Serikali sasa kununua mitambo ya DOWANS!

Serikali sasa kununua mitambo ya DOWANS!

Wenye macho tuliona zamani sana,
John cheyo ni dalali wa chochote, hata yale matusi na shout bungeni alikua analinda commission yake
Augustino Mrema ni mgonjwa, anahitaji kutulia nyumbani his brains are done
January ni dalali, amekua msemaji wa Tanesco, amekua msemaji wa wizara, msemaji wa kamati ya bunge na pia msemaji wa kila fisadi... puppet
Zitto - nothing to say, he is crazy about money and can do anything hata kama ni kujidhalilisha (boot-licking)

We have choices.... rise up
sio kwenye udaku ila ngoja nicheke hahahahaha,no komment
 
Sikilizeni WADANGANYIKA wenzangu. January Makamba ni wakala wa mafisadi. Amepewa ubunge na Rostam Aziz na Edward Lowassa ili wamtoe William Shellukindo aliyetoa uamuzi kamati ya ubunge ichunguze Richmond. Pia wamemuweka kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo ya Bunge ya Nishati na Madini ili kufanikisha ufisadi wa Richmond/Dowans na uporaji mwingine mkubwa kwenye umeme na madini.

Ndiyo maana siku zote January anazungumzia Dowans eti kama mitambo hiyo ndiyo suluhisho pekee la tatizo la umeme Tanzania. Gridi ya taifa ina upungufu wa 230MW. Dowans inaweza kuzalisha maximum 100MW. Hivyo hata Dowans ikiwashwa, mgao wa umeme bado utaendelea.

Mpango uliopo ni kuwa eti Dowans wajidai wamesamehe kulipwa tozo ya 100bn/- ya ICC halafu wawashe umeme na kuwauzia Tanesco. Lengo ni kusaini mkataba wa miezi 3 na Tanesco wa kununua umeme.

Baada ya kuisha kwa mkataba huu wa miezi 3, kamati hiyo hiyo ya January itaiagiza Tanesco na Wizara ya Nishati na Madini inunue mitambo ya Dowans ili kukidhi tatizo la nishati.

Hivyo basi, ule mpango wa kifisadi wa siku nyingi wa kununua mitambo ya DOWANS utarudi kwa mlango wa nyuma na kuungwa mkono na wenyeviti kadhaa wa kamati za Bunge wakiongozwa na January Makamba, Zitto Kabwe, John Cheyo, Augustine Mrema, nk.

Kweli sisi Wadanganyika tutaendelea kuliwa mpaka kiama chini ya utawala wa CCM na mawakala wao kwenye kambi ya upinzani.
He! Kumbe ni hayo?bac wabongo 2meliwa
 
thanks for ur insight about uozo wetu wa tz.
well taken and appreciated
Kama serikali yetu ina busara ni vyema kuachana na hii mitambo ya DOWANS.


1.Kwanza sheria ya manunuzi hairuhusu kununua vitu chakavu (mitumba) na kwa sasa mitambo ya DOWANS ni mitumba haitakiwi kununuliwa kwa fedha za walipa kodi.

2. J Makamba anaonekana msomi asiyeelimika na anatumia nguvu nyingi kuliko akili, jambo dogo tu la kufikiria, kama kweli serikali ina nia ya kununua mitambo ingeweza kununua mitambo mipya kabisa tena pengine ya kisasa zaidi kuliko hii ya DOWANS.

HATUHITAJI MGWATT. 100 tunataka zaidi ya hizo ili kukidhi mahitaji ya umeme kwa nchi nzima na siyo Dar es salaam pekee.

3. Inaonyesha wazi kabisa kuwa kamati nzima imerubuniwa na 10% na ndiyo hiyo wanapigania usiku na mchana, na pengine tayari wameshatanguliziwa KILEGEZA KOO sasa wana haha kutetea FISADI mwenzao apate hiyo tenda.

