14. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #14
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ni kawaida ya viongozi wa nchi au jumuiya fulani kubwa kuvipiga marufuku vitabu vinavyosema ukweli. Kwa mfano Kiongozi wa Iran Ayatollah Ally Khomeini alikipiga marufuku kitabu cha Sulman Rushdie; Satanic Verses
   
 15. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #15
  Jun 4, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Mohamed Said,

  Deep down your heart, do you believe waislamu wanaonewa wasiweze kusoma? Kama una evidence kama hizo, na siyo here say this here say that, zilete jamvini. Tukianza kuendesha mambo yetu kwa kuhadithiwa tu tunaweza kabisa kufanya makosa makubwa kwenye maamuzi yetu. Tulianza kuleta chokochoko kwenye utaifa wetu, hakuna atakayesalimika maana ndivyo hovyo tulivyo.

  Umaskini kweli ni kitu kibaya sana na kama hatujui namna ya kupigana na umaskini, ndiyo haya malalamiko yasiyokwisha.

  Naamini katika maisha yangu nimekutana na watu wengi wema na ninawaheshimu sana ambao sio wa dini wala imani yangu. Ntafanya makosa kuchukia kila mtu wakati wenye kutuletea matatizo ni watu wachache tu.
   
 16. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #16
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Chadema uwa wanafurahisha sana linapokuja swala la NECTA wote wanarudi upande wa serikali ya CCM...halafu usema Chadema watachukuwa nchi.
   
 17. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #17
  Jun 4, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,568
  Likes Received: 1,932
  Trophy Points: 280
  Nasikia hata mavazi tunayovaa ni matokeo ya mfumo kistu. Maandamano yatakayofuatia ni ya kupinga wanaume kuvaa suruali badala ya kanzu na msuli.
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Jun 4, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,531
  Trophy Points: 280
  Maalim MS ni funga kazi!.
   
 19. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #19
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Waziri wa Elimu haya madudu huyaoni mimi nashauri utaratibu wa namba kwenye mitihani irudishwe ili kuondoa hii dhana
   
 20. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #20
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Watu mmevimbiwa na amani, subirini muone madhara yake hivi hiyo NECTA kama inapendelea wakristo mbona wadogo na vijan wenzangu wanapiga division ZERO za kufa mtu huku nao ni wakristo, Mbona mm hapa ni mkristo lakini nakumbuka kwenye NECTA yangu ya 4M4 nilipiga F ya kufa mtu kwenye math nawakti mm ni mkristo? Jamani hamjui historia au mnataka mrudishe tena JIHAD kama ilivyokuwa west Afrika kwenye karne ya 19? Kweli watu mna elimu duni kupambanua mambo hivi leo kanisa likisema linasitisha huduma kwney shule na hospitali zao kwa waislamu hiv patakalika kweli?? Huyo shek ponda waache ujinga au wahamie huko zanzibar na huku ss hapa ni amani tu kwani hata kaka yangu ana mke muislamu alafu wajinga wachache mnaanza chokochoko za udini! Eboo

  THINK BIG'
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...