Serikali sasa kununua mitambo ya DOWANS! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali sasa kununua mitambo ya DOWANS!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kambarage, Feb 25, 2011.

 1. K

  Kambarage Member

  #1
  Feb 25, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sikilizeni WADANGANYIKA wenzangu. January Makamba ni wakala wa mafisadi. Amepewa ubunge na Rostam Aziz na Edward Lowassa ili wamtoe William Shellukindo aliyetoa uamuzi kamati ya ubunge ichunguze Richmond. Pia wamemuweka kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo ya Bunge ya Nishati na Madini ili kufanikisha ufisadi wa Richmond/Dowans na uporaji mwingine mkubwa kwenye umeme na madini.

  Ndiyo maana siku zote January anazungumzia Dowans eti kama mitambo hiyo ndiyo suluhisho pekee la tatizo la umeme Tanzania. Gridi ya taifa ina upungufu wa 230MW. Dowans inaweza kuzalisha maximum 100MW. Hivyo hata Dowans ikiwashwa, mgao wa umeme bado utaendelea.

  Mpango uliopo ni kuwa eti Dowans wajidai wamesamehe kulipwa tozo ya 100bn/- ya ICC halafu wawashe umeme na kuwauzia Tanesco. Lengo ni kusaini mkataba wa miezi 3 na Tanesco wa kununua umeme.

  Baada ya kuisha kwa mkataba huu wa miezi 3, kamati hiyo hiyo ya January itaiagiza Tanesco na Wizara ya Nishati na Madini inunue mitambo ya Dowans ili kukidhi tatizo la nishati.

  Hivyo basi, ule mpango wa kifisadi wa siku nyingi wa kununua mitambo ya DOWANS utarudi kwa mlango wa nyuma na kuungwa mkono na wenyeviti kadhaa wa kamati za Bunge wakiongozwa na January Makamba, Zitto Kabwe, John Cheyo, Augustine Mrema, nk.

  Kweli sisi Wadanganyika tutaendelea kuliwa mpaka kiama chini ya utawala wa CCM na mawakala wao kwenye kambi ya upinzani.
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wenye macho tuliona zamani sana,
  John cheyo ni dalali wa chochote, hata yale matusi na shout bungeni alikua analinda commission yake
  Augustino Mrema ni mgonjwa, anahitaji kutulia nyumbani his brains are done
  January ni dalali, amekua msemaji wa Tanesco, amekua msemaji wa wizara, msemaji wa kamati ya bunge na pia msemaji wa kila fisadi... puppet
  Zitto - nothing to say, he is crazy about money and can do anything hata kama ni kujidhalilisha (boot-licking)

  We have choices.... rise up
   
 3. k

  kayumba JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hiyo mipango yao itakutana na nguvu ya umma!
   
 4. D

  Deo JF-Expert Member

  #4
  Feb 25, 2011
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 1,193
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Kweli january ni mtoto wa nyoka tu. dalali aliyepwa kazi na maagizo. Jiulize alishawahi kusemakwamba wasitumie siasa kwenye kazi ya mitambo ya Dowanas kana kwamba yeye ni electrical egeneer.

  Siku zako januari kwenye siasa zi fupi kama akili zako
   
 5. eliakeem

  eliakeem JF-Expert Member

  #5
  Feb 25, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 2,933
  Likes Received: 1,034
  Trophy Points: 280
  Ni uzao uleule wa nyoka. Lazima atajitahidi kulinda maslahi ya waliomuweka. LAKINI MWISHO WAO UKO KARIBU.
   
 6. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,205
  Trophy Points: 280
  Spidi aliyokuja nayo January ataondoka nayo.
   
 7. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  January ni kenge kati ya mamba
  zitto sasa anataka kuwa simba nzee
  mapesa anatetea chakula
  ngeleja hajui anachofanya
   
 8. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #8
  Feb 25, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180

  Ngeleja yupo uwanjani ila alichokifanya ni kutoa pasi kwa January huku akisubiri arudishiwe mpira na kutufunga goli la kisigino
   
 9. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #9
  Feb 25, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Amaaaaa kweli ipo kazi wadanganyika
   
 10. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #10
  Feb 25, 2011
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  huyu January mimi namuonea huruma sana, anatafuta umaarufu bila kufanya tafakari, yeye toka achukue uenyekiti hoja ni mitambo ya dowans tuu, tena anaongelea suala lile kwa kujiamini sana as if he is well informed, anaonekana anajua nini wenye dowans wanataka na nini wako tayari kufanya kwakuwa amekuwa akiwalazimisha Tanesco waanze majadiliano na dowans na mmiliki ambaye anaonekana amekutana nae....
   
 11. s

  smz JF-Expert Member

  #11
  Feb 25, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi kamati ya january na serikali yake wanapozungumzia ufumbuzi wa tatizo la umeme nchini wanaangalia mitambo ya Dowans tu. Yaani hawana mpya, wanakanyaga mule mule walimokanyaga baba zao. Hivi huyu haoni kabisa kuwa hilo ni bomu. Naomba wfikirie njia mbadala kumaliza hili tatizo. "Let them think beyond the next meal".