4. Watanzania ni watu wa KUKURUPUKA KAMA NDEGE KIOTANI, yaani kila jambo kukurupuka tuuu, halafu kufuata upepo kama manyoya na bendera. Badala ya kufikiria mahitaji ya umeme ya miaka 300 ijayo, watu wanafikiria eti tupate umeme kesho halafu....?

Ndiyo maana unakuta mipango mingi sana ya KITANZANIA haitekelezeki.
Wabongo ni wazuri sana katika planning lakini utekelezaji ni ZEROOOOO.

PLAN ZETU WAKIZICHUKUA WENZETU NA KUZIFANYIA KAZI HUWA ZINAWANUFAISHA SANA, mfano mzuri ni mpango wa makao makuu DODOMA ambao Wanigeria waliuchukua na kuumodify na kujenga mji wa kisasa kabisa wa Abuja, ukweli ukifika Abuja utapenda sana. Sie tunaimba tu makao makuu makao makuu, sasa yamekuwa MAKALIO MAKUU HOVYOOOO, MJI HOVYOOOO, MIUNDOMBINU HOVYOOOOO KILA KITU HOVYOOOO!

Mfano mwingine ni wa BOMOA BOMOA inayoendelea sasa, iwe kupisha ujenzi wa barabara, kujenga viwanda n.k.

Hivi wale walioplan mwanzo WAKO WAPI? JAMANI, yaani kama wajinga vile, tunaona kabisa sehemu inajengwa isivyo kihalali tunanyamaza, eti baada ya miaka 50 tunaibuka kama vicheche kutoka shimoni na kudai kuwa hapo hapakujengwa kihalali na kuanza kuwavunjia watu nyumba zao. Hizi mie naona ni akili za Kizezeta.

Nasema haya kwa uchungu sana nikiwa na mie Mtanzania. Sina dhamana kubwa sana kazini lakini sehemu ninayofanyia kazi naona kabisa naimudu na ninafuata misingi na taratibu za kazi. Baadhi ya wenzangu huniona mnoko lakini bora iwe hivyo kwani HASARA TUNAYOIPATA TZ INATOKANA NA ''INDIVUDUAL PEORSON", YAANI MTU MMOJA NATOA MAAMUZI YASIYO SAHIHI NA KUATHIRI WATU MILIONI 40 JUST THINK ABOUT THIS!

NASEMA TENA, YAANI JITU MOJA LENYE UROHO, TAMAA NA KIBURI LINAHARIBU MAISHA YA WATU MILIONI 40 KWA FIKRA ZAKE POTOFU.
HALAFU JITU HILO HILO ETI LINAENDA KANISANI AU MSIKITINI AU LINAABUDU CHOCHOTE KILE!

USHAURI WANGU:

1. Wa TZ tutulize vichwa tupange vitu vinavyoendana na wakati na kuzingatia wakati ujao wa vizazi vyetu la sivyo tutazidi kulalamika mpaka tunaingia kaburini na hata huko ahera tutalamika tu.
2. Hasa wale wenye dhamana zenu, hebu kila unapotaka kufanya jambo litafakari kwa undani na siyo kukurupuka tu kama ndege na kutoa maamuzi yasiyo ya haki.

3.Asilimia kubwa ya Viongozi Wa TZ ni WATU WASIOPENDA 'KUSHARE' IDEAS NA WALE WANAOWAONGOZA. Yaani hujiamulia mambo wakiwa mezani peke yao bila kuwashirikisha watu/wafanyakazi wa ngazi ya chini. wanasahau kuwa wale wanaowaongoza pengine wana akili na maarifa kuwazidi wao, cheo ni dhamana tu hata mbumbumbu anaweza kupewa. basi ni vyema kujenga tabia ya kuwashirkisha wafanyakazi wa ngazi ya chini ambao wanaweza kutoa ushauri mzuri na wenye tija kwa Taifa.

Baadhi ya taasisi huendesha mikunano ya ndani ya wafanyakazi kila wiki ili kupata michango na maoni yao, taasisi kam hizi hufanikiwa sana.