  Kwani Tz haiwezi kununua mitambo yake popote mipya hadi wachukue hiyo hiyo ya ndugu zao?? January, chunga spidi yako!!!
   
 12. L

  Log Member

  #12
  Feb 25, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 71
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 15
  Mara nyingi crisis hutengenezwa na wafanya biashara ili wauze bidhaa zao, nafikiri hata huu mgao wa umeme ni crisis iliyobuniwa na Dowans na washirika wao ili wananchi waone kuwa suruhisho la tatizo la mgao ni kuwahasha/ kutumia mitambo ya Dowans. Hebu tazama siku hizi hao washirika wanavyosisitiza kuiwasha na kuitumia mitambo ya Dowans! mimi muono wangu ni kwamba huu mgao hautakwisha mpaka umeme wa Dowans uingizwe ktk gridi ya taifa. Waziri alipata kusema Dar na MWZ kutanunuliwa mitambo ya 100MW kila mkoa lakini mpaka sasa hadithi ni bado ktk mchakato.

  Nawasilisha
   
 13. t

  the ricks Member

  #13
  Feb 25, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  the decision may sound right, but the motive for the decision...i doubt...
   
 14. F

  FUSO JF-Expert Member

  #14
  Feb 25, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,871
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  Chama Kimetekwa ( Makamba kampa ubunge mwanae na uwenyekiti juu wa kamati ya madini na nishati li waendeleze mlo - kadandia hoja ya Dowans aonekane eti mpiganaji kumbe changa la macho)
  Serikali Imetekwa ( JK hana maamuzi yupo yupo tu, as if haelewi kichachoendelea nchini)
  Bunge Limetekwa ( installed Mama makinda na kamati nyeti wamezichukua)

  Mtanzania subiri maumivu kila kona umebanwa.....

  Mafisadi wanaona mbali miaka 200 ijayo - na mtanunua tu service ya Dowans mtake msitake....
   
 15. YanguHaki

  YanguHaki Senior Member

  #15
  Feb 25, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadanganyika lazima tuelewe kuwa ''CORRUPTION CORRUPTS MIND'' Hao mliowataja wanafikiri na kuzungumza only about DOWANS kwa kuwa uwezo wao wa kufikiri umekuwa damaged na hongo inayoambatana nayo. Akili zao haziwazi namna kutatua tatizo la umeme bali ni namna ya kumtumikia fisadi na kupata Hongo hiyo.
  Hivyo basi hapa tusiwaachie mzigo huu CDM bali Watanzania wote wenye kukerwa na jambo hili tuungane na sauti zetu zisikike. Kwa nini tuache nchi hii mambo yake yapelekwe na wapumbavu wachache wanaotanguliza rushwa. PEOPLEZ POWER
   
 16. F

  FUSO JF-Expert Member

  #16
  Feb 25, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,871
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  Ningekuwa mimi ni Ngeleja nisingekubali kutumika kiashi hicho kwa faida ya watu wachache, kama U GOD father na uende, Wewe ni Kijana mdogo wasikuue kisiasa kwa manufaa yao.

  wao wako ki fedha zaidi - kwa sasa wananchi hawana imani na wewe, safari yako ya kisiasa imeingia dosari - Ushauri tu kwako.
   
 17. Mpasuajipu

  Mpasuajipu JF-Expert Member

  #17
  Feb 25, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 838
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kama serikali yetu ina busara ni vyema kuachana na hii mitambo ya DOWANS.


  1.Kwanza sheria ya manunuzi hairuhusu kununua vitu chakavu (mitumba) na kwa sasa mitambo ya DOWANS ni mitumba haitakiwi kununuliwa kwa fedha za walipa kodi.

  2. J Makamba anaonekana msomi asiyeelimika na anatumia nguvu nyingi kuliko akili, jambo dogo tu la kufikiria, kama kweli serikali ina nia ya kununua mitambo ingeweza kununua mitambo mipya kabisa tena pengine ya kisasa zaidi kuliko hii ya DOWANS.

  HATUHITAJI MGWATT. 100 tunataka zaidi ya hizo ili kukidhi mahitaji ya umeme kwa nchi nzima na siyo Dar es salaam pekee.

  3. Inaonyesha wazi kabisa kuwa kamati nzima imerubuniwa na 10% na ndiyo hiyo wanapigania usiku na mchana, na pengine tayari wameshatanguliziwa KILEGEZA KOO sasa wana haha kutetea FISADI mwenzao apate hiyo tenda.

  4. Watanzania ni watu wa KUKURUPUKA KAMA NDEGE KIOTANI, yaani kila jambo kukurupuka tuuu, halafu kufuata upepo kama manyoya na bendera. Badala ya kufikiria mahitaji ya umeme ya miaka 300 ijayo, watu wanafikiria eti tupate umeme kesho halafu....?

  Ndiyo maana unakuta mipango mingi sana ya KITANZANIA haitekelezeki.
  Wabongo ni wazuri sana katika planning lakini utekelezaji ni ZEROOOOO.