Ninayo mengi sana ya kusema, lakini naona bora niishie hapa nisiwachoshe.

TAFADHALI NAOMBA MTOE MAONI TU KWANI HAYA NI MAWAZO YANGU BINAFSI NA SIMLAZIMISHI MTU KUFUATA MSIMAMO WANGU.
Ahsanteni-
 
Ulilolisema ni kweli maana huyo ni WAZIRI na mwingine ni mwenyekiti tu wa kamati
Kuna utofauti mkubwa sana wa majukumu Ngeleja akiwa ndio serikali hakupaswa huwa very lo kiasi hicho..
hapo ni kumalizwa kisiasa kabisa
anyway aliyataka mwenyewe alipokubali kutumiwa na kuwadanganya bibi zake kule Kanda ya ziwa kuhusu Dowans
Ningekuwa mimi ni Ngeleja nisingekubali kutumika kiashi hicho kwa faida ya watu wachache, kama U GOD father na uende, Wewe ni Kijana mdogo wasikuue kisiasa kwa manufaa yao.

wao wako ki fedha zaidi - kwa sasa wananchi hawana imani na wewe, safari yako ya kisiasa imeingia dosari - Ushauri tu kwako.
 
Dowans sasa yalainika, wafuta deni kwa Tanesco

Na Richard Makore
headline_bullet.jpg
Sasa wataka walipwe tu Sh. bilioni 36



Januari(4).jpg

January Makamba



Kampuni ya Dowans Tanzania Limited ya kufua umeme wa dharura ambayo ilishinda kesi dhidi ya Tanesco katika Mahakama ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) na kupewa tuzo ya Sh. bilioni 94, sasa imelainika na imetangaza kusamehe deni hilo.
Uamuzi huu ambao unatangazwa baada ya kuwapo kwa malumbano makali nchini juu ya hukumu ya ICC na kiasi cha fedha kilichotolewa, sasa Dowans wanataka Tanesco ilipe tu Dola za Marekani milioni 24 (Sh. bilioni 36 tu). Fedha hizo ni gharama halisi ya umeme uliouzwa kwa Tanesco.
Uamuzi wa Dowans ulitangazwa na Stanley Munai ambaye ni Mkurugenzi wake wa Fedha, akiwa pia mwakilishi wa kampuni hiyo nchini.
Mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Munai alisema kuwa wamechukua hatua ya kufuta deni hilo kutokana na kusikia kilio cha Watanzania.
Hata hivyo Dowans imesema licha ya kutoa msamaha huo, Tanesco bado imeshindwa kujibu kama imeukubali msamaha huo au la ili mazungumzo yaanze.
Munai alidai fedha wanazolidai shirika hilo kwa sasa zinakaribia Sh. bilioni 99 badala ya Sh. bilioni 94 za mwaka jana.
Alisema ongezeko hilo limetokana na kampuni ya Dowans kuitoza Tanesco kila siku Dola za Marekani 11, 800 (Sh. milioni 15.3) kama gharama za kuweka mtambo hata kama hauzalishi umeme na kwamba nyongeza ya gharama hizo ilianza kutozwa kila siku tangu Juni 15, mwaka 2010 hadi sasa.
Alisema deni la Sh. bilioni 94 liliishia Juni 14, mwaka 2010 na baada ya hapo limekuwa likiongezeka siku hadi siku. Munai aliwaambia waandishi wa habari walioambatana na kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuwa kampuni yake haina tatizo kuhusu kusamehe deni hilo, lakini Tanesco muda wote imekuwa haitaki kukubali msamaha huo.
Aliongeza kuwa ikiwa Tanesco na Serikali watakataa kupokea msamaha huo nje ya mahakama na wao wataacha sheria iendelee kuchukua mkondo wake.
Munai alisema mkataba kati ya Dowans na Tanesco unasema kuwa ikiwa pande hizo mbili zitatofautiana na zikaenda kwa msuluhishi maamuzi yatakayotolewa yatatakiwa kuheshimiwa na pande zote na hakuna upande utakaoruhusiwa kukata rufaa.
“Kwa mujibu wa mkataba huu, Tanesco haiwezi kukata rufaa kwa kuwa kipengele hicho kinawazuia na wao wanajua, lakini hajui ni kwanini hawataki kuwaambia wananchi ukweli,” alisema.
Alifafanua kuwa endapo serikali na Tanesco wataendelea na msimamo wa kugoma kupokea msamaha huo wataendelea na utaratibu wa kimahakama ili wapate kibali cha kukamata mali za Tanesco za ndani na nje ili ziuzwe ili kufidia fedha za Dowans.
“Tumewandikia barua Tanesco kwamba tukae meza moja kwa maelekezo ya mmiliki wa Dowans ili tuwasamehe deni, lakini hawataki kujibu, sasa tuwafanyeje?” alihoji Munai.
Alisema Dowans inaidai Tanesco Dola milioni 24 (Sh. Bilioni 31.2) kutokana na kuwauzia umeme kabla ya kuvunjwa kwa mkataba.
Alifafanua kuwa deni la umeme lazima lilipwe kwa kuwa waliwauzia Tanesco nishati hiyo na wakawauzia wateja wao hivyo wana uhakika fedha hizo walizichukua na wanazo.
Mtambo huo wa Dowans jana ulikuwa umezimwa lakini, Munai alibainisha kwamba muda wowote wakitakiwa kuwasha watafanya hivyo.
Alisema mtambo huo una uwezo kuzalisha megawati 120 na kwamba endapo watauwasha una uwezo wa kuanza kuzalisha umeme baada ya dakika 12 tangu kuwashwa.
Wakati huo huo, kampuni ya Dowans imekiri kudaiwa na benki ya Baclays Tanzania Dola za Marekani milioni mbili na kusema kuwa wanaendelea kulipa kama ilivyo kwa wateja wengine wanaokopa katika taasisi za fedha.
Jumapili iliyopita mmiliki wa Dowans, Brigedia Jenerali Mstaafu Suleiman Yahya Al Adawi, alikutana na wahariri wa vyombo vya habari na kueleza kuwa alikuwa radhi kukukana na Tanesco kwa mazungumzo.
Alisema walikuwa tayari kusamehe sehemu ya deni hili kwa masharti wakubaliwe kuendelea kuzalisha umeme.
Wakati huo huo, Kamati ya Nishati na Madini jana ilitembelea mitambo ya gesi ya Tanesco iliyopo Ubungo, mitambo ya Dowans na ya Songas ambayo pia inatumia gesi.
Akizungumza wakati wa kutembelea mitambo hiyo, Mwenyekiti wa kamati hiyo, January Makamba, alihoji ni kwa nini mitambo hiyo ya Dowans isihamishwe eneo la Tanesco kwa kuwa haifanyi kazi.
“Sasa hii mitambo inafanya nini hapa wakati haifanyi kazi na mmeizima au mna malengo gani nayo,” January alimhoji Munai.
Akijibu swali la January, Munai alisema awali walitaka kuondoa mitambo yao lakini Tanesco wakawazuia.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, William Mhando, akizungumzia maamuzi ya Dowans, hakutaka kutoa ufafanuzi badala yake alisema kinachosababisha matatizo yote hayo ni kauli za kisiasa na wanasiasa.
Naye January alipoulizwa kuhusiana na maamuzi ya Dowans, alijibu kwa kifupi kuwa suala hilo ni la Tanesco.
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, hakupatikana kuzungumzia msamaha wa Dowans kutokana na simu zake za kiganjani kuzimwa.
Nipashe
 
Let them do whatever they want to do,hukumu yao ni nguvu ya umma,,watakumbana na nguvu ya umma na hakika hawatakwepa ghadabu hiyo
 
Back
Top Bottom