  PLAN ZETU WAKIZICHUKUA WENZETU NA KUZIFANYIA KAZI HUWA ZINAWANUFAISHA SANA, mfano mzuri ni mpango wa makao makuu DODOMA ambao Wanigeria waliuchukua na kuumodify na kujenga mji wa kisasa kabisa wa Abuja, ukweli ukifika Abuja utapenda sana. Sie tunaimba tu makao makuu makao makuu, sasa yamekuwa MAKALIO MAKUU HOVYOOOO, MJI HOVYOOOO, MIUNDOMBINU HOVYOOOOO KILA KITU HOVYOOOO!

  Mfano mwingine ni wa BOMOA BOMOA inayoendelea sasa, iwe kupisha ujenzi wa barabara, kujenga viwanda n.k.

  Hivi wale walioplan mwanzo WAKO WAPI? JAMANI, yaani kama wajinga vile, tunaona kabisa sehemu inajengwa isivyo kihalali tunanyamaza, eti baada ya miaka 50 tunaibuka kama vicheche kutoka shimoni na kudai kuwa hapo hapakujengwa kihalali na kuanza kuwavunjia watu nyumba zao. Hizi mie naona ni akili za Kizezeta.

  Nasema haya kwa uchungu sana nikiwa na mie Mtanzania. Sina dhamana kubwa sana kazini lakini sehemu ninayofanyia kazi naona kabisa naimudu na ninafuata misingi na taratibu za kazi. Baadhi ya wenzangu huniona mnoko lakini bora iwe hivyo kwani HASARA TUNAYOIPATA TZ INATOKANA NA ''INDIVUDUAL PEORSON", YAANI MTU MMOJA NATOA MAAMUZI YASIYO SAHIHI NA KUATHIRI WATU MILIONI 40 JUST THINK ABOUT THIS!

  NASEMA TENA, YAANI JITU MOJA LENYE UROHO, TAMAA NA KIBURI LINAHARIBU MAISHA YA WATU MILIONI 40 KWA FIKRA ZAKE POTOFU.
  HALAFU JITU HILO HILO ETI LINAENDA KANISANI AU MSIKITINI AU LINAABUDU CHOCHOTE KILE!

  USHAURI WANGU:

  1. Wa TZ tutulize vichwa tupange vitu vinavyoendana na wakati na kuzingatia wakati ujao wa vizazi vyetu la sivyo tutazidi kulalamika mpaka tunaingia kaburini na hata huko ahera tutalamika tu.
  2. Hasa wale wenye dhamana zenu, hebu kila unapotaka kufanya jambo litafakari kwa undani na siyo kukurupuka tu kama ndege na kutoa maamuzi yasiyo ya haki.

  3.Asilimia kubwa ya Viongozi Wa TZ ni WATU WASIOPENDA 'KUSHARE' IDEAS NA WALE WANAOWAONGOZA. Yaani hujiamulia mambo wakiwa mezani peke yao bila kuwashirikisha watu/wafanyakazi wa ngazi ya chini. wanasahau kuwa wale wanaowaongoza pengine wana akili na maarifa kuwazidi wao, cheo ni dhamana tu hata mbumbumbu anaweza kupewa. basi ni vyema kujenga tabia ya kuwashirkisha wafanyakazi wa ngazi ya chini ambao wanaweza kutoa ushauri mzuri na wenye tija kwa Taifa.

  Baadhi ya taasisi huendesha mikunano ya ndani ya wafanyakazi kila wiki ili kupata michango na maoni yao, taasisi kam hizi hufanikiwa sana.

  Ninayo mengi sana ya kusema, lakini naona bora niishie hapa nisiwachoshe.

  TAFADHALI NAOMBA MTOE MAONI TU KWANI HAYA NI MAWAZO YANGU BINAFSI NA SIMLAZIMISHI MTU KUFUATA MSIMAMO WANGU.
  Ahsanteni-
   
 18. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #18
  Feb 25, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  hili linawezekana maana huyu dogo anapenda na anashabikia sana hii mitambo......

  kwa hili watatubebea kenye uma... ni mpuuzi sana huyu dogo
   
 19. chipanga

  chipanga JF-Expert Member

  #19
  Feb 25, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 661
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 60
  anaelewa vizuri sana, yy ndo kamisaa wa mchezo!!
   
 20. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #20
  Feb 25, 2011
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Kununua au kuwasha mitambo ya Dowans kwa sasa sio tatizo.
  Tatizo kubwa ni je mitambo hiyo itamaliza kero ya umeme kwa asilimia ngapi.
  Je mkataba/bei yake itakuwa kwa maslahi ya taifa,kwamba hakutakuwa na kasoro au rushwa ambayo italiingiza taifa kwenye matatizo mengine?
  Mwisho:
  Kabla ya kuamua kununua au kukodi mitambo hiyo,TANESCO au Serikali iwachukulie hatua kali wale waliotufikisha hapa tulipo sasa na matatizo ya DOWANS ili iwefundisho kwa watakao deal na DOWANS sasa.
   
Loading...